Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-28 16:14:14    
Wajasiriamali wa nchini na wa nchi za nje wavutiwa na viwanda vyenye maendeleo makubwa vya China

cri

Katika kipindi hiki cha nchi yetu mbioni tutazungumzia hali ya uwekezaji wa wajasiriamali kwa viwanda vyenye maendeleo makubwa. Katika miaka ya karibuni pamoja na maendeleo endelevu ya uchumi wa China, kila mwaka kulikuwa na viwanda vingi vipya vilivyojengwa, kati ya viwanda hivyo kuna baadhi ya viwanda vinavyoweza kuwa na maendeleo makubwa na kupata faida, vinapendwa na wajasiriamali wa nchini na wa nchi za nje. Kwa mfano, kampuni ya Baidu ya utafutaji wa habari kwenye tovuti ya lugha ya kichina na kampuni ya vifaa vya elektroniki ya Zhongxing, ambayo inafanya utafiti kuhusu Coms chips za multi-media, ziliwekezwa vitega-uchumi na wajasiriamali wa nchini na wa nchi za nje.

Naibu mkurugenzi mkuu wa kamati ya usimamizi ya eneo la ustawishaji wa teknolojia ya kisayansi la Zhongguancun Bw. Guo Hong alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, katika miaka miwili iliyopita, kila mwaka kulikuwa na viwanda vipya 4,000 vilivyojengwa kwenye eneo hilo, vyenye pato la wastani wa Yuan zaidi ya milioni 100 vilifikia 100, ongezeko la kasi la pato la kampuni linawavutia wajasiriamali wengi wa nchini na wa nchi za nje, Bw. Guong Hong alisema,

"Takwimu za taarifa ya uwekezaji nchini zinaonesha kuwa, kampuni na viwanda 72 vya Beijing, ambavyo vingi viko Zhongguancun, vilivutia uwekezaji kutoka nchi za nje wa dola za kimarekani milioni 378 mwaka uliopita, ukichukua nafasi ya kwanza nchini, na kuzidi jumla ya uwekezaji wa Shanghai na mkoa wa Jiangsu, ambazo zilichukua nafasi ya pili na tatu."

Katika miaka ya karibuni, sekta za Internet, mawasiliano ya habari ya simu za mkononi na software zilikuwa na maendeleo ya haraka, kampuni na viwanda vingi kati yao vyenye maendeleo makubwa vilifuatiliwa zaidi na wajasiriamali wa nchi za nje. Kutokana na kushawishiwa na mustakabali wa kupata faida kubwa, mashirika mengi ya uwekezaji yaliingia kwenye soko la China na kutafuta kampuni na viwanda vyenye uwezo mkubwa wa maendeleo.

Kampuni ya takwimu ya kimataifa ya Marekani inayojulikana kwa IDG ni shirika la uwekezaji la kimataifa lililoingia China mapema zaidi. Baada ya kuingia kwenye soko la China mwaka 1992, shirika hilo liliwekeza katika viwanda zaidi ya 150 vya China, hususan kampuni na viwanda vyenye teknolojia ya sayansi ya kisasa. Naibu mkurugenzi mkuu wa idara ya uwekezaji kwa uanzishaji wa kampuni za teknolojia ya kampuni ya takwimu ya kimataifa ya Marekani Bw. Li Jianguang alisema,

"Eneo hasa tunalowekeza ni eneo la teknolojia ya mawasiliano ya habari. Kwanza kabisa ni Internet. La pili, ni nyongeza ya thamani ya uhamiaji, yaani baadhi ya shughuli zenye nyongeza ya thamani zinazohusika na Internet. Tatu, ni software. Nne ni huduma na teknolojia zinazohusika na mawasiliano ya habari. Hapo nyuma, zaidi ya 90% ya mitaji yetu iliwekezwa katika maeneo hayo manne."

Bw. Li Jianguang alisema, faida tunayopata kutokana na uwekezaji wetu nchini China ni kiasi cha 40%, ambacho ni kikubwa zaidi kuliko faida tunayopata nchini Marekani. Katika miaka mitatu au minne ijayo, kampuni yetu itawekeza dola za kimarekani milioni 500 hadi 600 nchini China.

Hivi sasa, kampuni za uwekezaji za kimataifa zinazowekeza nchini China ni zaidi ya 30, ambazo zile zenye uchangamfu zaidi ni pamoja na The WIHARPER GROUP, Soft Bank ya Japan na kampuni ya Goldman Sachs. Kampuni hizo ziko kwenye maeneo ya yenye shughuli nyingi za kiuchumi na maeneo ya ustawishaji wa sayansi na teknolojia kwa kufuatilia baadhi ya miradi yenye mustakabali mzuri wa maendeleo. China imekuwa sehemu inayofuatiliwa sana na wajasiriamali duniani.

Kampuni na viwanda vyenye maendeleo makubwa vya China si kama tu vinavutia uwekezaji wa wajasiriamali wa nchi za nje, bali pia vinavutia wafanyabiashara wawekezaji wa China. Kampuni ya uwekezaji ya Infotech ni kampuni ya uwekezaji nchini, ambayo ilianzishwa mwaka 2,000, kampuni hiyo inawekeza zaidi katika maeneo ya mawasiliano ya habari yakiwa ni pamoja na njia ya mzunguko ya umeme (electric circuit), software na vipuri. Naibu meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Zhou Ning alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari, alisema,

"Kampuni imewekeza katika baadhi ya miradi, ambayo moja ya miradi hiyo ilianza kuuza hisa zake katika soko la Nasdaq, hiyo ni kampuni ya usanifu wa Com Chips, na ni kampuni ya kwanza ya usanifu wa Com Chips ya nchini iliyoingia soko la Nasdaq. Huo ni mradi mzuri, umekuwa na ufanisi mzuri wa kiuchumi, faida tunayopata kutokana na uwekezaji pia ni nzuri."

Kampuni ya Com Chips iliyowekezwa na kampuni ya Infotech ni kampuni ya elektroniki ya Zhongxing, ambayo ilianza kuuza hisa zake kwenye soko la Nasdaq nchini Marekani mwishoni mwa mwaka uliopita, Com Chips zilizozalishwa na kampuni hiyo zilipata tuzo ya ngazi ya kwanza la maendeleo ya sayansi ya teknolojia ya China mwaka 2004, na ni kampuni yenye maendeleo makubwa inayoongoza nchini China. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1999, bidhaa za kampuni hiyo zimezidi 70% ya nafasi ya soko la dunia.

Hivi sasa, wajasiriamali wa nchini na wa nchi za nje wanajitahidi kutatufa nafasi ya uwekezaji mbali na maeneo ya teknolojia ya mawasiliano ya habari, tena wanarekebisha sera na upendeleo wao katika uwekezaji. Kwa mfano, kampuni ya takwimu ya kimataifa ya Marekani licha ya kuendelea kuwekeza katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano ya habari, inapanua uwekezaji wake hadi sekta ya burudani katika miaka miwili iliyopita, wakati kampuni ya uwekezaji ya Infotech inaanza kufuatilia aina mpya ya nishati, na uzalishaji wa vifaa vipya na dawa za viumbe (biological).

Wakati kampuni za uwekezaji zinavivutia viwanda na kampuni za China, baadhi ya maeneo ya uzalishaji mali ya teknolojia ya kisasa yanajitahidi kuvutia uwekezaji mwingi zaidi. Naibu mkurugenzi wa kamati ya usimamizi ya eneo la teknolojia ya sayansi la Zhongguancun la Beijing, Bw. Guo Hong alisema, katika miaka ya karibuni, eneo la sayansi na teknolojia la Zhongguancun lilichukua hatua kadha wa kadha na kujitahidi kuanzisha mazingira bora ya uwekezaji yakiwa ni pamoja na kuanzisha mazungumzo ya uwekezaji kila baada ya kipindi maalumu na kutoa mkopo wa mwanzo kwa kuvutia uwekezaji zaidi.

Kama lilivyo eneo la sayansi na teknolojia la Zhongguancun la Beijing, eneo la sayansi na teknolojia ya kisasa la Shanghai katika kipindi cha ujenzi pia linafanya utafiti na kutafuta njia ya uwekezaji, kuimarisha wazo la uwekezaji wenye hatari na kuanzisha mazingira ya uwekezaji wenye hatari. Mbali na kuvutia uwekezaji wa wajasiriamali, Shanghai na Beijing zinajitahidi kuvutia mitaji ya uvumbuzi ya viwanda vya wastani na vidogo vya serikali, mitaji ya uvumbuzi wa huko huko na kuanzisha kampuni za uwekezaji kwa kuanzisha kampuni ili kuunga mkono maendeleo ya kampuni za sayansi na teknolojia kwa njia mbalimbali.

Idhaa ya kiswahili 2006-03-28