Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-15 18:28:45    
Wachina wengi watilia maanani afya ya kisaikolojia

cri

Feng Yuxuan ni mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo kikuu cha umma cha China. Kutokana na kukabiliwa na shinikizo la masomo na hisia, anapata fikra za ajabu mara kwa mara, hali hii inamsumbua sana. Alimwambia mwandishi wa habari kuwa, "Wakati wa mapumziko, nakuwa na fikra mbalimbali za ajabu kichwani mwangu, nashindwa kupumzika. Na hali hii inanifanya nichoke sana darasani. "

Tarehe 25, Februari kijana huyo aliwahi sana kufika kwenye darasa la mihadhara la chuo kikuu hicho kushiriki kwenye mafunzo ya darasa la afya ya kisaikolojia.

Mafunzo ya darasa hilo yanahusu masomo 24 ambayo yanaandaliwa kwa pamoja na asasi ya utafiti na utatuaji wa matatizo ya kisaikolojia ya Beijing na Chuo kikuu cha umma cha China. Masomo hayo ni kuhusu namna ya kuthibitishwa tatizo la kuwa na majonzi na kuondoa huzuni, umaalumu wa kisaikolojia na kihisia wa wanafunzi wa vyuo vikuu, na kuondoa matatizo ya kisaikolojia. Masomo hayo yanatolewa na wataalamu wa China na wageni wanaofanya kazi katika asasi ya utafiti na utatuaji wa matatizo ya kisaikolojia ya Beijing na walimu wanaoshughulikia elimu ya afya ya kisaikolojia katika vyuo vikuu vya Beijing. Mafunzo hayo yataendelea hadi mwezi Januari mwakani.

Bw. Feng Yuxuan alipohojiwa alieleza kuwa, aliwahi kwenda kwa daktari wa matatizo ya kisaikolojia lakini matatizo yake hayakuweza kutatuliwa.

Alisema, "Kuonana na daktari anayeshughulikia matatizo ya kisaikolojia ni gharama sana. Katika hospitali kadhaa, mazungumzo ya kisaikolojia yanatoza malipo ya Renminbi Yuan 40 hadi 80 kwa saa, kiasi ambcho siwezi kumudu. Lakini darasa hilo la afya ya kisaikolojia ni bure, ambalo linafundishwa katika Jumamosi ya wiki ya tatu ya kila mwezi. Kushiriki kwenye darasa hilo hakika kutanisaidia."

Mkurugenzi wa asasi ya utafiti na kushughulikia matatizo ya kisaikolojia ya Beijing Bw. Cao Lianyuan alifafanua kuwa, "Sambamba na mabadiliko ya jamii ya China, kila mtu anakabiliwa na changamoto ya kisaikolojia kwa kiwango fulani. Suala la afya ya kisaikolojia si kama tu linahusiana na mtu binafsi, bali pia afya ya watu wengine katika jamii yetu."

Takwimu kutoka Wizara ya afya ya China zinaonesha kuwa, nchi hii yenye watu bilioni 1.3, watu wasiopungua laki 2 na elfu 50 walijiua na wengine milioni 2 wanajaribu kujiua kila mwaka. Na miongoni mwa sababu zinazosababisha vifo vya watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 34, kujiua ni sababu inayoongoza. Kwa hiyo tatizo hilo linastahili kuzingatiwa.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa asasi ya utafiti na kushughulikia matatizo ya kisaikolojia ya Beijing, nchini China asilimia 70 ya watu waliojiua au waliojaribu kujiua hawakutafuta msaada wowote wa kisaikolojia, na asilimia 60 ya watu waliojiua na asilimia 40 ya watu waliojaribu kujiua walikuwa wanasumbuliwa na matatizo makubwa ya kisaikolojia.

Somo la kwanza la Darasa la afya ya kisaikolojia liliwavutia wasikilizaji zaidi ya 300, wakiwemo walimu na wanafunzi wa vyuo vikuu, watu wanaojitolea na wakazi wa kawaida wa mji wa Beijing.

Mzee mstaafu Li Renze mwenye umri wa miaka 73 alikuwa miongoni mwa wasikilizaji wa somo hilo la kwanza. Alitoa maoni yake kuwa, "Afya ya kisaikolojia ni jambo muhimu la kwanza. Furaha ni jambo zuri kuliko mengine. Furaha ya mtu mmoja inaweza kusambazwa na kuwa na athari kwa wenzake." Alisema anatumai kufuata masomo hayo ili apate elimu na mbinu za kudumisha afya ya kisaikolojia.

Kijana Feng Yuxuan alieleza kukaribisha sana masomo hayo, akisema "Katika jamii yenye ushindani mkali, watu wanakabiliwa na mashinikizo mbalimbali ya kisaikolojia." Alipendekeza kuandaliwa kwa mafunzo mengi ya namna hii yanayotolewa na wataalamu wa afya ya kisaikolojia ili watu wengi zaidi wawe na fursa ya kupata elimu ya afya ya kisaikolojia.