Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-21 16:46:36    
China yajenga reli ya pili ya sumaku na kuinua kiwango cha teknolojia ya sekta hiyo

cri

Katika mawasiliano kwenye reli za aina mbalimbali, reli ya sumaku ina umaalum wa kusaidia hifadhi ya mazingira, ujenzi wake unatumia ardhi kidogo, na mwendo kwenye reli ya sumaku ni wa kasi. Miaka mitatu iliyopita, China iliingiza teknolojia ya ujenzi wa reli ya sumaku kutoka Ujerumani, ikaanza kujenga reli ya kwanza ya sumaku mjini Shanghai. Hivi karibuni China imeidhiisha tena ujenzi wa reli ya pili ya sumaku kutoka Shanghai hadi Hangzhou, ili kuinua kiwango cha teknolojia hiyo nchini China.

Njia hiyo ya reli ya sumaku itaunganisha mji wa Shanghai na mji wa Hangzhou mkoani Zhejiang, kusini magharibi ya Shanghai, reli hiyo itaanza kazi rasmi kabla ya kufunguliwa kwa maonesho ya makumbusho ya Shanghai mwaka 2010. Ujenzi wa reli hiyo utakapokamilika, safari ya kwenda Hangzhou kutoka Shanghai itakuwa ya muda wa nusu saa tu, na hivi sasa muda huo wa haraka zaidi ni saa mbili. Hivyo habari hiyo imewafurahisha sana wakazi wa miji ya Shanghai na Hangzhou. Mkazi wa Shanghai Bwana Zhou Hongwei ana matarajio makubwa sana na ujenzi wa reli hiyo akisema:

Hivi sasa bado ni vigumu kwenda Hangzhou kutoka Shanghai, hata tukiendesha gari kwenda huko bado ni vigumu. Reli ya sumaku ya kutoka Shanghai hadi Hangzhou ikikamilika, sisi wakazi wa Shanghai tutakuwa tumepata urahisi zaidi, kwenda na kurudi tutahitaji saa moja tu. Hivyo tunaunga mkono ujenzi wa mradi huo, na tunatarajia kuwa ujenzi wa reli hiyo utakamilika mapema iwezekanavyo.

Naibu meya wa Mji wa Hangzhou Bwana Sheng Jifang alisema:

Ujenzi wa reli hiyo ya sumaku utaonesha umuhimu wake kwa ujenzi wa mji wa Hangzhou, maendeleo ya mji na maendeleo ya uchumi na jamii ya Hangzhou, kwani reli hiyo itaufanya mji wa Hangzhou ujulikane zaidi; aidha umbali mfupi kati ya miji hiyo miwili utawawezesha wakazi wa miji hiyo miwili waone kama waishi katika mji mmoja.

Reli hiyo itakayojengwa kuanzia mwaka huu itakuwa na urefu wa kilomita 175, gharama za mradi huo zitafikia fedha za renminbi Yuan bilioni 35. Profesa wa chuo kikuu cha mawasiliano cha Beijing Bwana Ji Jialun anaona kuwa, kujenga reli ya sumaku kati ya Shanghai na Hangzhou, mbali na sifa mbalimbali ya reli ya sumaku yenyewe, mradi huo pia una umuhimu wa kufanyiwa majaribio. Alisema:

Kujenga reli ya sumaku kati ya miji hiyo miwili kweli kutafanya ujenzi wa majaribio, kama uzoefu mwingi utapatikana, siku hadi siku uzoefu huo utaendelea kutumika katika sehemu mbalimbali, halafu China itafanya tena uvumbuzi wa kiteknolojia, na kiwango cha teknolojia kuhusu reli ya sumaku nchini China kitainuliwa kwa kiasi kikubwa.

Habari zinasema kutokana na ujenzi wa mradi huo, China inatazamiwa kudumisha nguvu yake ya kuongoza duniani kwenye sekta hiyo, hali hii itasukuma mbele maendeleo ya kasi ya mawasiliano ya reli na shughuli zinazohusika.

Idhaa ya Kiswahili 2006-03-21