Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-28 20:21:15    
"Made in China" inavutia zaidi katika maonesho makubwa ya kimataifa mjini Hannover, Ujerumani

cri

Maonesho makubwa ya kimataifa ya teknolojia ya mawasiliano ya habari yaliyofanyika mjini Hannover, Ujerumani, tarehe 15 yamefungwa. Mashirika 6,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani yalihudhuria maonesho hayo ya siku saba. Kwenye maonesho hayo bidhaa zilizobuniwa na kuoneshwa na mashirika 1,300 kutoka China bara, Taiwan na Hong Kong zilivutia zaidi.

Kwenye maonesho, China ilikuwa ni nchi ya pili iliyoonesha bidhaa za aina nyingi baada ya Ujerumani kama ilivyokuwa mwaka jana, na kwa mara ya kwanza sehemu zote za mabanda ya maonesho ya ujumbe wa China zilipambwa kwa sare na kwa rangi ya aina moja nyekundu. Bidhaa zilizooneshwa na mashirika ya Huawei na Aigo zinaongoza katika teknolojia na zote zinabuniwa na kutengenezwa na China, "Made in China" ilikuwa na maana mpya. Meneja wa kitengo cha Ulaya katika Shirika la Huawei Bw. Yao Weijie alisema,

"Bidhaa zote zinazooneshwa hapa tulizibuni na sisi wenyewe, shirika letu linatilia mkazo zaidi katika utafiti na ubunifu wa bidhaa, karibu nusu ya wafanyakazi wanafanya kazi ya utafiti, na fedha zisizopungua 10% za shirika letu zinatumika katika kazi hiyo.

Hapo kabla ukumbi Nam.1 ulitumiwa tu na mashirika makubwa ya kimataifa, lakini mwaka huu mashirika ya China pia yamekuwa na nafasi kwa kwa kuwa na bidhaa zao zenye hakimiliki. Aigo ni chapa ya bidhaa za Shirika la Huaqi. Meneja wa kitengo cha mambo ya nje katika shirika hilo Bw. Zhou Zongwu alisema,

"Bidhaa zilizoshiriki katika maonesho hayo zina sifa mbili. Moja ni kuwa tumeongeza huduma zilizoongeza thamani ya hard ware. Na pia tumezalisha bidhaa za hard ware, na kuongeza huduma za kuhifadhi muziki kwenye MP3 na MP4. Katika siku hizi ambapo ushindani umekuwa mkubwa kati ya MP3 na MP4, teknolojia yetu ya kunganisha soft ware na hard ware inavutia sana."

Sifa nyingine ni kamera ya kitarakimu inayoweza kuchapa tarakimu kwenye picha na inaweza kuonekana chini ya mwangaza. Kwa mujibu wa maelezo ya Bw. Zhou Wuzong, picha zilizopigwa kwa kamera hiyo zinaweza kuhakikishwa kama ziliwahi kuhaririwa au kufanyiwa mabadiliko, kwa hiyo inaweza kwa uhakika kuhifadhi ukweli wa picha zenyewe na hakimiliki. Hivi sasa teknolojia hiyo inaongoza duniani.

Kabla ya hapo, bidhaa za China zilizouzwa katika nchi za nje zilikuwa zikifikiriwa kuwa ni "bidhaa za kuigwa", lakini sasa kwa kuonesha bidhaa za mashirika ya Huawei na Huaqi kwenye maonesho makubwa ya kimataifa, wateja wa nchi za nje wamekuwa na imani kubwa zaidi na bidhaa zinazotengenezwa China, bidhaa za China zinasifiwa zaidi. Bw. Zhou Zongwu alisem,

"Lengo letu la kushiriki katika maonesho hayo ni kuwaonesha watazamaji bidhaa za chapa ya China, mashirika yenye hakimiliki za bidhaa yanaongezeka siku hadi siku nchini China. Baada ya kushiriki kwenye maonesho hayo kwa miaka mine, tumeona kwamba wateja wengi hawakuwa kama walivyokuwa miaka miwili iliyopita kwamba walidhani sisi ni Wajapan au watu wa Korea ya Kusini. Tunataka kuwafahamisha kuwa sisi ni Wachina, na mashirika ya China pia yanaweza kuzalisha bidhaa zenye uvumbuzi duniani."

Mejena mkuu wa kitengo cha nchi za nje katika Shirika la Xiaxin Bw. Xu Zhaohui alisema, mabadiliko makubwa ya uzalishaji wa bidhaa yanatokana na kuwa, mashirika ya China yanataka kubadilisha "iliyotengenezwa China" iwe "iliyobuniwa China".

"Bidhaa zilizotengenezwa China zinajulikana kwa wateja wengi duniani, lakini kitu tunachotaka ni kuigeuza 'bidhaa zilizotengenezwa China' kuwa 'bidhaa zilizobuniwa na China' ". Hii ni hatua kubwa ya kuinua hadhi ya mashirika ya uzalishaji bidhaa nchini China.