Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-17 18:08:33    
Watu wa fani mbalimbali wa Kenya wakaribisha kufunguliwa kwa kituo cha FM cha Radio China Kimataifa Nairobi Kenya

cri

Tarehe 27 Februari mwaka huu, sherehe rasmi ya kuzinduliwa kituo cha kwanza cha FM cha Radio China Kimataifa kilichoanzishwa katika nchi ya nje kilifanyika rasmi huko Nairobi, Kenya. Kituo hicho kinatangaza kwa saa 19 kwa lugha ya Kiingereza, saa tatu za matangazo ya lugha ya Kiswahili na saa 3 za matangazo ya lugha ya Kichina. Vipindi vya matangazoya kituo hicho vinahusu ujenzi wa uchumi, maendeleo ya jamii na utamaduni wa China, mawasiliano ya kirafiki kati ya China na Kenya na nchi nyingine za Afrika, matukio makubwa yaliyotokea duniani na burudani za muziki na nyimbo za China, Afrika na duniani. Wasikilizaji wa Kenya pia wanaweza kuwasalimia jamaa na marafiki zao kwa kupitia matangazo ya kituo hicho.

Kuzinduliwa kwa kituo cha FM cha Radio China Kimataifa kumewavutia watu wa fani mbalimbali nchini Kenya. Waziri wa habari wa Kenya Bwana Mutahi Kagwe alipotoa hotuba kwenye tafrija ya uzinduzi wa kituo cha FM cha Radio China Kimataifa alisema:

"Matangazo ya radio ni njia muhimu ya mawasiliano, kuzinduliwa kwa kituo cha FM cha Radio China Kimataifa Nairobi kumefungua dirisha kwa watu wa Kenya kufahamu historia na utamaduni wa China na maendeleo ya mambo ya kisasa ya China."

Bw. Kagwe alisema serikali ya Kenya itaendelea kuunga mkono kituo cha FM cha CRI Nairobi, na kutarajia kuimarisha zaidi mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika eneo la upashanaji habari.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Utangazaji la Kenya Bwana Wachira Waruru alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema:

"Sisi kwa KBC tumefurahia sana hayo maendeleo. Uhusiano kati ya KBC na CRI umekuwepo kwa muda mrefu sana. Uhusiano huo sio wa upande mmoja, pande zote mbili zinanufaika sana, kwa sababu uhusiano huo umetuletea vyombo vya utangazaji. Hata Kenya yenyewe itanufaika kwa sababu wameleta vifaa vya uhusiano wa hali ya juu. CRI ina vipindi kuhusu mambo ya maendeleo na teknolojia. China imeendelea sana kwa teknolojia kwa hivyo tumenufaika sana kwa matangazo ya CRI."

Mwenyekiti wa shirikisho la Wakenya waliosoma nchini China Bwana Franklin Asira alisema:

"Kuzinduliwa kwa kituo cha FM cha Radio China Kimataifa ni mafanikio makubwa. Baada ya kurudi nchini Kenya sisi bado tunafuatilia sana mambo ya China, lakini hatukuwa na njia sahihi. Sasa daraja hilo limeanzishwa, tunaona kuwa, kuanzisha kwa kituo cha FM cha CRI hapa Kenya ni hatua ya busara, kituo hicho si kama tu kitafupisha umbali kati ya watu wa Kenya na watu wa China, bali pia kitasaidia kukuza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili."

Meneja aliyeshughulikia matangazo ya radio ya KBC Bwana John Osoro alisema:

Waandishi wa habari wa Kenya walisema kuwa, kuzinduliwa kwa kituo cha FM cha Radio China Kimataifa ni maendeleo mazuri, wakisema:

Mkuu wa shirikisho la wachina wanaoishi nchini Kenya, ambaye pia ni mkuu wa shirikisho la kuhimiza muungano wa amani la China nchini Kenya Bwana Han Jun alisema:

"Kuzinduliwa kwa kituo cha FM cha Radio China Kimataifa nchini Kenya ni jambo zuri sana kwa wachina wanaoishi nchini humo. Natoa pongezi kubwa kwa kuzinduliwa kwa kituo cha FM cha Radio China Kimataifa kwa niaba ya shirikisho la wachina wanaoishi nchini Kenya. Pia natumai kuwa, kituo hicho kitatangaza vipindi vingi zaidi kuhusu maisha ya wachina wanaoishi nchini Kenya na nchi nyingine duniani. Tutaimarisha mawasiliano kati yetu kwa kupitia Radio China Kimataifa."

Mjumbe wa wachina wanaoishi nchini Kenya Bwana Meng Shutian alisema:

"Nilifurahi sana niliposikiliza sauti kutoka China kwa mara ya kwanza, ni furaha kubwa kwa wachina wanaoishi katika nchi za nje kupata matangazo ya lugha ya kichina kupitia mitabendi ya FM. Hivi sasa kila ninapoendesha gari huwa nasikiliza matangazo ya Radio China Kimataifa. Natumai kuwa vipindi vya CRI vitakuwa vizuri siku hadi siku."

Naibu mkuu wa chuo cha Confucious cha chuo kikuu cha Nairobi Bi. Song Lixian alisema, hivi sasa watu wengi wa Kenya wanataka kujifunza lugha ya Kichina, alitarajia kufanya ushirikiano na idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa katika kutunga vipindi vya Jifunze Kichina, na kuchapisha vitabu vya "Jifunze Kichina".

Idhaa ya kiswahili 2006-03-17