Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-21 19:42:56    
"Mapinduzi ya rangi" yamegonga mwamba nchini Belarus

cri

Tume ya uchaguzi ya Belarus tarehe 20 ilitangaza kuwa, rais wa sasa wa Belarus Bw Alexander Lukashenko alipata 82.6% ya kura za ndiyo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 19, hivyo atakuwa rais wa awamu ya 3 ya nchi hiyo. Belarus ni nchi nyingine ya Jumuiya ya madola huru inayosema "hapana" kwa "mapinduzi ya rangi".

Wachambuzi wanaona sababu za kuendelea na urais kwa awamu nyingine kwa rais Alexander Lukashenko ni kama ifuatavyo:

Kwanza, katika miaka 12 iliyoptia tangu Lukashenko achukue wadhifa wa urais, Belarus ilidumisha ongezeko la kasi la uchumi. Hivi sasa pato la nchi hiyo limedumisha wastani wa ongezeko la 7%, tena katika miaka mitano iliyopita wastani wa ongezeko la mshahara wa watu wa nchi hiyo uliongezeka kwa mara dufu; kiwango cha kiinua mgongo cha uzeeni pia kinaongezeka hatua kwa hatua. Mambo hayo yamemwezesha Lukashenko kuwa na msingi madhubuti wa imani ya watu.

Pili, katika miaka mingi iliyopita, nchi za magharibi zimekuwa zikiiwekea nchi hiyo vikwazo vya kisiasa na kiuchumi, kwa kiwango fulani vikwazo hivyo vinawachukiza watu wa nchi hiyo na kutopenda mtazamo wa thamani na wazo la demokrasia ya magharibi. Nchi zile zilizokumbwa na "mapinduzi ya rangi" zimekuwa na hali mbaya ya kiuchumi na kijamii, hivyo watu wa Belarus wamekuwa na makini na uangalifu mkubwa zaidi juu ya "mapinduzi ya rangi".

Ya mwisho, kuchaguliwa tena kwa kura nyingi kwa Lukashenko kunatokana na uungaji mkono mkubwa wa Russia. Kwa mfano mwanzoni mwa mwaka huu, Russia haikuweka bei kubwa ya gesi ya asili ya nchi hiyo inayosafirishwa nchini Belarus, wakati bei ilipandishwa kwa gesi iliyouza kwa Ukraine na nchi nyingine.

Tarehe 20, Lukashenko alipoonana na waandishi wa habari wa nchi mbalimbali alitangaza kwa sauti kubwa, "Mapinduzi ya rangi" yaliyopangwa na baadhi ya watu yameshindwa nchini Belarus, na tena hayatatokea tena!"

Kuhusu matokeo ya uchaguzi huo, Russia, Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zina maoni tofauti kabisa. Wizara ya mambo ya nje ya Russia tarehe 20 ilitangaza kuwa hakuna mashaka yoyote kwa uhalali wa matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Belarus. Rais Putin wa Russia siku hiyo alitoa pongezi kwa Bw Lukashenko kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo katika ujumbe aliomtumia.

Lakini msemaji wa Ikulu ya Marekani Scott McClellan siku hiyo alisema, kuna udanganyifu na ukiukaji wa haki za binadamu katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Belarus, Marekani inakataa matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo. Aliongeza kusema, Marekani inaunga mkono pendekezo lililotolewa la kutaka ufanyike upya uchaguzi nchini humo, na kuwa pamoja na Umoja wa Ulaya kufikiria kuchukua hatua za kuweka vikwazo kwa shughuli za utalii na mambo ya fedha kwa maofisa waliofanya udanganyifu nchini Belarus katika uchaguzi mkuu.

Hivi sasa nchini Belarus kiongozi wa kundi la upinzani Alexander Milinkevich ametoa wito wa kutaka watu wafanye maandamano barabarani na kuonesha malalamiko yao. Lakini, wachambuzi wanaona, itakuwa ni vigumu sana kwa makundi ya upinzani kuanzisha wimbi lingine ya "mapinduzi ya rangi" nchini Belarus.

Idhaa ya Kiswahili 2006-03-21