Tarehe 9 naibu waziri wa mambo ya ndani wa Iraq Bw. Hussein Ali Kamal alipohojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC alisema, kwa kweli vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea nchini humo katika mwaka mmoja uliopita, vimesababisha waislamu wa madhehebu ya Shia na madhehebu ya Suni, Wakurd, na Wakristo kadhaa kuuawa.
Kabla ya hapo, waziri mkuu wa zamani wa serikali ya muda ya Iraq Bw. Iyad Allawi alisema wazi kuwa, vifo vya watu 50 hadi 60 kila siku vimeonesha kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vimetokea. Lakini waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Iraq bw. Ibrahim al-Jaafari tarehe 9 katika hotuba yake alisema kuwa, Iraq haijajitumbukiza katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Alisema ingawa watu kadhaa wanajaribu kuharibu mshikamano wa Iraq, lakini kwa ujumla Iraq ni nchi kamili, hakuna mtu yeyote anayeweza kusema kuwa mgogoro kati ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na madhehebu ya Suni ni vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katika miaka mitatu iliyopita, migogoro nchini humo iliendelea kupamba moto mgogoro kati ya madhehebu mbalimbali umezidi kuwa mkali, hali ya kisiasa haikuboreshwa, majeshi ya nchi mbalimbali nchini humo hayakuweza kuondoka, na Iraq iko mbali zaidi na hali ya kuwa na demokrasi na uhuru iliyoahidiwa na Marekani na Uingereza.
Kuhusu Iraq inakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe au la, wanasiasa wa Iraq wana maoni tofauti. Wakati inapokaribia siku ya kutimiza miaka mitatu tangu serikali iliyoongozwa na Saddam Hussein ilipinduliwa, watu wanaona kuwa, baada ya vita vya Iraq kumalizika, migogoro iliendelea kutokea nchini humo. Kwanza migogoro ilitokea kati ya makundi ya madhehebu ya Suni na madhehebu ya Shia na majeshi yanayoikalia Iraq; baada ya majeshi ya Marekani na Uingereza kuikabidhi Iraq mamlaka, hasa baada ya serikali ya mpito kuundwa mwaka jana, migogoro ya kunyang'anya madaraka kati ya madhehebu ya Shia, madhehebu ya Suni na Wakurd imekuwa mkondo mkuu nchini humo. tarehe 22 mwezi Februari, mashambulizi dhidi ya msikiti wa Ali al-Hadi ambao ni msikiti mtakatifu wa madhehebu ya Suni yalisababisha mgogoro mkubwa kati ya madhehebu ya Shia na madhehebu ya Suni, na kusababisha vifo vya watu mamia kadhaa. Hivi karibuni mashambulizi dhidi ya majengo mengi ya madhehebu ya Shia yamesababisha hali ya wasiwasi ya Iraq kuwa mbaya zaidi.
Hali mbaya ya usalama yamesababisha wananchi wa Iraq kuishi katika hali ya wasiwasi katika miaka mitatu iliyopita. Jamaa zao kuweza kurudi nyumbani kwa usalama ni matumaini yao makubwa. Wakati inapotimiza miaka mitatu tangu serikali iliyoongozwa na Saddam Hussein ilipopinduliwa, Wairaq wanaona kuwa hivi sasa hali mbaya ya usalama na matatizo ya kuunda serikali mpya yameonesha kuwa, Iraq ikikaliwa na majeshi ya nchi za nje, hali yake itakuwa mbaya zaidi.
Wakati huo, mchakato wa kisiasa nchini Iraq inakabiliwa na matatizo mengi. Hivi sasa kazi ya kuunda serikali mpya inakwama, makundi mbalimbali bado hayajaafikiana kuhusu mgombea wa waziri mkuu wa serikali mpya.
Shirikisho la mshikamano wa Iraq ambalo ni chama kikubwa cha madhehebu ya Shia katika bunge la Iraq tarehe 12 lilimteua Bw. Ibrahim al-Jaafari kuwa mgombea wa waziri mkuu wa serikali mpya. Lakini vyama vya madhehemu ya Suni na Wakurd vinapinga kithabiti. Vinalaani kuwa Bw. Jafaari alipokuwa waziri mkuu wa serikali ya mpito, hakuweza kuhakikisha usalama na utulivu nchini Iraq, serikali za Marekani na Uingereza pia zinashuku Bw. Jafaari ana uwezo wa kushika wadhifa huo au la. Katika hali hiyo, wanachama wa Shirikisho la mshikamano la Iraq pia wana maoni tofauti. Baadhi yao walitoa mwito wazi kumtaka ajiuzuru. Kuhusu mashinikizo hayo, Bw. Jafaari anapinga kithabiti, na kutaka kutatua suala hilo kwa kuamuliwa na bunge, lakini bado hakuna dalili ya kutatuliwa kwa suala hilo.
Yote hayoi yameonesha kuwa, baada ya miaka mitatu tangu serikali iliyoongozwa na Saddam Hussein kupinduliwa, hali nchini Iraq bado ni mbaya. Jambo muhimu ni kuwa madhehebu mbalimbali lazima yazingatie zaidi maslahi ya taifa badala ya kupambana wenyewe kwa wenyewe, ama sivyo migogoro mingi na mikubwa zaidi itatokea nchini humo.
Idhaa ya Kiswahili 2006-04-10
|