Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-15 18:25:19    
Si busara kwa Japan kuubana Umoja wa Mataifa kwa kisingizio cha ada ya uanachama

cri

Tokea kushidwa mwaka jana kwa azma ya Japan ya kuwa mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, mwaka huu Japan imeanza tena kuzishawishi nchi nyingine na kuchukua hatua nyingi za wazi na za chinichini kujaribu kutimiza azma yake. Lakini azma hiyo ya Japan ilishindwa tena tarehe 13, ambapo kamati ya 5 inayoshughulikia bajeti ya baraza kuu la 60 la Umoja wa Mataifa, ilijadili viwango vya uanachama wa nchi mbalimbali za Umoja wa Mataifa, pendekezo lililotolewa na Japan wiki iliyopita kuhusu kiwango cha chini kabisa cha ada kwa nchi wajumbe wa baraza la usalama, lilikosolewa na nchi nyingi zikiwemo Russia na China. Wachambuzi wanasema, si busara kwa Japan kuubana Umoja wa Mataifa kwa kisingizio cha ada ya uanachama.

Kwa kufuata jadi yake, ugawaji wa ada ya Umoja wa Mataifa huwa unathibitishwa kila baada ya miaka mitatu, kamati ya 5 ya Umoja wa Mataifa, ambayo inakabidhiwa jukumu la kushughulikia bajeti ya umoja huo, itatoa uthibitishaji wa ugawaji wa ada ya uanachama ya nchi wanachama ya kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2009. Tarehe 10 mwezi huu Japan ilitoa pendekezo la kutaka kufanya marekebisho juu ya ugawaji wa ada ya uanachama ya Umoja wa Mataifa uliopo hivi sasa, ili ilingane na hali halisi za uchumi za nchi mbalimbali, na tena iendane na "hadhi na majukumu" yake katika Umoja wa Mataifa, yaani ada za nchi za wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama kwa uchache kabisa zingechukua 3% au 5% ya jumla ya ada ya Umoja wa Mataifa. Mshiriki wa mkutano kutoka Russia alisema, pendekezo hilo la Japan limekwenda kinyume na "kanuni za ulipaji wa uwezo", na Russia inashindwa kukubaliana na pendekezo hilo. Naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Zhang Yishan alisema, pendekezo la Japan lina lengo la kisiasa na halilingani na kanuni za ulipaji kutokana na uwezo, hivyo China haikubaliani na pendekezo hilo.

Ukweli ni kwamba si mara ya kwanza kwa Japan kufanya mchezo wa namna hiyo. Tokea mwezi Septemba mwaka uliopita, maofisa wa Japan katika ngazi mbalimbali na kwa nyakati tofauti walisema, Japan inanuia kuutaka Umoja wa Mataifa ufanye majadiliano mwaka 2006 kuhusu suala la Japan kupunguziwa ada ya uanachama, na kutarajia Umoja wa Mataifa ufuate njia ya ugawaji wa ada ya haki na usawa zaidi. Kwani Japan inaona, ada inayotoa hivi sasa hailingani na umuhimu inaofanya katika Umoja wa Mataifa.

Kanuni husika za Umoja wa Mataifa zinaagiza kuwa kiasi cha ada inachotoa nchi mwanachama kinathibitishwa na kamati ya 5 ya Umoja wa Mataifa, hususan kwa kuzingatia mambo mengi yakiwemo mapato na madeni ya nchi hiyo. Kwa nchi zinazoendelea zenye pato dogo kwa wastani, utoaji ada unathibitishwa kwa kufuata njia nyingine maalumu ya nafuu. Aidha, utoaji ada unafuata kanuni za kiwango cha juu kabisa na kiwango cha chini kabisa. Hivi sasa, kiwango cha juu kabisa ni chini ya 22% ya ada ya Umoja wa Mataifa na kile cha chini kabisa kisiwe chini ya 0.001%. Hali hii inaonesha kuwa uthibitishaji wa viwango vya ada ya uanachama vya nchi mbalimbali ni wa makini kwa sasa katika utoaji ada wa Umoja wa Mataifa, Marekani inachukua 22%, Japan inachukua 19.468% zikifuatiwa na Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Canada, Italia, Hispania, na China ikichukua nafasi ya 9 ikitoa 2.053%.

Umoja wa Mataifa ukiwa jumuiya ya kimataifa iliyo kubwa na yenye heshima kubwa zaidi, toka muda mrefu uliopita ulifanya kazi kubwa na muhimu katika kulinda amani na utulivu wa dunia, kuhimiza ushirikiano wa kimataifa, kusawazisha ugawaji wa maslahi duniani na kuhimiza maendeleo ya nchi maskini. Ingawa Japan inadai, kupunguza ada ya uanachama wake hakuhusiani na ombi lake la kuwa nchi mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama, lakini ofisa wa kudumu wa Japan katika Umoja wa Mataifa aliwahi kusema, hivi sasa nafasi ya utoaji ada ya uanachama ya nchi nyingine 4 wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama kati ya wajumbe watano, bado ni ndogo ikilinganishwa na ada inayotoa Japan, ambayo siyo mjumbe wa kudumu wa baraza hilo, hali ya namna hii haiwezi kuendelea tena. Ni dhahiri kuwa kwa Japan, ada ya uanachama ya Umoja wa Mataifa inahusiana sana na hadhi ya kuwa mjumbe wa kudumu ya baraza la usalama.

Vyombo vya habari vinasema, endapo Japan itaendelea kuubana Umoja wa Mataifa kwa tishio la kupunguza utoaji ada, itakosa uungaji mkono wa nchi husika.