Mkutano wa baraza la shirika la atomiki duniani tarehe 8 ulijadili taarifa iliyotolewa na mratibu mkuu wa shirika hilo kuhusu suala la nyukilia la Iran. Jambo linalofanya watu wawe na wasiwasi mkubwa ni kwamba, siku hiyo Marekani na Iran zote zilisisitiza misimao yao thabiti. Baadhi ya wachambuzi wanaona, mapambano kati ya Marekani na Iran kuhusu suala la nyuklia yataathiri pande zote mbili.
Mwakilishi wa kudumu wa Marekani aliyeko katika shirika la atomiki duniani Bw. Gregory Schulte alipotoa hotuba kwenye mkutano huo alisema, kinadharia, Iran hivi sasa imeshakuwa na hewa yenye uranium UF6 inayotosha kwa uzalishaji wa mabomu 10 ya atomiki, aliongeza, "hivi sasa ni wakati wa kuchukua hatua kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa". Alisema baraza la usalama linatakiwa kusisitiza, endapo Iran haitatekeleza ahadi ilizotoa, "itakiona cha mtema kuni". Siku moja kabla, makamu wa rais wa Marekani Bw. Dick Cheny alionya kuwa, endapo Iran haitafanya kama inavyotakiwa na jumuiya ya kimataifa, "itakiona cha mtema kuni".
Kiongozi wa ujumbe wa Iran ambaye pia ni naibu katibu wa kamati ya usalama ya taifa ya Iran, ambaye hivi sasa anahudhuria mkutano huo, Bw. Jawad Wayi tarehe 8 aliashiria kuwa endapo Marekani inachukua hatua dhidi ya Iran, basi Iran itapambana nayo ncha kwa ncha. Alitangaza taarifa moja kwa vyombo vya habari mara tu baada ya kumalizika kwa mkutano wa siku hiyo, alisema Marekani inaweza kuipatia nchi nyingine madhara na taabu, lakini nchi hiyo yenyewe pia ni rahisi kupatwa na madhara na taabu. Alisema, "ikiwa Marekani itachagua njia hiyo, basi wacha ichague!" Alisisitiza Iran haitajali chochote kitakachoweza kutokea, itaendelea na shughuli za utafiti wa kisayansi kuhusu usafishaji wa uranium. Rais Mohamed Ahmadinej siku hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika nchini humu alisema, "wale wanaotaka kushambulia haki za Iran watajuta haraka!" Mwakilishi kwa kwanza wa Iran kwenye mkutano kuhusu suala la nyukilia hivi karibuni alisema, endapo nchi za magharibi zitatumia mbinu za kimabavu dhidi ya Iran, Iran itapambana nazo hadi mwisho. Hakuzuia uwezekano wa Iran kutumia "silaha ya mafuta".
Kutokana na kukabiliwa na msimamo thabiti wa Iran, Marekani inasema itachagua njia yoyote ikiwemo ya kijeshi dhidi ya Iran. Kwanza zana za nyukilia za Iran zimeenea chini kwa chini katika sehemu mbalimbali nchini Iran, hivyo mashambulizi yanayojulikana kwa "operesheni" hayatasaidia kitu. Pili, Iran ina makombora ya masafa ya kati, hivyo nchi za ghuba na Israel zenye majeshi ya Marekani zinaweza kupigwa na makombora hayo. Aidha, Iran inaweza kutumia mbinu isiyo ya kijeshi dhidi ya shinikizo la kijeshi ya Marekani, ikiwa ni pamoja na kufunga mlango wa bahari ya Holmes, hatua ambayo itaweza kupunguza pato la Marekani kwa asilimia 4 au 5 hivi ndani ya miezi mitatu, tena kuongeza upungufu wa ajira kwa 2%. Mbali na hayo, yawe mapigo ya kijeshi au vikwazo vya kiuchumi, vitahimiza Iran kuimarisha azma yake ya kufanya uvumbuzi wa nyukilia, hatimaye si kama tu suala la nyukilia la Iran halitaweza kudhibitiwa, tena itakuwa na uwezekano wa kuleta mgogoro mkubwa kwenye mashariki ya kati.
Kwa Iran, yawe mashambulizi ya kijeshi ua vikwazo vya kiuchumi, itaathirika sana. Kuhusu vikwazo vya kiuchumi, usafirishaji wa mafuta ya asili ya petroli wa Iran unachukua nafasi ya 3 ya mahitaji ya dunia, lakini pato la Iran kutokana na usafirishaji wa mafuta linachukua 90% ya jumla ya pato lake na kuchukua nafasi ya 50% ya bajeti ya serikali. Uchumi wa Iran unaotegemea sana usafirishaji wa mafuta ni dhaifu sana. Licha ya hayo, katika miaka ya karibuni kiasi cha ukosefu wa ajira na mfumuko wa bei viliongezeka kwa mfululizo, na inahitaji sana mitaji ya nchi za nje. Hivyo, nchi hiyo kutumia "silaha ya mafuta" au kupinga kuwekewa vikwazo, itapatwa na matatizo makubwa.
Hivi sasa baadhi ya nchi na vyombo vya habari vinatoa wito wa kutaka pande mbalimbali husika zijizuie na kuepusha mambo kuharibika zaidi ili kuwezesha suala hilo kutatuliwa kwa njia mwafaka ndani ya shirika la atomiki duniani.
Idhaa ya Kiswahili 2006-03-09
|