Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-22 19:30:49    
Mapishi ya matango machungu pamoja na nyama iliyosagwa

cri

Mahitaji:

Matango machungu mawili, nyama iliyosagwa gramu 300, uyoga gramu 25, yai moja, mchuzi wa soya gramu 15, wanga gramu 25, maji ya wanga gramu 10, vitunguu saumu gramu 50, pilipili manga gramu 1, M.S.G gramu 1, chumvi gramu 2, mafuta ya ufuta gramu , mafuta gramu 500

Njia:

1. kata matango machungu yawe vipande vyenye urefu wa 4sm, na ondoa vitu vya ndani, uviweke kwenye maji, baada ya kuchemka, vipakue halafu vikaushe.

2. kata uyoga uwe vipande, koroga yai, halafu koroga yai pamoja na nyama iliyosagwa, wanga, maji ya wanga, chumvi na vipande vya uyoga. Halafu weka kwenye vipande vya matango machungu.

3. Washa moto tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu saumu, korogakoroga, halafu tia vipande vya matango machungu, vikaange mpaka viwe na rangi ya manjano, kisha vipakue kwenye sahani, mimina mchuzi wa soya, weka kwenye chungu chenye maji, na baada ya maji kuchemka pakua.

4. Tia mafuta kwenye sufuria tena, washa moto, mimina maji yaliyochemshwa kwenye chungu, tia M.S.G na maji ya wanga, pilipili manga korogakoroga, baada ya kuchemka mimina kwenye vipande vya matango machungu. Mimina mafuta ya ufuta, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

Idhaa ya Kiswahili 2006-03-22