Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-28 18:31:05    
Uchaguzi mkuu wenye maana kubwa

cri

Tarehe 28 ni siku ya upigaji kura ya uchaguzi mkuu nchini Israeli. Baadhi ya wachambuzi wanaona, katika uchaguzi huo kura za wapiga kura mamilioni kadhaa nchini Israel si kama tu zinaweza kuanzisha kipindi kipya kabisa cha siasa, bali pia zinaweza kuthibitisha mwelekeo wa maendeleo ya nchi hiyo, hata ya sehemu ya mashariki ya kati.

Gazeti moja nchini Israel "Jerusalem Post", hivi karibuni lilichapisha makala ikisema, huu ni uchaguzi unaolingana na chaguzi kuu tatu zilizoleta mabadiliko makubwa ya kihistoria nchini Israel. Wa kwanza ni ule uliofanyika mwaka 1977, ambapo chama cha Likud kilimaliza hali ya nchi hiyo kutawaliwa moja kwa moja na chama cha Leba tangu kuasisiwa nchi hiyo, na kuanzisha hali mpya ya siasa ya nchi hiyo kutawaliwa kwa zamu na vyama hivyo viwili muhimu; ule uchaguzi muhimu uliofanyika mwaka 1992, chama cha Leba kilichoongozwa Yitzhak Rabin kilishinda na kuanzisha mchakato wa amani wa Oslo; katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2003 Ariel Sharon alishinda na kuchukua madaraka ya utawala, alibatilisha mkataba wa Oslo na kuanza kutekeleza kwa nguvu hatua ya kuondoka sehemu ya Gaza kwa upande mmoja wa Israel.

Kitu kinachofuatiliwa zaidi na watu katika uchaguzi mkuu wa safari hii ni chama cha Kadima, ambacho ni chama chenye msimamo wa katikati kilichoanzishwa nusu mwaka uliopita. Kaimu waziri mkuu wa Israel Bw. Ehud Olmert alinyanyuka katika hali ya kuweko vyama viwili vya jadi vya mrengo wa kushoto na mrengo wa kulia, akijumuisha matakwa ya kisiasa ya baadhi ya vyama na makundi ya kisiasa, na kuwa nguvu kubwa ya kisiasa. Kura za maoni ya raia zinaonesha kuwa chama cha Kadima kitavishinda kwa urahisi chama cha Likud cha mrengo wa kulia na chama cha Leba cha mrengo wa kushoto.

"Utarejeshewa Israel moja tofauti" ni kauli-mbiu ya chama cha Kadima, "Kuondoka peke yake kwa Israel na kuthibitisha mipaka ya baadaye ya Israel" ni mpango wa vitendo wa chama hicho. Chama cha Kadima kimeunganisha msimamo wenye siasa ya upole wa kidiplomasia wa chama cha Leba na msimamo wenye siasa kali wa mrengo wa kulia, katika kampeni ya uchaguzi kilitoa mwongozo wa kuendelea kuondoka peke yake kutoka baadhi ya makazi madogo yaliyoko kwenye kando ya magharibi ya mto Jordan, kuimarisha makazi makubwa yenye umuhimu wa mkakati wa kivita, ili kuthibitisha mpaka wa baadaye kati ya Israel na Palestina. Wachunguzi wa mambo ya kisiasa nchini Israel wanasema, kunyanyuka kwa chama cha Kadima kunaonesha hali halisi ya siasa na imani ya watu wa Israel, ambayo imeweka njia ya kisiasa kwa madai ya umma wenye msimamo wa kati yaliyokuwepo kwa miaka mingi. Kuondoka kutoka sehemu kubwa inayokalia, kuruhusu Palestina kuanzisha nchi yake, na kutatua kwa kiwango fulani mgogoro kati ya Palestina na Israel ili kuwa na hali tulivu ya muda katika sehemu hiyo kumekuwa imani muhimu ya umma.

Wachunguzi wanasema, endapo chama cha Kadima kitachukua madaraka ya serikali bila matatizo na kuunda serikali kwa kushirikiana na makundi ya mrengo wa kushoto yenye misimamo ya kisiasa ya karibu kikiwemo chama cha Leba, basi "kuondoka kwa upande mmoja kwa Israel" kutakuwa sauti kubwa katika uhusiano kati ya Palestina na Israel katika miaka kadhaa ijayo, wakati mpango wa "ramani ya njia" ya amani ya mashariki ya kati itazidi kufifia. Chanzo cha kutokea kwa hali ya namna hiyo ni mambo mawili. Jambo la kwanza: jamii ya Israel inaona, kuchukua madaraka ya nchi kwa chama cha upinzani cha kiislamu, Hamas, kumefanya Israel kupoteza nafasi ya mazungumzo ya amani; La pili, kundi la Hamas na Israel zote zinakataa kutatuliana kati yao, hali ambayo inaweza kufanya Marekani na Umoja wa Ulaya kufikiria kuwa vitendo vya upande mmoja wa Israel ni mpango pekee unaoweza kukwamua hali ya sehemu hiyo.

Hata hivyo hivi sasa kuna vitu vingi vinavyohusika na kufanikiwa kwa mpango wa kuondoka kwa upande mmoja wa Israel. Ili kupata nafasi kubwa ya usuluhisho, chama cha Kadima bado hakijaondoa uwezekano wa kuwa na mazungumzo na upande wa Palestina.

Vyombo vya habari nchini Israel vinasema, wachunguzi wa siasa wa Israel wamesema, bila kujali chama kipi kinashinda katika uchaguzi mkuu, mustakabali wa Israel utakabidhiwa kwa watu wa kizazi kipya.