Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-29 20:59:34    
Ehud Olmert akabidhiwa majukumu makubwa

cri

Kaimu waziri mkuu wa Israel, ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Kadima Bw. Ehud Olmert tarehe 28 usiku alitangaza, chama cha Kadima kimepata ushindi katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, kwa kupata viti vingi zaidi katika bunge la taifa, na kupata haki ya kuunda baraza la mawaziri la serikali ya awamu ijayo.

Kutokana na utaratibu wa kisiasa wa Israel, katika hali ya kawaida matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu hutangazwa katika wiki moja inayofuata, ambapo rais atafuata matokeo ya mashauriano na wawakilishi wa vyama mbalimbali walioko katika bunge na kumteua mwenyekiti wa chama kilichopata kura nyingi zaidi kuwa waziri mkuu, ambaye atakabidhiwa madaraka ndani ya siku 42 kuunda baraza jipya la mawaziri. Wachambuzi wanasema, baada ya Bw. Olmert na chama cha Kadima anachokiongoza kushika madaraka ya utawala, atabeta majukumu makubwa na kukabiliana na changamoto kubwa.

Ingawa kura za maoni zilizopigwa kabla ya uchaguzi mkuu zinaonesha kuwa chama cha Kadima kilipata uungaji mkono mkubwa kuliko vyama vingine vya kisiasa, hivyo ni dhahiri kwa chama hicho kupata ushindi katika uchaguzi kama ilivyotarajiwa na watu. Lakini uchunguzi wa mwanzo umeonesha kuwa kiasi cha watu waliokwenda kupiga kura ni kidogo zaidi kuliko chaguzi zilizofanyika hapo nyuma. Kura kilizopata chama cha Kadima pia zilikuwa kidogo ikilinganishwa na kura zilizotarajiwa. Katika bunge lenye viti 120, chama cha Kadima kimepata viti kati ya 29 na 32, wakati chama cha Leba cha mrengo wa kushoto kimepata viti 20 hadi 22, na chama cha Likud kilichoundwa miaka mingi iliyopita kilipata viti 11 hadi 12 tu, chama cha Yisrael Beiteinu kinachodai kuchukua msimamo mkali cha mrengo wa kulia kimepata viti 12 hadi 14. Kimepata uungaji mkono chini ya kiwango kilichotarajiwa, hali ya kisiasa yenye matatizo mengi itaongeza shida kwa utawala wa siku za baadaye wa Olmert.

Jambo la haraka kwa hivi sasa ni kwa Olmert kuanza kujadiliana na vyama mbalimbali vya kisiasa nchini Israel na kuunda serikali ya umoja haraka iwezekanavyo. Wachambuzi wa mambo ya kisiasa nchini Israel wamesema, kushinda kwenye uchaguzi mkuu kwa chama cha Kadima ni kama kupanda kwenye kidato cha kwanza cha utawala, na itakuwa ni vigumu kwa chama hicho kuunda serikali tulivu na yenye umoja. Kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu, Bw. Olmert aliwahi kusema wazi kuwa yeyote anayetaka kushiriki katika serikali ya umoja, hana budi kuunga mkono mpango wake wa kuendelea kuondoka kutoka kwenye sehemu ya kando ya magharibi ya mto Jordan, na Israel kuweka peke yake mpaka wa baadaye kati ya Israel na Palestina. Uchunguzi wa mwanzo unaonesha, chama cha Kadima na vyama vingine vya mrengo wa kushoto visivyopinga mpango wa kuondoka kwa upande wa Israel peke yake vimepata zaidi ya nusu ya idadi ya viti vya bunge. Hivyo kuunda serikali mpya kwa kushirikiana na vyama vya mrengo wa kushoto ni chaguo zuri kwa chama cha Kadima.

Jukumu lingine muhimu ni kwa Olmert kuendelea kudumisha umoja ndani ya chama cha Kadima. Ndani ya chama hicho kuna mzee wa chama cha Leba Shimon Peres, vilevile kuna wanachama muhimu wa Likud akiwemo waziri wa mambo ya nje Tzipi Livni, ambao walikuwa pamoja kwa kuvutiwa na Ariel Sharon. Lakini watu hao wana misimamo inayotofautiana kidogo. Sasa bado haijatimia nusu mwaka tangu chama cha Kadima kianzishwe, namna ya kusawazisha mitazamo tofauti ya kisiasa na madai ya maslahi yao ni shida kubwa kwa Olmert, ambaye hana uzoefu mkubwa kwenye shughuli za kisiasa.

Kabla ya uchaguzi mkuu, Bw Olmert alitoa mpango kamili wa kuondoka kwa Israel peke yake na kuahidi kuwa baada ya kumaliza kipindi chake cha utawala, "mipaka ya Israel itakuwa tofauti sana na ile ya sasa". Hivi sasa chama cha Kadima kimeshinda katika uchaguzi, Olmert anatakiwa kutimiza ahadi alizotoa katika kampeni ya uchaguzi. Sasa bado inasubiriwa kama Bw Olmert anaweza kuondoa vikwazo vingi na kutekeleza ahadi zake au la.