Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-11 16:49:50    
Miaka ya Utawala wa Sharon imepita kabisa

cri

Wizara ya Sheria ya Israel tarehe 11 imeamua kutangaza kwamba "Sharon hatakuwa tena na uwezo wa kuwajibika", kwa hiyo miaka ya utawala wa Sharon imepita kabisa.

Tarehe 4 Januari mwaka huu, Sharon alipata ghafla ugonjwa wa kuvuja damu kwenye ubongo na kulazwa hospitali. Ingawa alifanyiwa opresheni mara nane lakini hajazinduka. Mpaka sasa Bw. Ehud Olmert ameshika madaraka badala ya Sharon kwa siku mia moja. Kwa mujibu wa sheria ya Israel, hivi sasa ni lazima kutangaza kuwa "Sharon hatakuwa tena na uwezo wa kuwajibika" ili Olmert awe waziri mkuu rasmi.

Mwezi Februari mwaka 2001 Sharon alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Israel, na alichaguliwa tena katika mwaka 2003. Katika miaka mitano Sharon alipokuwa madarakani hali ya Israel ilikuwa tulivu ambayo haikupatikana katika muda wa miaka zaidi ya kumi kabla ya hapo, lakini uhusiano kati ya Israel na Palestina uliingia katika kipindi cha misukosuko mingi. Katika kipindi chake cha kwanza Sharon aliendelea kutekeleza msimamo mgumu ili kuridhisha hasira iliyokuwa ikiongezeka ya watu wa mrelngo wa kulia na kumpuuza kiongozi wa zamani hayati Arafat, kuitendea Palestina kwa "ngumi ya chuma" na kuifanya Palestina itengwe. Katika kipindi hicho migogoro kati ya Palestina na Israel ilikuwa ikipamba moto. Machoni mwa watu wa mrengo wa kulia, Bw. Sharon ni "mtu pekee anayeweza kuwaletea usalama".

Lakini, baada ya kuchaguliwa tena kuwa waziri mkuu mwaka 2003, Sharon aliuachilia mbali msimamo wa watu wa mrengo wa kulia na kuchukua msimamo wa watu wa mrengo wa kushoto. Bila kujali upinzani mkubwa wa watu wa mrengo wa kulia alishikilia sera ya kuondoa wakazi wa Israel kutoka sehemu ya Gaza, kitendo ambacho ni cha kijasiri kabisa katika historia ya uhusiano kati ya Palestina na Israel, Sharon akabadilisha sifa yake mbaya ya "mchinjaji" alipokuwa uzeeni, na watu wengi waliona kuwa ni yeye tu ndiye aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kuleta mkataba wa amani kati ya Palestina na Israel. Wachambuzi wanaona kuwa Sharon alifanikiwa kufuata maoni ya watu walio wengi yaliyopuuzwa miaka mingi, na alipata imani kubwa ya watu wa Israel.

Katika miezi kadhaa Bw. Sharon alipokuwa mahututi, Israel iliingia kimya katika kipindi cha mwisho cha utawala wake. Mali ya kisiasa aliyoacha Sharon ni fikra zake za kisiasa ziendele kutawala chama alichounda, Kadima, kabla yeye kuwa mgonjwa, na kimepata ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Machi mwaka huu na kuweka sera za kisiasa katika kipindi cha mwisho wake. Rafiki mkubwa wa kisiasa wa Sharon alipokuwa hai Bw. Olmert aliendeleza zaidi "Fikra za Sharon" na kutangaza wazi lengo lake la mwisho la kuendelea kuondoa wakazi wa Israel kutoka sehemu ya Gaza na kuweka wazi mipaka kati ya Israel na Palestina.

Kwenye mkutano wa hadhara Bw. Olmert alisema, kama siku fulani Sharon ataezinduka, atamwambia, "Ndoto yako imetimizwa, chama ulichounda, Kadima, kwa juhudi zako kimekuwa chama tawala na kitaongoza Istael mpaka kufikia lengo lako uliloshindwa kulifikia."

Idhaa ya kiswahili 2006-04-11