Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-11 16:38:04    
China yaboresha mazingira ya mambo ya fedha sehemu ya vijiji

cri

Katika miaka ya karibuni serikali ya China ilitenga fedha nyingi mwaka hadi mwaka kwa sehemu ya vijiji nchini. Lakini katika sehemu nyingi za China, wakulima waliotajirika wamekumbwa na tatizo moja jipya, ambalo ni shida kwao kukusanya mitaji. Wakulima wanapotaka kupanua uzalishaji mazao au wakati wanapokumbwa na maafa ya kimaumbile si rahisi kwao kupata mitaji kwa njia ya kukusanya mitaji isipokuwa kutoka kwa serikali au kupewa fedha za kupunguza athari za maafa. Ili kutatua suala hilo, serikali ya China imeanza kuboresha mazingira ya mambo ya fedha kwenye sehemu ya vijiji na kuwasaidia wakulima kupanua njia ya ukusanyaji mitaji.

Mkoa wa Hainan, ambao uko kwenye sehemu ya kusini kabisa nchini China, idadi ya wakazi wa sehemu ya vijiji inachukua 60% ya idadi ya watu wa mkoa huo mzima. Katika miaka ya karibuni pamoja na maendeleo ya uvuvi kwenye bahari ya mbali, wavuvi wa mkoa wa Hainan wanatarajia kubadilisha mashua zao za uvuvi kuwa mashua za chuma cha pua zenye uwezo mkubwa wa kukabiliana na upepo na mawimbi. Lakini gharama ya mashua moja ya uvuvi ya chuma cha pua yenye uwezo wa kubeba uzito wa tani 100 ni kiasi cha Yuan milioni 2, ambayo hesabu hiyo kubwa inaonekana kama ni hesabu katika elimu ya anga kwa wavuvi. Mvuvi wa mji wa Sanya, mkoani Hainan Bw. Lin Mingfang alieleza shida za wavuvi.

"Wavuvi wote wanataka kuwa na mashua kubwa, shida ni fedha."

Shida ya mvuvi Lin Mingfang inaonesha baadhi ya matatizo yaliyoko katika mfumo wa mambo ya fedha kwenye sehemu ya vijiji nchini China. Benkii nyingi za biashara za China hazipendi kutoa mikopo kwa wakulima na miradi ya kilimo, na aina za bima zinazotolewa na kampuni ya bima kwa wakulima pia ni chache sana. Mkurugenzi wa idara ya utafiti wa uchumi wa sehemu ya vijiji ya ofisi ya utafiti wa maendeleo ya baraza la serikali Bw. Han Jun alisema,

"Moja ya sababu muhimu ya kuwa na shida kupata mikopo kwa wakulima na viwanda vidogo vya sehemu ya vijiji na muda mrefu kwa benki kurudisha fedha za mikopo, kuwa na faida ndogo, kukabiliwa na hatari kubwa na gharama yake ni kubwa. hivyo benki za biashara hazina shauku ya kutoa mikopo ya kilimo. Mbali na hayo, bima ya kilimo iliwahi kupata maendeleo makubwa, lakini hapo baadaye ilichukuliwa kuwa ni bima ya biashara, ambapo serikali haitoi msaada wowote mwingine ila tu kutoa nafuu katika utozaji kodi, hatua hiyo ilifanya bima ya kilimo kuzorota moja kwa moja, hivi sasa China ni nchi iliyoko nyuma katika maendeleo ya bima ya kilimo miongoni mwa nchi zinazoendelea."

Suala la kuwa nyuma kwa mfumo wa mambo ya fedha kwenye sehemu ya vijiji linafuatiliwa sana na serikali ya China hivi sasa. Katika mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii ya China ya mwaka huu, waziri mkuu Wen Jiabao alisema, serikali itaimarisha mageuzi ya mambo ya fedha na kuboresha mfumo wake kwenye sehemu ya vijiji. Hii inaonesha kuwa serikali ya China imefahamu licha ya kuendelea kuongeza uwekezaji kwa miradi ya kilimo, serikali pia inatakiwa kupanua njia ya kukusanya mitaji ya wakulima, kuwasaidia kukuza uzalishaji mali kwa mbinu ya mambo ya fedha wala siyo kutegemea misaada ya serikali. Naibu spika wa bunge la umma la taifa Bw. Cheng Siwei alisema, uungaji mkono wa mitaji ni kitu muhimu sana kwa maendeleo ya sehemu ya vijiji nchini China.

"Vitu vitatu muhimu kwa maendeleo ya kilimo ni mitaji, nguvukazi na jumla ya vitu vingine husika. Sehemu ya vijiji ina nguvukazi ya kutosha, kitu kinachopungukiwa ni mitaji, sekta ya kilimo hakitaweza kupata maendeleo bila mitaji, hivyo tatizo kubwa la sehemu ya vijiji ni mambo ya fedha, ni lazima kuwawezesha wakulima wanaohitaji mitaji kupata fedha, utatuzi wa suala hilo ni ushirikiano wa pande mbalimbali husika ili kutatua vizuri suala la upungufu wa mitaji la maendeleo ya sehemu ya vijiji."

Wataalamu husika wanaona, moja ya mbinu nzuri ya kupanua njia ya ukusanyaji fedha ya wakulima ni benki za kisera kutoa mikopo kwa wakulima. Benki za kisera zitaanzishwa na serikali, ambazo mitaji yake itatoka katika bajeti ya serikali, lengo la shughuli zake siyo kupata faida, hivyo zinafaa zaidi kukabidhiwa jukumu la kuboresha huduma ya mambo ya fedha katika sehemu ya vijiji. Hivi sasa Benki ya Maendeleo ya taifa, ambayo ni moja ya benki tatu za kisera nchini China, inajaribu kutoa huduma ya mambo ya fedha kwa wakulima. Mkuu wa benki hiyo Bw. Chen Yuan alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa ili kupunguza hatari ya mikopo na gharama ya ukaguzi wa hesabu, Benki ya Maendeleo ikishirikiana na serikali za mitaa imeanzisha jumuiya nyingi za utoaji mikopo, ambazo zinafanya tathimini kuhusu uaminifu na uwezo wa kurudisha fedha kwa wanaotaka mikopo, kisha mikopo inatolewa baada ya ukaguzi wa benki. Bw. Chen alisema, "Tunaimarisha kazi za jumuiya za utoaji mikopo kwa kushirikiana na serikali za mitaa ili kuimarisha msingi wa jumuiya za utoaji mikopo na kuwawezesha baadhi ya wateja wakulima wapate mikopo kwanaza, baada ya kupata njia ya ukusanyaji fedha, tunajitahidi kudumisha mfumo huo wa ukusanyaji fedha, kufanya mnyororo huo usikatike na udumishwe."

Mbali na kutoa uungaji mkono wa mitaji wa kisera, serikali ya China inarekebisha vyama vya ushirika wa fedha vya zamani vilivyoko kwenye sehemu za vijijini. Vyama vya ushirika wa fedha vya vijijini vilianzishwa katika utaratibu wa uchumi wa kimpango, jukumu lake ni kutoa uungaji mkono wa fedha zinazohitajiwa na wakulima washiriki katika shughuli za uzalishaji mali na maisha yao. Kutokana na usimamizi mbaya wa uendeshaji kazi, katika miaka ya karibuni hali ya fedha ya vyama vya ushirika wa fedha vya sehemu ya vijijini haikuwa nzuri, fedha za mikopo mingi hazikuweza kurudishwa. Hivyo serikali ya China iliamua kubadilisha hatua kwa hatua vyama hivyo kuwa benki ya biashara ya sehemu ya vijiji, ikiongozwa na utaratibu mpya wa usimamizi na kuongeza ufanisi wa kazi. Hivi sasa China imeanzisha benki 72 za aina hiyo, ambapo benki nyingine 9 zimepata idhini ya uanzishaji. Katika mahojiano, mwandishi wetu wa habari amefahamishwa kuwa benki za biashara za sehemu ya vijiji zilizomaliza kurekebishwa zinafanya kazi nzuri kwa maendeleo ya kilimo. Mkuu wa benki ya biashara ya sehemu ya vijiji Bw. Ji Weihong alisema, "Hivi sasa mikopo yetu inayotolewa kwa wakulima inachukua 67% ya jumla ya mikopo tunayotoa, sehemu kubwa sana ya mikopo inatumika katika ujenzi wa vijiji."

Wakati tunapotatua tatizo la wakulima la kupata mikopo, sekta ya bima ya kilimo ya China pia inaendelezwa kwa mfululizo. Mwezi Januari mwaka 2005, kampuni ya kwanza ya bima ya kilimo yenye utaratibu wa ushirika ilianzishwa katika mkoa wa Helongjiang, sehemu ya kaskazini mashariki ya China inayojulikana kama Kampuni ya Bima ya Kilimo ya Mwangaza wa Jua, mkulima anatakiwa kulipa 65% ya gharama ya bima, sehemu nyingine ni juu ya serikali na idara ya kilimo ya mkoa huo.

Idhaa ya kiswahili 2006-04-11