Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-05 14:11:57    
Chama cha Kadima cha Israel na Chama cha leba cha Israel vyashirikiana kuunda baraza la mawaziri

cri

Chama cha Kadima cha Israel na Chama cha Leba cha Israel tarehe 4 vimetangaza kuwa vitashirikiana kuunda baraza la mawaziri, hali hii itakomesha hali ya kuchuana kati ya vyama hivyo viwili kwa ajili ya kugombea madaraka ya kuunda baraza la mawaziri, na kutandika njia ya kumwezesha kaimu waziri mkuu Olmert kuunda serikali ya Israel itakayofuata msimamo wa katikati na kuelekea mrengo wa kushoto kidogo.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika siku hiyo na Mwenyekiti wa chama cha Kadima cha Israel Ehud Olmert pamoja na mwenyekiti wa chama cha leba Amir Peretz, Bwana Olmert alisema, rais Moshe Katsav akimpa madaraka rasmi madaraka ya ya kuunda baraza la mawaziri, mara atafanya mashauriano na chama cha Leba kuhusu suala la kuunda serikali ya shirikisho. Alisema chama cha Leba kitakuwa mwenzi muhimu wa chama cha Kadima katika utawala wa serikali. Mwenyekiti wa chama cha Leba Bwana Peretz alisema, ili kuharakisha mchakato wa kuunda baraza la mawaziri, atamshauri rais Katsav ampe Bw Olmert madaraka ya kuunda baraza la mawaziri.

Katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Machi, chama cha Kadima kinachoongozwa na Bw Olmert kilipata viti 29, na kimekuwa chama kikubwa cha kwanza kwenye bunge, na chama cha Leba kimepata viti 20. Baada ya kumalizika kwa uchaguzi, vyama hivyo viwili vilichuana kugombea madaraka ya kuunda baraza la mawaziri. Ofisa wa chama cha Leba alisema, ingawa waziri mkuu huwa ni kiongozi wa chama kikubwa cha kwanza kwenye bunge, lakini sheria ya kimsingi ya Israel haisemi kuwa ni lazima kumwacha kiongozi wa chama kikubwa cha kwanza aunde baraza la mawaziri, hivyo chama cha Leba kitashirikiana na vyama kadhaa vya mrengo wa kulia pamoja na chama cha Likud kuunda "umoja wa jamii". Kwa kuwa umoja huo utaweza kuwa na nusu zaidi ya viti kwenye bunge, chama cha Leba kinaona kuwa serikali itakayoundwa kwenye msingi wa "umoja wa jamii" itakuwa ya utulivu zaidi kuliko serikali itakayoundwa na chama cha Kadima. Na chama cha Kadima kilifanya chini juu kushikilia kuunda baraza la mawaziri peke yake. Wakati michuano kati ya vyama hivyo viwili ilipokuwa inafuatiliwa na watu, pande hizo mbili zilitangaza ghafla kuunda baraza la mawaziri, habari hiyo iliwashangaza watu wengi pamoja na wanachama wa chama cha Leba. Ofisa mwandamizi wa chama cha Leba alisema, chama cha Leba kilipendekeza kuunda "umoja wa jamii", hili ni "pazia la moshi" tu, chini ya pazia hilo, chama cha Kadima na chama cha Leba kwa kweli siku zote vilifanya mawasiliano faraghani.

Wachambuzi wanaona kuwa, mwenyekiti wa chama cha Leba Bwana Peretz aliacha kuunga "umoja wa jamii" na kukubali kushirikiana na chama cha Kadima katika utawala wa serikali, kwa sababu tatu. Kwanza, chama cha Leba ni chama kikubwa cha pili kwenye bunge, kikishirikiana na vyama na vikundi vingine kitakabiliwa na taabu kuwa kujipatia nusu zaidi ya viti kwenye bunge. Pili, mpango wa kuunda baraza la mawaziri uliotolewa na chama cha Leba ulikosolewa na vyombo vingi vya habari nchini Israel. Kabla ya kampeni za uchaguzi, Bwana Peretz alitangaza wazi kuwa kama atapata madaraka ya kuunda baraza la mawaziri, hatashirikiana na vyama vya mrengo wa kulia hasa chama cha Likud katika kuunda baraza la mawaziri. Lakini baada ya kumalizika kwa uchaguzi, alikialika kwanza chama cha Likud kuunda "umoja wa jamii", kitendo chake hicho kilivichukiza sana vyombo vya habari vya Israel. Na tatu Bwana Peretz hana uzoefu mkubwa wa kisiasa, si rahisi kwake kushika wadhifa wa waziri mkuu.

Na Bwana Olmert anataka kuunda serikali ya shirikisho ili iwe uhakikisho wake wa kutekeleza mpango wa upande mmoja na kuthibitisha mpaka kati ya Palestina na Israel. Wachambuzi wanaona kuwa, vyama hivyo viwili vikishirikiana kuunda baraza la mawaziri, ni chaguo zuri na vyama hivyo viwili kutapata ushindi kwa pamoja.

Idhaa ya kiswahili 2006-04-05