Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-24 18:45:00    
Watu wa Russia wasifu Shughuli za "Mwaka wa taifa" wa Russia na China na uhusiano kati ya nchi hizo mbili

cri

Rais Vladimir Putin wa Russia hivi karibuni alifanya ziara nchini China, ziara yake imeanzisha shughuli za "mwaka wa taifa" wa China na Russia. Katika miaka miwili ijayo, wananchi wa China na Russia wataongeza maelewano na urafiki kwa kupitia shughuli mbalimbali za "mwaka wa taifa". Watu wengi wa Russia walipohojiwa na mwandishi wetu wa habari walisifu sana shughuli hizo na kuwa na matarajio mengi juu ya kuendeleza zaidi uhusiano kati ya China na Russia.

Ruslan ni mhandisi kutoka Russia, ameeleza imani yake kuwa ziara ya rais Putin na shughuli za "mwaka wa taifa" za Russia na China, zitaleta manufaa mengi zaidi kwa maendeleo ya uchumi wa nchi hizo mbili na kuboresha maisha ya wananchi wa nchi hizo mbili. Alisema:

Naona ziara ya rais Putin nchini China ni ishara kubwa kwa maendeleo mapya ya uhusiano kati ya Russia na China, pia ni hatua moja kubwa ya Russia na China kuzidisha maendeleo ya ushirikiano katika sekta za uchumi na biashara, sayansi na teknolojia. Shughuli za "mwaka wa Russia" zilizoanzishwa mjini Beijing si kama tu ni hatua muhimu ya nchi hizo mbili kufanya maingiliano kwenye sekta ya utamaduni, bali pia zimeleta fursa mpya kwa ushirikiano kati ya Russia na China kwenye sekta za uchumi, uzalishaji na biashara, hizo zote zitasukuma zaidi ongezeko la thamani ya biashara ya nchi hizi mbili, na kusaidia kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wa Russia na China.

Bi. Lyudmila ni mwanafunzi wa mwaka wa 4 katika chuo kikuu, naye anapenda sana utamaduni wa China. Alipozungumzia maendeleo ya uhusiano wa Russia na China alisema kwa furaha kubwa:

Nafurahia ziara ya rais Putin nchini China. Russia imepata mengi kutoka utamaduni wa China katika maendeleo yake. Najua wananchi wa China wanawapenda wananchi wa Russia, na wananchi wa Russia pia wanawapenda wananchi wa China. Hisia hizo nzuri zitaleta athari zenye juhudi kwa ushirikiano kati ya Russia na China kwenye sekta za uchumi na biashara. Natumai kuwa Russia na China zitadumisha ushirikiano wenye mafanikio katika sekta zote.

Bwana Nikolay ni meneja mmoja wa kampuni moja ya dawa ya Moscow, anatarajia sana uhusiano kati ya Russia na China uweze kuendelea vizuri akisema:

China ni nchi nzuri, maendeleo ya China yana mustakbali mzuri. Rais Putin ameitembelea China mara 6, hii imeonesha kuwa Russia inatilia maanani uhusiano kati ya Russia na China. Naona Russia na China zingeendelea kukuza urafiki na uhusiano wa kibiashara.

Na wakazi kadha wa kadha wa Russia pia wanatarajia maendeleo ya uhusiano kati ya Russia na China yatawaletea manufaa halisi.

Bi. Kristina ni mwanafunzi wa chuo kikuu, mbali na kusoma kozi maalum, pia anashiriki somo la kujifunza kichina. Anafuatilia sana maendeleo ya uhusiano wa Russia na China na mafanikio ya ziara ya Putin nchini China, pia anatarajia zaidi urafiki kati ya Russia na China utamletea mustakbali mzuri na fursa kubwa. Alisema:

Rais Putin ameitembelea China mara nyingi, ziara ya hivi karibuni ni muhimu zaidi, kwani katika ziara yake hiyo Russia na China zimesaini mikataba mingi kuhusu ushirikiano wa viwanda na biashara. Naamini mikataba hiyo itatuletea wanafunzi wa Russia tunaosoma kichina fursa nyingi na mustakbali mzuri.

Na wakazi wengine wa Moscow wanaona kuwa wananchi wa kawaida wa Russia na China wanapaswa kuongeza mawasiliano na maelewano, ili kusaidia kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Idhaa ya Kiswahili 2006-03-24