Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-10 20:01:26    
Wajumbe wa Bunge la umma la China watoa maoni na mapendekezo kuhusu utatuzi wa suala la malipo makubwa ya matibabu

cri

Katika miaka ya hivi karibuni, wananchi wengi wa China wanalalamika zaidi malipo makubwa ya matibabu, kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la umma la China unaofanyika hivi sasa hapa Beijing, suala la malipo makubwa ya matibabu linajadiliwa zaidi na wajumbe, ambapo wajumbe wengi wametoa maoni na mapendekezo juu ya utatuzi wa suala hilo.

Mkazi wa Xuchang mkoani Henan, katikati ya China Bibi Han Ping siku chache zilizopita, alipata mafua akaenda hospitali moja kubwa mjini Xuchang kutibiwa ugonjwa wa mafua, baadaye alilipa zaidi ya yuan 200, kiasi ambacho ni sawa na pato la mwezi mmoja kwa kila mkulima wa China. Han Ping alimwambia mwandishi wetu wa habari akisema:

Watu husema, bora usiugue, usije ukapoteza pesa nyingi. Nilipata mafua tu, nikalipa zaidi ya yuan 200 kwa matibabu. Naona malipo hayo ni makubwa ya kupita kiasi.

Uchunguzi uliofanyika umeonesha kuwa, wakazi wa China wakiugua, karibu nusu yao ambao wangekwenda hospitali hawaendi kukutana na madaktari, na karibu asilimia 30 ya wagonjwa ambao wangelazwa hispitalini lakini waliacha kulazwa, sababu kubwa ni kwamba malipo ya matibabu ni makubwa ya kupita kiasi.

Kwa nini malipo ya matibabu ni makubwa ya kuwatisha watu? Katika miaka ya hivi karibuni, mjumbe wa Bunge la umma la China ambaye ni profesa wa Chuo kikuu cha tiba cha Nanjing Bibi Guan Xiaohong anafuatilia sana suala hilo na alikwenda mara kwa mara hospitali, viwanda vya kutengeneza madawa, idara za serikali, pia alizungumza na madaktari na wagonjwa, anaona kuwa, sababu kubwa kwa malipo makubwa ya matibabu ni kutokana na bei kubwa za kupita kiasi ya madawa. Na bei kubwa za madawa ni kutokana na kupandishwa juu na wakala kwenye ngazi mbalimbali, ambapo wafanyabiashara walipata faida kuwa, aidha, madawa kadha wa kadha yaliyojulikana zamani siku hizi yamepambwa upya na kubadilishwa majina, yakawa madawa mapya, hivyo bei zao zimepandishwa juu kwa kiasi kikubwa. Bibi Guan alisema:

Madawa fulani kwa kweli yalikuwa ya bei chini na yenye ufanisi, lakini kutokana na faida ndogo katika mauzo, viwanda viliyapamba upya au kuyabadilisha kuwa ya aina nyingine, halafu kupandisha bei za madawa hayo. Watu wa viwanda walisema, madawa kadha wa kadha ya bei chini na yenye ufanisi hayatengenezwi tena kwenye viwanda.

Sababu nyingine kubwa ya malipo makubwa ya matibabu ni kwamba serikali haikutenga fedha za kutosha kwa shughuli za tiba nchini China. Hivi sasa fedha zilizotengwa na serikali kwenye shughuli za tiba hazifikii asilimia 10 ya mapato ya hoispitali. Naibu mkuu wa hospitali moja ya mkoa wa Shanxi ambaye pia ni mjumbe wa Bunge la umma la China Bwana Wei Xiaochun alisema:

Katika miaka mingi iliyopita, sera ya China haikutilia maanani zaidi uwekezaji kwenye shughuli za afya. Ndiyo maana, hospitali nyingi zinajitahidi kuchuma pesa, na hakika faida zilizopata zilitokana na malipo ya wagonjwa.

Bibi Guan anaona serikali ingetenga fedha zaidi katika sekta ya afya, hasa ingetenga fedha zaidi katika sekta ya afya vijijini na mitaani.

Mjumbe Miao Yu amependekeza serikali itilie maanani kuendeleza kliniki kwenye sehemu za makazi, ili wagonjwa wasiwe na haja ya kwenda hospitali kubwa kutibiwa magonjwa ya kawaida.

Wajumbe wengi wanaona kuwa, bado kunahitaji muda mrefu kutatua suala la malipo makubwa ya matibabu nchini China, wameipendekeza serikali ichukue mbinu mbalimbali za kuhimiza suala hilo litatuliwe mapema iwezekanavyo.

Idhaa ya Kiswahili 2006-03-10