Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-13 19:11:24    
Kwanini mkutano wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa umeahirishwa kwa wiki moja

cri

Mkutano wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa hufanyika kwa wiki 6 huko Geneva katika ya mwezi Mach kila mwaka. Kutokana na utaratibu uliopangwa, mkutano wa 62 wa mwaka huu ungefanyika kati ya tarehe 13 mwezi Mach hadi tarehe 21 mwezi Aprili. Lakini katika siku chache kabla ya kufanyika kwa mkutano wa mwaka huu, mwenyekiti wa mkutano Bw. Manuel Rodriguez Cuadros aliviambia vyombo vya habari kuwa, baada ya kushauriana wajumbe wa kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa wamekubaliana kuahirisha mkutano wa mwaka huu kwa wiki moja ili kusubiri uamuzi wa mwisho wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuanzishwa kwa baraza la haki za binadamu.

Bw. Cuadros alidokeza kuwa, njia itakayofuatwa ni kufungua mkutano tarehe 13 kama kawaida, lakini mara tu baada ya mkutano kufunguliwa, akiwa mwenyekiti wa mkutano atatoa pendekezo la kupumzika kwa wiki moja. Kama hakuna maoni ya kupinga, atatangaza mkutano ufanyike tarehe 20 mwezi Machi.

Kuanzisha baraza la haki za binadamu kuibadili kamati ya haki za binadamu iliyoko hivi sasa mjini Geneva ni moja ya mambo muhimu katika mageuzi ya Umoja wa Mataifa yaliyothibitishwa kwenye mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mwezi Septemba mwaka uliopita na kuorodheshwa katika "Nyaraka za Mafanikio" za mkutano. Lakini nchi nyingi zilikuwa na maoni ya aina mbalimbali kuhusu suala hilo, hata zilikuwa na maoni ya kwenda kinyume na maoni hayo. Nia ya nchi za magharibi ni kupunguza ukubwa wa kamati ya haki za binadamu na kuondoa nchi wanazoziona kuwa zina rekodi mbaya ya haki za binadamu na kudhibiti zaidi shughuli za haki za binadamu za Umoja wa Mataifa. Lakini nchi nyingi zinazoendelea zinataka kutumia mageuzi hayo kuepusha suala la haki za binadamu kuwa la kisiasa, ili kuondoa mazoea ya kamati ya haki za binadamu ambayo imekuwa mahali pa nchi za magharibi pa kushutumu na kusingizia nchi zinazoendelea. Tofauti hiyo ya maoni kuhusu baraza la haki za binadamu hakika italeta shida kubwa kwa baraza hilo.

Baada ya kufanyika kwa mazungumzo ya maduru zaidi ya 30 katika nusu mwaka uliopita, nchi nyingi zimekuwa na maoni ya namna moja kuhusu baadhi ya mambo. Juu ya msingi huo, mwenyekiti wa baraza kuu la 60 la Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson mswada mmoja wa azimio ambao ulitangazwa tarehe 23 mwezi Februari. Alidhani kuwa mswada huo ungepitishwa kwa upigaji kura katika Umoja wa Mataifa katika wiki iliyofuata, na kuanzisha rasmi baraza la haki za binadamu kabla ya kufanyika kwa mkutano wa haki za binadamu mwaka huu, ili kumaliza mchakato wa kupokezana kati ya idara hizo mbili. Mswada huo uliungwa mkono na nchi nyingi mara tu baada ya kutangazwa. Umoja wa Ulaya ulitoa taarifa ikiunga mkono na kusema, "mswada huo unatimiza masharti ya kimsingi ya kuanzisha baraza la haki za binadamu".

Lakini tarehe 27 mwezi Februari mwakilishi wa kudumu wa Marekani aliyeko Umoja wa Mataifa Bw. John Bolton alisema, mswada huo haulingani sana na matakwa ya Marekani kuhusu ukubwa wa baraza, sifa za wajumbe na uendeshaji wa shughuli, hivyo alitaka kufanya mazungumzo kuhusu mswada na kufanya marekebisho. La sivyo, Marekani itapiga kura ya kuupinga.

Kuhusu ukubwa wa baraza, nchi zinazoendelea zinataka kwa uchache kubakiza nchi wanachama 53 zilizopo hivi sasa ili kuwa na uwakilishi wa nchi nyingi. Mswada wa Bw. Eliasson unapendekeza kuweka nchi wanachama 47, lakini Marekani inaona idadi hiyo ni kubwa sana ikilinganishwa na inayotaka ya nchi wanachama 30. Marekani inaona, nchi wanachama zikiwa nyingi, hususan kuingiza nchi ambazo zinaonekana kuwa na rekodi mbaya, ni sawa tu kuweka "pombe mpya" ya baraza la haki za binadamu katika "chupa ya zamani" ya kamati ya haki za binadamu. Kuhusu sifa za nchi wanachama, mswada unataka nchi wanachama ziwe zinapata zaidi ya nusu ya kura za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa; lakini Marekani inataka kuinua kigezo chake, yaani nchi wanachama wa baraza sharti zipate zaidi ya theluthi mbili za kura za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Kuhusu uendeshaji wa shughuli za baraza, Marekani inaona kuwa mkutano wa kamati ya haki za binadamu unachukua muda wa wiki 6 tu kwa mwaka, uendeshaji shughuli wake ni kama haupo, hivyo inataka baraza hilo liwe la kudumu na liweze kuwa na mkutano wakati wowote. Mswada wa azimio baada ya kusikiliza pendekezo la nchi zinazoendelea la kupinga baraza hilo liwe la kudumu, unataka baraza hilo liwe na mikutano mara tatu kwa uchache kwa mwaka, na muda wa mkutano usiwe chini ya wiki 10, tena mkutano wa dharura uweze kuitishwa wakati wowote. Lakini Marekani bado haijakubaliana na hali hiyo.