Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-08 16:56:48    
Mashine ya kufulia isiyotumia sabuni ya unga

cri

Kama watu wote wanavyojua mashine ya kufulia inategemea sabuni ya unga kufua nguo. Lakini hivi sasa aina mpya ya mashine ya kufulia inayonunuliwa sana nchini China, imevunja kanuni hiyo, na inaweza kufua nguo kama kawaida bila kutumia sabuni ya unga.

Mwandishi wetu wa habari aliona aina hiyo mpya ya mashine ya kufulia katika duka moja kubwa mjini Beijing. mashine hiyo inaonekana kama ya kawaida na rangi yake ya nje ni ya fedha na kifuniko chake ni cha rangi ya kibuluu, inapendeza sana. Mwuzaji alionesha jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi. Alichafua taulo jepesi kwa coke, sosi na siki, halafu aliweka taulo hilo ndani ya mashine hiyo iliyojazwa maji. Baada ya kufua kwa dakika chache tu, taulo hilo likawa safi tena. vipi mashine ya kufulia inaweza kufua nguo bila kutumia sabuni ya unga? mwandishi wetu wa habari alikwenda kuuliza swali hilo kwa shirika la Haier lililosanifu na kutengeneza mashine hiyo. Mkurugenzi wa idara ya utafiti wa mashine ya kufulia ya shirika hilo Bw. Lv Peishi alieleza siri ya mashine hiyo. Alisema:

"mashine hiyo ni tofauti kabisa na mashine ya kufulia ya kawaida kwa muundo na namna inavyofanya kazi. Sehemu yake ya kiini ni electrobath. Hivyo inaweza kufua nguo bila kutumia sabuni ya unga."

Bw. Lv alieleza kuwa, sehemu hiyo ya electrobath inaweza kuchanganua maji ya bomba kuwa maji yenye alkali dhaifu, na uchafu kwenye nguo ni wa siki dhaifu, hivyo mchanganyiko wa kikemikali utaondoa uchafu huo, basi nguo zitakuwa zimefuliwa.

Shirika la Haier lilisanifu aina hiyo ya mashine ya kufulia kutokana na mtizamo wa afya na hifadhi ya mazingira. Kama inavyojulikana, sabuni ya unga ina vitu vingi vya kemikalis, kama vitu hivyo vikibaki kwenye nguo zinaweza kudhuru ngozi ya binadamu na kusababisha kubanduka na kuwasha kwa ngozi. Si kama hivyo tu, maji yaliyotolewa baada ya kufua nguo kwa sabuni ya unga pia yanachafua mazingira.

Ili kusanifu mashine ya aina hiyo ya kufulia, shirika la Haier liliunda kikundi cha utafiti lililoshirikisha idara nane zikiwemo idara za masoko, utafiti, huduma baada ya kununua na hakimiliki. Baada ya juhudi za miaka minne, shirika hilo lilifanikiwa kusanifu mashine mpya ya aina hiyo. mashine ya kufulia ya aina hiyo ina hakimiliki za aina 32. matokeo ya uchunguzi uliofanywa na idara ya uchunguzi na usimamizi wa sifa za vyombo vya umeme vya matumizi ya nyumbani ya taifa ya China, mashine ya kufulia ya aina hiyo inaweza kufua nguo kwa asilimia 87.5 bila kutumia sabuni ya unga, ikiwa ni asilimia 25 zaidi kuliko mashine ya kufulia ya kawaida.

Kutokana na uwezo wake mkubwa, mwanzoni mwa mwaka huu, mashine ya kufulia ya aina hiyo ilikabidhiwa tuzo ya maendeleo ya sayansi na teknolojia ya taifa ya China, na imekuwa bidhaa pekee iliyopewa tuzo hiyo katika sekta ya vyombo vya umeme vya matumizi ya nyumbani nchini China. tokea mashine ya aina hiyo ianze kuuzwa mwaka jana, imetambuliwa na kufurahiwa kwa haraka na wateja na kuwa bidhaa inayonunuliwa sana.

Meneja mauzo wa duka moja kubwa la Beijing Bw. Ren Zhenhua alieleza kuwa, mauzo ya mashine ya kufulia ya aina hiyo mpya yanachukua asilimia 20 ya mauzo ya jumla ya aina zaidi ya 20 ya mashine ya kufulia ya Haier. Alisema,

"mashine ya kufulia ya aina hiyo inanunuliwa sana. Wajawazito wanachukua asilimia kubwa ya wanunuaji, kwani wanafikiri ni nzuri zaidi kwa watoto wao wachanga. Kama nguo za watoto wachanga haziwezi kufuliwa kikamilifu na sabuni ya unga ikabaki kwenye nguo, itakuwa na madhara kwa watoto wachanga."

Bw. Yang Qinglin aliyekuwa anataka kununua mashine ya kufulia kwenye duka hilo baada ya kusikiliza maelezo ya mwuzaji, aliamua mara moja kununua mashine ya kufulia ya aina hiyo.

"mashine ya kufulia ya aina hiyo ni nzuri sana. Kwanza inaweza kupunguza matumizi ya sabuni ya unga, pili inasaidia kuhifadhi mazingira."

Bw. Zhang Yang aliyefunga ndoa mwezi uliopita pia amechagua kununua mashine ya kufulia ya aina hiyo, na ameridhika sana na mashine hiyo.

"kabla ya kununua mashine hiyo pia nilikuwa na mashaka, nilikuwa sijui kama inaweza kufanya kazi vizuri kama ilivyotangazwa. Baadaye rafiki yangu alinishawishi, kwa hiyo nikaamua kununua mashine hiyo. Mpaka sasa nimeitumia kwa mwezi mzima, na inafanya kazi vizuri sana. Ingawa haitumii sabuni ya unga lakini inaweza kufua nguo vizuri sana."

Mashine ya kufulia ya aina hiyo ikiwa ni bidhaa ya teknolojia mpya ya juu, baada ya kutolewa sokoni, imeathiri sana mtizamo wa kawaida ya kufua nguo. Lakini kutokana na shirika la Haier kujitahidi kueneza ujuzi wa teknolojia hiyo mpya, hivi sasa watu wameanza kuelewa na kupokea mtizamo huo mpya ambao mashine ya kufulia inaweza kufua nguo bila kutumia sabuni ya unga. Lakini bei yake kubwa zaidi ya yuan elfu tano bado inawakwamisha wateja wengi. Wanaona kuwa, bei yake ni ghali sana ambayo ni mara mbili ya mashine ya kufulia ya kawaida.

Lakini Bi. Wang Yanfang aliyeanza kutumia mashine hiyo alisema, mashine hiyo haitumii sabuni ya unga basi inapunguza matumizi hayo na pia matumizi ya maji na umeme. Hivyo ingawa mashine hiyo ni ghali sana lakini matumizi yake ni ya machache, kwa jumla thamani yake inalingana na bei hiyo.

"ingawa bei yake ni kubwa. Lakini inapunguza matumizi ya sabuni ya unga, maji na hata umeme. "

mashine ya kufulia ya aina hiyo ya Haier isiyotumia sabuni ya unga pia inawavutia wageni wengi. Hivi karibuni, wafanyabiashara kutoka nchi zaidi ya 10 ziliwemo Marekani, New Zealand, Japan, Singapore, Pakistan na India kwa nyakati tofauti wamesaina mkataba na shirika la Haier kuagiza mashine ya kufulia ya aina hiyo. Katika siku za baadaye, mashine ya kufulia ya aina hiyo itaingia kwenye soko la nchi za nje na kuwahudumia wateja wengi zaidi.