Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-10 20:43:12    
Kikosi cha tatu cha kulinda amani cha China nchini Liberia chatunukiwa nishani ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.

cri

Tarehe 28 Februari mwaka huu, sherehe ya utoaji wa nishani ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa kwa kikosi cha tatu cha kulinda amani cha jeshi la ukombozi la watu wa China kilichotekeleza jukumu la kulinda amani nchini Liberia, ilifanywa kwa shangwe huko Liberia. Ofisa wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia Bwana Tiago Dos Reis, naibu mkuu, na makamanda wa vikosi mbalimbali vya jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa nchini Liberia waliwatunukia nishani ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa askari na maofisa wa vikosi vitatu vya uchukuzi, uhandisi na matibabu vya China walioko nchini Liberia.

Ofisa mwandamizi wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia, ambaye pia ni konsela wa kisiasa wa China nchini Liberia Bwana Gou Haodong alisoma risala kwa niaba ya balozi wa China nchini Liberia. Kwenye risala hiyo aliwasifu askari na maofisa wa China waliotekeleza jukumu la kulinda amani nchini Liberia kwa mchango waliotoa katika kuisaidia serikali ya Liberia na wananchi wake kutimiza amani na kuanza ukarabati wa nchi, na kuzidisha uhusiano wa kirafiki kati ya China na Liberia. Alisisitiza kuwa, ikiwa nchi kubwa inayoendelea ambayo ni mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na nchi inayowajibika, China itashikilia njia ya kujiendeleza kwa amani, kufanya juhudi kama ilivyokuwa siku zote katika kulinda amani ya dunia, na kuhimiza maendeleo ya pamoja ya binadamu.

Bw. Dos katika risala yake aliipongeza China kwa mchango mkubwa ilitoa katika kushiriki vitendo vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na kuleta amani ya dunia, kutathmini vizuri umuhimu uliofanywa na vikosi vitatu vya kulinda amani vya China katika kuleta amani, na kuhakikisha utekelezaji wa jukumu la tume ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia. Bw. Dos pia aliwasifu askari wa kikosi cha uhandisi cha China kwa kuchapa kazi katika kutengeneza barabara na madaraja na kutoa mchango wao ipasavyo katika kuboresha hali ya mawasiliano ya barabara, askari wa kikosi cha matibabu kutoa huduma nzuri na msaada wa kibinadamu kwa wafanyakazi wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia na wenyeji, ambapo askari wa kikosi cha uchukuzi waliendesha magari usiku na mchana ili kusafirisha shehena kwa wakati.

Bw. Dos alisema uchaguzi mkuu wa Liberia umefanyika bila matatizo, hali ya usalama ya nchi hiyo inakuwa mzuri siku hadi siku, lakini jukumu la ukarabati wa amani la nchi hiyo bado ni kubwa, alitumai kuwa askari na maofisa wa vikosi vya kulinda amani ya China watachangia zaidi katika kuleta amani ya kudumu na kustawisha uchumi wa nchi hiyo.

Idhaa ya Kiswahili 2006-03-10