Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-13 15:20:23    
Vivutio vya maua ya Also (cymbidium) mjini Guiyang

cri

Guiyang ni mji mkuu wa mkoa wa Guizhou, mjini humo hakuna baridi kali katika majira ya baridi, na hakuna joto kali katika majira ya joto, hali ya hewa ya huko inafaa sana kwa ukuaji wa maua ya Also. Mwanzoni mwa majira ya mchipuko, sehemu nyingi mbalimbali nchini China bado zinakuwa na baridi, lakini hali ya mchipuko inaonekana kote mjini Guiyang.

Ukipata nafasi kutembea mjini Guiyang utaona maua ya Also yanachanua katika mabustani na barabarani, harufu nzuri inanukia kote mjini, siku za majira hayo ni siku za kuangalia maua ya Also ili kupata raha mustarehe.

Maua ya Also yanasifiwa sana na wakazi wa Guiyang, ambayo yamechaguliwa kuwa maua ya alama ya mji huo, kila ifikapo siku za kuchanua kwa maua hayo, popote unapokwenda utawaona wakazi wa Mji Guiyang wanaonunua maua kwenye maduka au magulio. Mfanyabiashara ya maua ya Also Bibi Wang Ping ametuambia, wakazi wa huko wana desturi ya kupanda maua ya Also, hata wanafanya juhudi kubwa katika kupanda na kutunza maua hayo. Akisema:

Duka letu linauza tu maua ya Also ya aina ya vipepeo, bei za maua hayo si ghali sana, lakini kila chungu cha maua ni Yuan mia 3 hadi mia 4, wakazi wa Guiyang wanapenda sana maua hayo wengi wananunua bila kujali bei yake.

Watu wanaokwenda kwenye duka hilo kununua maua, wengi ni wanaopenda maua ya also, lakini wengi walinunua maua ya Also ya kawaida ili kuyatunza nyumbani. Na mashabiki wa maua ya Also kila mmoja ana upendeleo wake maalum juu ya maua ya Also, wakienda dukani huchagua kwa makini sana. Bwana Luo Wendian kutoka mkoa wa Sichuan unaopakana na mkoa wa Guizhou ni shabiki maalum wa maua ya Also, yeye anapendelea maua ya Also ya porini, hivyo maua ya also porini yanayostawi mkoani Guizhou yanamvutia zaidi. Alisema:

Mji wa Guiyang una mazingira mwafaka zaidi kwa ukuaji wa maua ya Also ya porini, hivyo maua ya Also ya porini ya mji huo ni mengi ya aina mbalimbali. Naona kazi ya dharura ya hivi sasa, ni lazima kuhifadhi maua hayo ya porini, kwani kufanya hivyo kunasaidia kuboresha mazingira, kusafisha hewa, na kuinua sifa ya wakazi wa mji huo.

Bwana Luo kila mwaka anakwenda kutembelea maonesho ya maua ya Also yanayofanyika nchini China. Mwaka huu maonesho hayo ya maua ya also yalifanyika mjini Guiyang.

Maonesho hayo yaliandaliwa kwenye Jumba la utamaduni wa kitaifa katikati ya mji wa Guiyang, ambapo vyungu zaidi ya 4000 ya aina mbalimbali za maua ya Also vilioneshwa na kuchaguliwa na watu, kama chungu kimoja cha maua ya Also kikipata "tuzo", basi bei yake itapanda, si kama tu chungu hicho cha maua ya Also kitavutia watazamaji wengi bali pia kitanunuliwa kwa bei kubwa na watu wanaopenda maua ya Also wa nchini na za ng'ambo. Kwenye maonesho hayo ya mwaka huu, mtalii mmoja wa Japan alilipa Yuan ya kichina elfu 20 akanunua chungu kimoja cha maua ya Also kilichopewa "tuzo".

Kwenye maonesho hayo mwandishi wetu wa habari aliona chungu kimoja cha maua ya also kilichopewa "tuzo" ambacho kiliwavutia watazamaji wengi ambao wote ni wanaopenda maua ya Also. Maua ya Also ya chungu hicho ni ya rangi pinki, yalipewa jina la "msichana wa ndotoni". Chungu hicho cha maua ya also kilisifiwa sana na Bwana Hu Keqing kutoka mkoa wa Guangdong, kusini mwa China. Bwana Hu alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, hivi sasa watu wanaopenda maua ya Also wa sehemu mbalimbali nchini China kila mwaka wanaweza kwenda Guiyang kukutana na marafiki wao wanaopenda maua ya Also, Bwana Hu anaona Mji Guiyang ungeendeleza shughuli za maua ya also kuwa shughuli moja rasmi. Alisema:

Mjini Guiyang kuna hali nzuri ya hewa na mazingira safi ya hewa, mji huo pia ni kama mji wa bustani unaoegemea milima na mito, mazingira hayo yanasaidia kuendeleza shughuli za maua ya Also.

Kwenye maonesho ya maua ya Also yaliyofanyika mjini Guiyang mwaka huu, chungu kimoja cha maua ya Also yalilyopewa jina la "Taifa la China lenye ustawi na neema" kiliwavutia zaidi watazamaji. Maua hayo yana rangi nyekundu, kimanjano, kijani na nyeupe, mtindo wake pekee unaonekana dhahiri na wa kuvutia zaidi. Chungu hicho cha maua kilitoka mkoa wa Sichuan. Watazamaji waliopata fursa ya kutazama chungu hicho cha maua ya Also walifurahi sana. Bibi kizee Huang Fulin alisema, nimepata fursa ya nadra kutazama maua hayo yenye kivutio cha ajabu.

Tulipotazama maua hayo yanayopendeza tulifurahi kweli, hasa sisi wazee, tunapenda kutembelea kwenye maonesho ya maua, tukipata fursa ya kutazama maua hayo ya ajabu, tunaona kama tumepata raha mustarehe.

Lakini maonesho ya maua ya Also siyo kama yanafanyika kila mwaka mjini Guiyang, lakini kwa kweli mjini humo kuna sehemu nyingi zenye vivutio vya maua ya Also ya aina mbalimbali, miongoni mwa maua hayo, mengi ni yenye thamani kubwa. Kama wewe pia ni mshabiki wa maua ya Also, usikose fursa ya kuja China na kwenda mjini Guiyang mkoani Guizhou, kusini magharibi ya China kwa matembezi.

Idhaa ya kiswahili 2006-03-13