Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-07 11:08:26    
China kuharakisha hatua za kuendeleza shughuli za misitu

cri
Ofisa wa Idara ya Misitu ya China tarehe 27 alisema kuwa, katika miaka mitano ijayo, China itaendelea kutekeleza mikakati ya maendeleo ya shughuli za misitu inayoweka mkazo ujenzi wa kufanya viumbe na mazingira ziishi kwa kupatana, kutilia maanani kukuza shughuli za misitu, kuhudumia shughuli za ujenzi wa uchumi na hifadhi ya mazingira, kutosheleza mahitaji ya aina mbalimbali ya watu kwa shughuli za misitu.

Eneo la misitu la China si kubwa ambalo linachukua asilimia 18. 2 tu ya jumla ya eneo la China, kiasi ambacho kiko chini ya kiwango cha wastani duniani. Mkuu wa Idara ya Misitu ya China Bw. Jia Zhibang alisema, China inahitaji kudumisha upanuzi wa eneo la misitu, na kulifanya eneo hilo lifikie asilimia 20 ifikapo mwaka 2010, na kufanya asilimia 50 ya ardhi za oevu na asilimia 90 ya wanyama na mimea pori zihifadhiwe.

Imefahamika kuwa hivi sasa eneo la miti iliyopandwa nchini China limefikia hekta milioni 53, na hifadhi za misitu zimefikia 1700 ambazo kwa jumla zina eneo la hekta milioni 120, kiasi ambacho kimezidi kiwango cha wastani cha dunia, na eneo la jangwa limepungua mwaka hadi mwaka.

Bw. Jia Zhibang anasema: "Tunapaswa kuanzisha utaratibu kamili wa shughuli za misitu, ili kukidhi mahitaji ya watu kwa bidhaa za misitu, na kutoa fedha za kutosha kwa kuimarisha na kuhakikisha ujenzi wa utaratibu wa kupatanisha viumbe na mazingira, na kuimarisha matokeo yake."

Ofisa huyo amesema, eneo kubwa la misitu liko vijijini, hivyo kuharakisha maendeleo ya shughuli za misitu kutachangia kuhimiza maendeleo ya uchumi vijijini, pia kutahimiza kuboresha ujenzi wa kupatanisha viumbe na kuboresha mazingira ya viumbe vijijini, kuongeza mapato ya wakulima na kutoa ajira nyingi zaidi vijijini.

Imefahamika kuwa, hivi sasa mikoa mbalimbali ikiwemo Jiangxi, Fujian na Zhejiang nchini China zimeanzisha utaratibu wa kusaini mkataba na familia moja moja za wakulima ili waendeshe na kujipatia faida. Vitendo hivyo imehamasisha juhudi za wakulima za kufanya uzalishaji. Takwimu zimeonesha kuwa, zaidi ya nusu ya mapato ya wakulima walioko kijiji cha Nanping mkoani Fujian, China yanatokana na shughuli za misitu, na wastani wa mapato wa sehemu hiyo kwenye sekta ya misitu umezidi RMB yuan 5000 kwa watu.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 27, Februali msemaji wa Idara ya misitu ya China Bw. Cao Qingyao alidokeza kuwa, China imefanikiwa kutatua suala la matumizi ya mbao katika maendeleo ya uchumi na maisha ya watu. Bw. Cao alisema, watu kadhaa wa nchi za nje wanaona kuwa, kiasi kikubwa cha mbao kinachoagizwa na China kutoka nchi za nje kimeharibu maliasili ya misitu ya nchi hizo, maoni hayo hayana msingi wowote. Bw. Cao anasema: "Kuhifadhi na kuendeleza maliasili ya misitu ni jukumu la pamoja kwa nchi zote duniani. Serikali ya China ilianzisha ujenzi wa kupatanisha viumbe na mazingira katika shughuli za kuhifadhi misitu ya asili, hatua ambayo inabeba jukumu la kulinda usalama wa viumbe wa China, pia imetoa mchango kubwa kwa ujenzi wa viumbe duniani. China inahifadhi maliasili yake mwenyewe, wakati huo huo inajenga vituo va uzalishaji wa mbao, na tunaweza kutatua mahitaji ya mbao baada ya kufanya juhudi za kuinua sifa nzuri na uzalishaji wa mbao.

Ofisa huyo alisema, serikali ya China siku zote inatekeleza jukumu la pamoja la kimataifa, kupambana kithabiti na ukataji wa miti na uagizaji wa miti kutoka nchi za nje kwa njia haramu, na kufanya usimamizi kwa makini kwa kuagiza mbao kutoka nchi za nje. Licha ya kukamilisha sheria na kanuni za usimamizi wa kuagiza mbao kutoka nchi za nje, China imeongeza nguvu katika utekelezaji wa sheria, na kuanzisha utaratibu wa utekelezaji wa pamoja na nchi kadhaa jirani, na kupambana kwa pamoja na vitendo vya kusafirisha mbao kwa njia haramu.

Idhaa ya kiswahili 2006-03-07