Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-21 10:38:21    
Mapishi ya kamba wenye ladha ya pilipili hoho

cri

Mahitaji

Kamba gramu 200, kiasi kidogo cha pilipili hoho, pilipili manga, tangawizi, vitunguu maji na vitunguu saumu, sukari, chumvi, mchuzi wa soya, na mvinyo wa kupikia.

Njia

1. Kata kamba kwa kisu kwenye gamba lake, kata tangawizi, vitunguu maji na vitunguu saumu viwe vipande.

2. washa moto tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe na joto la nyuzi 80, tia kamba korogakoroga, halafu tia pilipili hoho na pilipili manga, korogakoroga kwa haraka, tia vipande vya tangawizi na vitunguu saumu, korogakoroga. Tia mchuzi wa soya, sukari na mvinyo wa kupikia, korogakoroga halafu tia vipande vya vitunguu maji korogakoroga na tia chumvi. Kisha upakue. Kufikia hapa kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.