Kwenye mchezo wa mbio za kuteleza kwenye barafu mita 500 kuzunguka duara dogo kwa wanawake wa michezo ya Olimpiki ya siku za baridi uliofanyika tarehe 15 mwezi Aprili mjini Torino, mchezaji kijana Wang Meng alipata ubingwa, ambayo pia ni medali ya kwanza ya dhahabu uliyopata ujumbe wa China kwenye michezo hiyo. Je, Wang Meng alipata vipi medali hiyo ya dhahabu na je yeye ni mchezaji wa aina gani?
Wang Meng mwenye umri usiotimia miaka 21 ameshiriki kwenye michezo ya Olimpiki ya siku za baridi kwa mara ya kwanza, lakini alikabiliwa na changamoto kubwa ya kubeba jukumu la kupata medali ya dhahabu kwenye mchezo wa mbio za kuteleza kwenye barafu mita 500 kuzunguka duara ndogo kwa wanawake. Kwenye michezo hiyo ya Salt Lake mwaka 2002, mchezaji wa China Yang Yang alipata medali ya kwanza ya dhahabu kwenye mchezo huo kwa michezo ya siku za baridi ya China. Baada ya miaka minne, kiwango cha mchezo huo cha timu nzima ya China kimekizidi kile cha nchi nyingine, kwa hiyo kupata medali ya dhahabu kwenye mchezo huo ni jukumu linalopaswa kukamilishwa na timu ya kuteleza kwenye barafu kuzunguka duara ndogo ya China. Ingawa Wang Meng ameorodheshwa kwenye nambari ya kwanza kwa jumla ya pointi za mashindano ya kombe la dunia ya awamu hiyo ya mchezo huo, na kuchukuliwa kuwa mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kugombea medali ya dhahabu, lakini alikuwa na wasiwasi kutokana na jinsi watu walivyokuwa na matarajio makubwa kwake. Baada ya kushiriki kwenye mchezo huo, Wang Meng alieleza kuwa aliposhiriki kwenye michezo ya Olimpiki kwa mara ya kwanza, alihisi kuwa mambo yote hayakuonekana kama jinsi watu walivyodhani kabla ya hapo na alisema:
"Hii ni safari ya kwanza kwangu kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki ya siku za baridi, nilipohojiwa nchini China kabla ya kufunguliwa kwa michezo hiyo, nilisema kuwa sina shinikizo wala wasiwasi wowote, lakini baada ya kufika kwenye uwanja wa mashindano wa michezo hiyo, niliona kuwa hayo ni mashindano yanayotofautiana sana na mashindano ya kombe la dunia na mashindano ya ubingwa wa dunia."
Kwa kuwa alikuwa na wasiwasi, Wang Meng alihisi kuwa hakutulia tangu tarehe 12 aliposhiriki kwenye mchezo wa awali. Ingawa alijitahidi kutokuwa na wasiwasi mara kwa mara, lakini hali ya michezo ya Olimpiki ya siku za baridi ilimfanya msichana huyo anayefanana kidogo na mvulana awe na hofu kwenye uwanja wa mashindano. Ilipofika tarehe 15, Wang Meng alionekana mwenye wasiwasi zaidi kwenye mashindano ya nusu fainali baada ya kugundua kuwa yeye na wapinzani wake wawili muhimu, Evgenia Radanova wa Bulgaria na Kalyna Roberge wa Canada walipangwa katika kundi moja. Wachezaji bora watatu wako katika kundi moja, lazima mmoja kati yao atatolewa kabla ya fainali, tena Wang Meng alipangwa katika njia ya tatu ambayo si nzuri. Jambo lililowafurahisha ni kuwa wakati huo wasiwasi ulimtoka. Baada ya nusu fainali kuanza, mara aliwapita wapinzani wake wawili, na kuchukua nafasi ya kuongoza na kuingia kwenye fainali bila vikwazo, Kalyna Roberge alitolewa. Kocha mkuu wa timu ya wanawake ya kuteleza kwenye barafu kwa kuzunguka duara ndogo ya China Yi Min aliona kuwa kufuzu kwa Wang Mengi katika nusu fainali sio tu kulimtoa mpinzani mwenye nguvu, bali pia kulipunguza imani ya mpinzani mwingine Evgenia Radanova anayeshikilia rekodi ya dunia na Wang Meng alijiongezea ari ya kushinda. Kocha wake Yi Min alisema:
"Wang Meng alishika nafasi ya kwanza katika nusu fainali, tulikuwa na imani yenye zaidi ya asilimia 50 ya kupata ubingwa".
Ukweli wa mambo unaonesha kuwa ushujaa wa Wang Meng katika nusu fainali uliweka msingi madhubuti kwa fainali. Katika mashindano ya fainali, Radanova hakupata nafasi ya kumzidi Wang Meng, lakini Wang Meng aliyepangwa katika njia mwafaka ya kwanza alisimama kwenye jukwaa la mshindi.
Wang Meng na wazazi wake
Kushinda wasiwasi moyoni na kuwashinda wapinzani wake, kijana Wang Meng alijipatia na kuupatia ujumbe wa China medali ya kwanza ya dhahabu kwenye michezo hiyo ya Olimpiki. Ingawa hakuelewa baada ya kupata ubingwa kuwa kwa nini alikuwa na wasiwasi kwenye mashindano ya michezo ya Olimpiki, lakini wengine walijua kuwa katika mashindano ya siku kadhaa kabla ya hapo, wachezaji wa China wote hawakupata na medali ya dhahabu kwenye michezo yenye fisa ya China yaani mchezo wa kuteleza kwenye barafu kwa vitendo mbalimbali kwa mwanamke na mwanaume, na mbio za kuteleza kwenye barafu mita 500 kuzunguka duara ndogo kwa wanawake. Ujumbe wa China haukupata medali hata moja ya dhahabu katika siku nyingi, jambo ambalo lilimwekea shinikizo Wang Meng. Kupata ushindi katika hali kama hiyo, kocha mkuu wa timu ya mchezo huo ya China Xin Qingshan anaona kuwa, mbali na uwezo mkubwa wa Wang Meng, udhaifu wa wapinzani wake pia ulikuwa ni chanzo cha kupata ushindi kwa Wang Meng na alisema:
"Kuhusu mchezo wa kuteleza kwenye barafu mita 500 kwa wanawake, wachezaji hawakubadilika sana katika miaka miwili iliyopita, kwa mfano Evgenia Radanova mwenye umri wa kukaribia miaka 30 bado amekuwa akicheza mchezo huo kwa miaka mingi na wachezaji wengine wana uwezo mkubwa katika kipindi cha kutoka kwenye kianzio, lakini hawakuwa na uwezo mkubwa kwa jumla, katika nusu fainali, tofauti kati ya wachezaji hao bado ilikuwepo na wachezaji wachache tu walimkaribia Wang Meng na wengine walikuwa na udhaifu mkubwa zaidi kuliko Wang Meng, kwa hiyo tulitabiri mwanzoni kuwa wapinzani wetu si wengi na uwezo wao ni dhaifu kiasi kwenye mchezo huo".
Kwa vyovyote vile, Wang Meng alipata medali ya dhahabu yenye thamani kubwa na kuondoa wasiwasi wa Wachina wote. Baada ya mashindano hayo, msichana huyo alisisimka sana, lakini baadaye alitulia. Alieleza matumaini yake ya kuupatia ujumbe wa China medali nyingine ya dhahabu katika mashindano yatakayofuata kwenye michezo hiyo ya Olimpiki, na alisema:
"Ninapaswa kutulia, kwani kuanzia sasa hadi tarehe 25 tutakuwa na mashindano mengi, bado kuna mashindano matatu ambayo nitashiriki, na shindano muhimu zaidi ni mbio za mita 3000 kupokezana kwa wachezaji wanne wanawake, tunapaswa kufanya mazoezi kwa bidii zaidi na kujipatia medali nyingi zaidi za dhahabu."
Idhaa ya kiswahili 2006-03-02
|