Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-03-29 21:32:56    
Mapishi ya supu ya slesi ya nyama ya kuku

cri

Mahitaji

Nyama ya kuku gramu 75, paja gramu 15, uyoga gramu 15, ute wa yai moja, wanga gramu 20, chumvi gramu 5, unga wa pilipili manga gramu 5

Njia

1. kata nyama ya kuku iwe vipande vidogovidogo, koroga pamoja na ute wa yai na wanga, halafu uviweke kwenye maji joto, korogakoroga vipakue.

2. kata paja na uyoga viwe vipande vidogovidogo, washa moto mimina maji kwenye sufuria baada ya kuchemsha, tia vipande vya paja na uyoga, tia chumvi na unga wa pilipili manga, korogakoroga tia vipande vya nyama ya kuku, kisha korogakoroga na ipakue. Mpaka hapo supu hiyo imekuwa iko tayari kuliwa.