Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-10 16:08:15    
Mlima Lushan China

cri

Mlima Lushan uko kwenye kitongoji cha Mji wa Jiujiang, mkoani Shanxi, kandokando ya Ziwa Boyang ambalo ni ziwa kubwa la kwanza nchini China, sehemu hiyo ina mvua nyingi na hali ya hewa fufutende inayofaa kwa maisha ya watu. Katika siku za mchipuko, hali joto kwenye sehemu za milimani ni tofauti sana, ambapo kuna mawingu na ukungu mwingi kwenye sehemu za milimani.

Katika majira ya mchipuko, huko sehemu ya Mlima Lushan, kila ukienda, popote utaona bahari ya mawingu. Na kwenye kilele cha mlima watalii wanaweza kutazama vizuri zaidi bahari ya mawingu. Asubuhi mapema, mawingu na ukungu hutanda juu kwa taratibu, na baadaye kuufunika Mlima Lusha ndani ya bahari ya mawingu. Ukiangalia kutoka chini ya mlima, utaona kilele cha mlima kinaonekana huku kinatoweka, na ukiangalia chini kutokea kileleni, utaona chini ni bahari kubwa ya mawingu, unaweza kujisikia kuwa kama unarukaruka ndani ya mawingu. Baadhi ya wakati ukungu hutanda juu ya mlima, na mvua ya manyunyu ilinyesha chini ya mlima; na wakati mwingine, ukungu na mawingu yakitoweka yote, utaona mandhari murua ya sehemu hiyo ya Mlima Lushan.

Bwana Li Wenliang ni mzaliwa wa sehemu ya Mlima Lushan, alimwambia mwandishi wetu wa habari:

Ukifanya utalii kwenye Mlima Lushan mwezi Machi au mwezi Aprili, ni bora uishi juu ya mlima. Asubuhi ukiamka na kutoka nje, utaona mawingu na ukungu pote mlimani, baadhi ya wakati hata unaweza kusahau uko wapi, ukijisikia kama unaelea, na unaweza kupata hisia za raha.

Kwa kuwa sehemu ya Mlima Lu ina mawingu mengi na ukungu mwingi, hivyo hata chai inayozalishwa na sehemu hiyo inaitwa Chai ya mawingu na ukungu. Chai hiyo ina sifa nzuri ambayo si kama tu inauzwa nchini China, bali pia inasafirishwa nchini Japan, Ujerumani, Korea ya kusini, Marekani na Uingereza. Mwanzoni mwa mwezi Aprili kila mwaka ni majira mazuri ya kuchuma majani ya chai hiyo, hivyo watalii wengi wakienda Mlima Lushan hununua chai hiyo ili kuwazawadia jamaa na marafiki zao nyumbani.

Hali ya hewa pekee ya Mlima Lushan inaifanya mimea ya sehemu hiyo isitawi vizuri. Hivi sasa maua mengi ya aina mbalimbali yanachanua vizuri kwenye sehemu ya Mlima Lushan.

Bustani ya mimea ya Lushan iliyojengwa mwaka 1934 ni bustani ya mimea iliyojengwa mapema zaidi kuliko nyingine zote nchini China, bustani hiyo inastahili kutembelewa na watu. Kwenye bustani hiyo kuna sehemu mbalimbali za miti, mimea inayositawi kwenye chumba chenye hali joto, mimea inayokua kwenye sehemu yenye matope, bustani ya chai na bustani ya mitishamba, kweli kuna mimea mingi inayopendeza ambayo inastawi kwenye bustani hiyo. Kutokana na takwimu zilizokusanywa, katika bustani hiyo imekusanyika mimea ya aina zaidi ya 3400 ya China na ya nchi za nje, China imeanzisha uhusiano wa kubadilishana mbegu za mimea na nchi zaidi ya 60. Naibu Mtafiti wa bustani ya mimea ya Lushan Bwana Xu Shangmei amefahamisha kuwa, katika majira ya mchipuko, mimea yote inachipua na kuanza kukua, wakati huo kwenye Bustani ya mimea ya Lushan, mimea ya aina ya misonobari na azalea inasitawi zaidi na kujaa kwenye bustani hiyo. Alisema:

"Mimea tuliyopanda, mingi zaidi ni misonobari na azalea na mimea hiyo tuliingiza kutoka nchi za nje wakati tulipoanzisha bustani ya mimea. Hivi sasa miti mikubwa ndani ya bustani ni ya aina nyingi na karibu yote iliingizwa kutoka nchi za nje."

Nyumba nyingi zinazoonekana katika ukungu na majani, ni sifa nyingine ya mandhari ya Mlima Lushan. Tokea mwaka 1885 mmisionari wa Uingereza alipojenga nyumba ya kwanza mlimani hadi sasa kumekuwa na nyumba zaidi ya 1,000 zenye mitindo ya nchi 18 katika mlima huo, ambazo licha ya kuwepo kwa nyumba za mtindo wa Brazil, pia kuna nyumba zenye mtindo wa kipindi cha ufufuaji wa utamaduni nchini Italia, na licha ya kuwepo kwa nyumba zenye paa za misonge za Ulaya ya Kaskazini, pia kuna nyumba zenye paa lililoinama. Baadhi ya nyumba zilijengwa kileleni na baadhi zilijengwa kando ya michirizi. Nyumba hizo zilizopo ndani ya majani zinavutia sana.

Mtalii Bi. Tang Dongdong mara mbili alifika kwenye Mlima Lushan na kuangalia nyumba hizo kwa makusudi. Alisema nyumba hizo sio tu zilijengwa kwa mitindo tofauti na nyumba hizo zinalingana sana na mazingira, kati ya milima mingi nchini China, ni kwenye Mlima Lushan tu ndipo tunapoweza kuona "kijiji ya kimataifa".

"Mandhari ya nyumba kwenye Mlima Lushan haipatikani mahali pengine, naweza kufahamu hadithi nyingi kutokana na nyumba hizo."

Baada ya kuwaeleza hayo, sasa tuwafahamishe majengo ya kale katika Mlima Lushan. Hekalu la Dalinsi liliwahi kusifiwa na mshairi mkubwa wa kale Bai Juyi akisema, "Harufu nzuri ya mwezi Aprili ilipotoweka, ndipo maua ya pichi yanaanza kuchanua." Hekalu lililojengwa mwaka 1700 ni moja kati ya mahekalu makubwa mlimani Lushan na Chuo cha Bailudong kilikuwa ni nyumba ya kusomea kwa mshairi wa kale Li Bo, ambayo ipo katika mazingira tulivu na miti mingi. Ndani ya hekalu kuna mawe mengi yaliyochongwa mashairi. Hiki ni moja kati ya vyuo vya zamani sana nchini China.

Idhaa ya kiswahili 2006-04-10