Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-07 18:27:32    
Rais wa Korea ya Kusini atafuta nishati barani Afrika

cri

Rais Roh Moo Hyun wa Korea ya Kusini tarehe 6 aliwasili Cairo na kuanza ziara yake ya kiserikali nchini Misri. Katika ziara yake hiyo pia atatembelea Nigeria na Algeria. Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Korea ya Kusini kutembelea Afrika katika miaka 24 iliyopita. Vyombo vya habari vinaona, tokea mwaka huu viongozi na maafisa wa Korea ya Kusini wametembelea Afrika mara kwa mara na kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi na Afrika, hatua ambayo inaonesha mabadiliko makubwa ya sera za kidiplomasia za Korea ya Kusini. Lengo lake muhimu ni kuongeza njia ya kuagiza mafuta ya asili ya petroli duniani.

Ikulu ya Korea ya Kusini siku hiyo ilisema, lengo kuu la ziara ya Rais Roh Moo Hyun ni kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa nishati na kiuchumi pamoja na nchi hizo. Watu walioufuatana na Rais Roh Mu Hyun katika ziara hiyo ni pamoja na kundi lenye watu 80 kutoka sekta za viwanda na biashara, ambao shauku yao ni kuhusu ujenzi wa miundo mbinu na usafirishaji bidhaa kwa nchi hizo.

Vyombo vya habari vinaona kuwa tokea muda mrefu uliopita Asia lilikuwa ni bara lililozingatiwa zaidi na Korea ya Kusini katika mambo ya kidiplomasia, na hakukuwa na uhusiano mwingi na bara la Afrika kutokana na umbali wa kijiografia na tofauti ya utamaduni. Lakini tokea mwishoni mwa mwaka uliopita, Korea ya Kusini iligeuza ufuatiliaji wake kwa Afrika. Benki ya usafirishaji bidhaa kwa nje na uagizaji bidhaa kutoka nchi za nje, ilisaini mkataba wa ushirikiano wa shughuli za benki na Benki ya Maendeleo ya Afrika mwezi Novemba mwaka jana. Mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu, waziri wa mambo ya kidiplomasia na biashara wa Korea ya Kusini Bw. Ban Ki-moon alitembelea Ghana na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, mwanzoni mwa mwezi Februari waziri mkuu wa Korea ya Kusini Bw. Lee Hae Chan alifanya ziara katika nchi za Afrika ya Kusini na Senegal na kuwa waziri mkuu wa kwanza wa Korea ya Kusini aliyetembelea bara la Afrika. Hivi sasa rais Roh Moo Hyun anafanya ziara katika nchi kadhaa muhimu za Afrika. Vyombo vya habari vya nchi hiyo vinaona kuwa mabadiliko hayo yaliyotokea katika mambo ya kidiplomasia ya Korea ya Kusini hasa yanatokana na mambo mawili ya kisiasa na kiuchumi.

Kisiasa, pamoja na kuimarika kwa nguvu ya Korea ya Kusini, nchi hiyo inataka kufanya kazi muhimu zinazolingana na nguvu yake katika shughuli za kimataifa ili kuinua hadhi yake duniani. Nchi za Afrika ni nguvu moja muhimu katika Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa duniani. Katika shughuli za kimataifa, Korea ya Kusini inahitaji ushirikiano wa Afrika. Hivyo tokea mwaka huu, Korea ya Kusini ilirekebisha sera zake za kidiplomasia ikinuia kuchukulia marekebisho ya sera za kidiplomasia na kutekeleza mambo halisi ya kidiplomasia kuwa moja ya kazi zinazotiliwa mkazo. Hususan ni kuimarisha shughuli za kidiplomasia na viongozi wa nchi za Afrika na sehemu ya mashariki ya kati, aidha imeamua kuimarisha utoaji misaada ya maendeleo ya kiserikali kwa nchi za Afrika ili kuwa karibu zaidi na nchi za Afrika.

Kiuchumi, Korea ya Kusini imetambua kuwa sehemu ya Afrika ni bahari kubwa ya nishati na rasilimali, soko lenye uwezo mkubwa ambao haujatumika na ina mahitaji makubwa katika ujenzi wa miundo mbinu, inaona hadhi ya Afrika duniani itaendelea kuwa muhimu zaidi. Kuimarisha uhusiano na nchi za Afrika kunaweza kuwa na uhakika wa kupata mafuta ya petroli na rasilimali nyingine, na kuanzisha masoko mapya na kupata miradi mikubwa ya ujenzi wa miundo mbinu kwa kampuni na viwanda vya Korea ya Kusini.

Korea ya Kusini ni nchi inayopungukiwa na rasilimali za kimaumbile, mali ghafi za viwanda zinategemea kuagizwa kutoka nchi za nje na 97% ya nishati inayohitaji inaagizwa kutoka nje. Serikali ya Korea ya Kusini ilisema, lengo muhimu la ziara hiyo ya Rais Roh Moo Hyun ni kuimarisha ushirikiano wa nishati na nchi hizo ili kuhakikisha usalama wa nishati wa nchi hiyo.

Maendeleo ya uchumi ya Korea ya Kusini yanategemea usafirishaji bidhaa kwa nchi za nje. Hivi sasa bidhaa zinazosafirishwa nchi hiyo kwa Afrika zinachukua nafasi ya 2.9% tu kati ya bidhaa zake zinazosafirishwa kwa nchi za nje.

Idhaa ya Kiswahili 2006-03-07