Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-24 19:57:20    
Bw. Su Huajie "balozi wa kiraia" kati ya China na Afrika ya kusini

cri

Bwana Su Huajie alizaliwa nchini China, aliwahi kujiendeleza nchini Thailand, na mwaka 1975 alikwenda Afrika ya Kusini akaanzisha kampuni ya kimataifa ya Xiangfa ya Afrika ya kusini. Katika miaka mingi iliyopita, alijishughulisha kuhimiza mawasiliano kati ya Afrika ya kusini na China katika sekta za uchumi, biashara, utamaduni na jamii, ni mkuu wa shirikisho la kuhimiza biashara kati ya Afrika ya kusini na China.

China ilipoanza kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, Bw. Su Huajie alianza kufanya biashara na China. Mwaka 1991, kutokana na msaada na mpango wa Bw. Su Huajie, wizara ya uchumi na biashara na nje ya China ilianzisha kampuni ya Changcheng nchini Afrika ya kusini. Hii ni kampuni ya kwanza iliyoanzishwa na serikali ya China nchini humo.

Mwaka 1992, Bw. Su Huajie alirudi China kuwekeza vitega uchumi, akiwa mwanakampuni wa kwanza wa Afrika ya Kusini kuwekeza nchini China. Alianzisha shughuli nyingi ambazo ni pamoja na ujenzi wa nyumba, bidhaa za elektroniki, mikahawa, usimamizi wa majengo, na elimu. Pia amechanga fedha nyingi kuanzisha mfuko wa elimu nchini China kuwasaidia watoto waliokosa nafasi ya kwenda shule, na kuunga mkono taasisi ya utafiti ya China kuhusu mambo ya nchi za Afrika.

Ili kuhimiza biashara kati ya Afrika ya kusini na China, Bw. Su Huajie alisajili kampuni ya kimataifa ya Huajin ya Afrika ya kusini, akiwa wakala pekee wa makampuni makubwa 41 ya kitaifa ya China katika Afrika ya kusini na barani Afrika. Mwezi Novemba mwaka 2002, Bw. Su Huajie alianzisha kampuni ya uwekezaji ya kimataifa ya Huajie ya China katika mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong, ambayo imefanya kazi nyingi za utafiti kuhusu miradi zaidi ya 6000 ya hifadhi ya mazingira, madini, usafirishaji kwa njia ya bahari, na tekinolojia mpya ya juu. Katika ripoti yake iliyokabidhiwa kwenye baraza la serikali la China aliainisha kuwa, kuhifadhi mazingira, kutumia malighafi zinazoweza kutumika tena badala ya plastiki, ili kutokomeza uchafu mweupe ni mapinduzi mapya ya teknolojia katika Karne ya 21.

Juhudi alizofanya Bwana Su Huajie katika kuhimiza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika ya kusini zimesifiwa sana na watu wa fani mbalimbali za Afrika ya kusini. Alichukuliwa kama "mjumbe wa urafiki wa China". Kwa mfano kabla China kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Afrika ya kusini, kila alipokwenda kufanya biashara na kampuni ya chuma cha pua ya Colombia ya Afrika kusini, ambayo ni kampuni maarufu sana nchini humo, Bw. Su Huajie alikuwa hupewa heshima ya kupandishiwa bendera ya China.

Bwana Su Huajie alisifiwa kuwa ni mtu wa kwanza aliyeshughulikia ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika ya kusini.

Akiwa mkuu wa shirikisho la kuhimiza biashara la Afrika ya kusini na China, Bwana Su Huajie alikuwa ametoa mchango mkubwa katika kuhimiza kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Afrika kusini. Si kama tu amechanga fedha nyingi katika kuanzisha shughuli za aina mbalimbali za kijamii, pia aligharamia mwenyewe kupokea ujumbe zaidi ya 30 wa ngazi ya juu wa China. Pia aliwafahamisha watu wa Afrika ya kusini hali ya China na kuwagharimu wajumbe wa fani mbalimbali za Afrika ya Kusini kuitembelea China, ili kuzidisha maelewano kati ya nchi hizo mbili. Pia ametoa mchango mkubwa katika kuwafahamisha watu wa China mambo ya Afrika ya kusini, na kukuza uhusiano wa kirafiki kati ya China na nchi za Afrika, kuhimiza maendeleo ya biashara kati ya China na Afrika ya kusini na kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.

Bw. Su Huajie pia aliongoza kuanzisha shirikisho la wafanyabiashara wa China wanaoishi nchini Afrika ya kusini, ambalo limetoa mchango mkubwa katika kuwahimiza wachina wanaoishi nchini Afrika ya kusini waishi maisha mazuri zaidi na kujiendeleza vizuri nchini humo, na limekuwa daraja la kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na maingiliano ya sayansi na tekinolojia na utamaduni kati ya China na Afrika ya kusini.

Kutokana na mafanikio yake makubwa ya kibiashara na mchango mkubwa alioutoa katika kuhimiza uhusiano wa kibalozi na ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika ya kusini, na kati ya China na Namibia, kuhimiza mshikamano mkubwa wa wachina wanaoishi kote duniani, na kupinga shughuli za kuifanya Taiwan ijitenge na China, Bwana Su Huajie amepata heshima kubwa, si kama tu amepewa sifa mbalimbali nchini China na nchini Afrika ya kusini, bali pia amewahi kuonana na viongozi wa nchi nyingi, na karibu kila mwaka anaalikwa na waziri mkuu wa China kuhudhuria karamu ya taifa la China.

Idhaa ya kiswahili 2006-03-24