Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-03 16:29:26    
Ushirikiano katika rasilmali kati ya China na Afrika wahimiza maendeleo endelevu ya nchi za Afrika

cri

Wataalamu wa China wanasema, China inapofanya ushirikiano kati yake na nchi za Afrika katika uendelezaji wa rasilmali, inatilia maanani kuzisaidia nchi za Afrika kugeuza sifa ya kuwepo kwa rasilmali nyingi kuwa sifa ya ushindani duniani, ili kuhimiza maendeleo endelevu ya nchi za Afrika.

Serikali ya China tarehe 12 mwezi Januari mwaka huu ilitoa waraka wa kwanza wa sera ya China kwa Afrika, ambao umetoa malengo ya ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta za siasa, uchumi, sayansi, elimu, utamaduni, afya, jamii, amani na usalama. Kuhusu ushirikiano wa rasilmali kati ya China na nchi za Afrika, waraka huo unasema, serikali ya China inahimiza na kuziunga mkono kampuni za China zenye uwezo zishirikiane na nchi za Afrika katika kuendeleza na kutumia vizuri rasilmali kwa kanuni ya kunufaishana na kujiendeleza pamoja?ili kuzisaidia nchi za Afrika kugeuza sifa yake ya kuwa na rasilmali nyingi kuwa sifa ya kushindania soko duniani na kuleta maendeleo endelevu.

Mtafiti wa mambo ya Afrika wa taasisi ya utafiti wa masuala ya kimataifa ya China Bi. Wang Yingying alisema, ingawa katika miaka ya karibuni, uchumi wa Afrika umepata ongezeko fulani, lakini uchumi wa nchi za Afrika bado ni dhaifu, bidhaa nyingi za Afrika zilizosafirishwa nje ni mazao ya awali yasiyosindikwa. China imetoa mafunzo ya aina mbalimbali ya kiufundi kwa watu wa nchi za Afrika, kuzisaidia nchi za Afrika kujenga viwanda vya usindikaji wa mazao ya kilimo ili kuongeza thamani ya nyongeza ya mazao yao na kuinua uwezo wao wa ushindani duniani.

Bi. Wang Yingying alisema, serikali ya China inatilia maanani kuleta maendeleo endelevu kwa nchi za Afrika, hivyo tofauti ya nchi za magharibi, kampuni za China zinapochimba madini barani Afrika pia zinajitahidi kuzisaidia nchi za Afrika kujiendeleza kiuchumi. Kwa mfano serikali ya China inatumia fedha zilizopatikana huko Afrika kuzisaidia nchi hizo kujenga miundombinu, kuanzisha vituo vya kuzalisha umeme ili kuwanufaisha wakazi wa huko na kuleta maslahi halisi kwa watu wa Afrika.

Bi. Wang Yingying alisema, nchi za Afrika zina kiasi kikubwa cha mafuta, chuma, na madini mengine mbalimbali yasiyokuwa ya chuma. Kampuni za China zinapoanzisha viwanda na kuchimba rasilmali kwenye nchi za Afrika pia zinafuatilia hifadhi ya viumbe ya huko.

?? Mkurugenzi wa shirikisho la utafiti wa masuala ya Afrika la China Bwana An Yongyu alisema, rasilmali nyingi zinazozalishwa katika nchi za Afrika zimeingia sokoni kwa bei chini sana kutokana na kutokuwa na sifa kubwa ya ushindani isiyokuwa na haki kwenye soko la kimataifa, na kuleta hasara kubwa za kiuchumi kwa nchi hizo. China inapofanya biashara ya nishati na nchi za Afrika hununua kwa bei halali ya kimataifa.

Bwana An Yongyu alisema, kushikilia maendeleo endelevu ni sera ya taifa la China, ambazo ni pamoja na matumizi halali ya nishati na kuokoa matumizi ya nishati. Wakati China inaposhirikiana na nchi za Afrika katika kuzalisha rasilmali, kampuni za China huzingatia namna ya kulinda uzalishaji endelevu wa rasilmali.

Bw. An Yongyu alifahamisha kuwa, ilipowekeza katika uchimbaji wa makaa ya mawe nchini Tanzania, kampuni ya China inafuata njia ya uzalishaji ya kiwango kikubwa na kuokoa gharama, si kama tu imehakikisha usalama na matumizi ya teknolojia katika uzalishaji, bali pia imehakikisha matumizi halali ya rasilmali. Inapoendeleza rasilmali ya misitu nchini Gabon, kampuni ya China inafuata njia ya kukata miti na kupanda miti, hivyo wakati wa kuzalisha miti na mbao pia imehifadhi maendeleo endelevu ya rasilmali ya misitu.

Bw., An Yongyu alisisitiza kuwa, ukweli wa mambo umeonesha kuwa, serikali ya China inatilia maanani sana maendeleo endelevu ya nchi za Afrika inapofanya ushirikiano na nchi za Afrika katika nishati.

Idhaa ya kiswahili 2006-03-03