Wasikilizaji wapendwa, uchaguzi wa bunge la awamu ya 17 la Israel utafanyika tarehe 28. Vyombo vya habari nchini Israel vinaona, uchaguzi huo utavunja muundo wa siasa ya jadi nchini Israel, ambapo hali ya mambo kati ya Palestina na Israeli huenda itakuwa na mabadiliko ya kihistoria. Waandishi wetu wa habari hivi karibuni waliwahoji wasomi na wachunguzi wa mambo ya kisiasa wa Israel na Palestina, na kuwaomba waeleze maana ya uchaguzi huo kwa watu wa Israel pamoja na athari yake kwa hali ya mashariki ya kati.
Wataalamu waliohojiwa wamesema, uchaguzi huo ni uchaguzi usioweza kutokewa na mambo yasiyotazamiwa. Kutokana na matokeo ya kura za maoni ya raia, uungaji mkono kwa chama cha Kadima kinachoongozwa na kaimu waziri mkuu wa Israel Bw. Ehgud Olmert unaongoza moja kwa moja na kuuzidi sana ule wa wapinzani wake muhimu, chama cha Leba cha mrengo wa kushoto na Chama cha Likud cha mrengo wa kulia. Mhariri mahiri wa zamani wa gazeti la "Jerusalem Post" Bw. Calev Ben-David alisema,
"Hata kama uungaji mkono kwa chama cha Kadima unaendelea kupungua, lakini uungaji mkono kwa chama hicho bado bado unaongoza."
Profesa wa kitivo cha siasa cha chuo kikuu cha Hebrew Bw. Reuven Hazan alisema,
"Chama cha Kadima bila shaka kitashinda katika uchaguzi mkuu, itakuwa si kitu kwa chama hicho kupata viti kadhaa zaidi au kupata pungufu ya viti kadhaa, hakuna chama kingine kinachoweza kukishinda chama hicho."
Bw. Ben-David alisema, uchaguzi wa safari hiyo utaunda upya muundo wa siasa nchini Israel.
"Muundo wa siasa nchini Israel utatokewa na mabadiliko makubwa ya kimsingi kutokana na uchaguzi mkuu wa safari hiyo. Tokea miaka mingi iliyopita Israel ilitawaliwa kwa zamu na chama cha Likud na chama cha Leba, lakini kujinyakulia utawala wa nchi kwa chama cha Kadima kunamanisha kuwa hali hiyo imefikia mwisho. Hayo yatakuwa mabadiliko makubwa kabisa kutokea katika muundo wa siasa nchini Israel tangu chama cha Leba kipoteze hadhi yake ya kuhodhi utawala wa kisiasa mwaka 1977."
Profesa wa chuo kikuu cha Hebrew Bw. Reuven Hazan alieleza kuwa, "Uchaguzi huo utaamua mipaka na muundo wa idadi ya watu ya Israel katika siku za baadaye. Endapo chama cha Kadima kitashinda katika uchaguzi mkuu, na kuunda serikali ya umoja pamoja na chama cha Leba au chama kingine cha kisiasa, basi watu watajua shabaha la Israel katika miaka minne ijayo, yaani wakazi wa nchi hiyo wataondoka kwenye ardhi inayokalia Palestina. Huu ni uamuzi wa kihistoria na ni maana muhimu ya uchaguzi huo."
Licha ya hayo wataalamu wa Israel wanaona, kuingia madarakani kwa kundi la Hamas, ambalo linajulikana kuwa na msimamo mkali wa kisiasa, kunachangia serikali na jamii ya Israel kujichukulia uamuzi kuhusu suala la amani la mashariki ya kati. Hivyo endapo chama cha Kadima, ambacho kimesema kitajichukulia uamuzi, kitashinda katika uchaguzi, basi mchakato wa amani ya mashariki ya kati hautawa wa kufurahisha. Mtaalamu wa mambo ya siasa na uhusiano wa Isreal Bw. Lior Charev alisema, "Kushinda kwa kundi la Hamas kwenye uchaguzi wa kamati ya utungaji sheria ya Palestina, kunamaanisha kutokea kwa mabadiliko makubwa ya kisiasa kwenye sehemu ya mashariki ya kati. Sera za kimkakati za Israel pia zitabadilika kutokana na hali hiyo. Kusema kwa maana fulani, mpango wa 'ramani ya njia' wa mashariki ya kati umekuwa si kitu muhimu. Israel haitaki kutupilia 'ramani ya njia', lakini hali halisi ni kuwa uwezekano wa kukubaliana na 'ramani ya njia' na masharti ya Israel ni mdogo sana."
Baada ya uchaguzi mkuu wa Israel, mustakabali wa mchakato wa amani utakabiliwa na matatizo mengi, kwani hadi leo hii Israel bado haijakitambua chama cha Hamas, ambacho kitatawala hivi karibuni, tena Hamas pia inakataa kuitambua Israel.
|