Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-11 20:48:35    
China yafuata njia yake ya uvumbuzi katika sekta ya magari

cri

Uzalishaji wa magari unaendelezwa kwa kasi nchini China, na umekuwa moja ya sekta ambazo ni nguzo ya uchumi nchini China, lakini katika miaka mingi iliyopita China haikuwa na magari mengi yenye hataza ya China.

Mwaka 2005 aina mpya zaidi ya 80 za magari yalianza kuuzwa kwenye soko la magari. Lakini magari yenye hataza za China hayakuwa mengi. Hata aina mpya za magari yaliyoanza kuuzwa mwanzoni mwa mwaka huu zilichukua 20% hivi. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa maendeleo ya baraza la serikali Bw. Liu Shijin alipoeleza hali hiyo alisema, gharama pamoja na hatari kubwa ni sababu zinazozuia viwanda vingi visiendelee katika utafiti kuhusu aina mpya za magari.

"Mwanzoni kipindi cha maendeleo ya sekta ya magari ya China, soko la nchini lilikuwa linahitaji magari mengi, viwanda vya magari vya China kwa kuingiza teknolojia ya kawaida kutoka nchi za nje viliweza kuzalisha magari na kupata faida. Kuna machaguo mengi, ambayo ni viwanda vyenyewe kufanya uvumbuzi, lakini vinakabiliwa na matatizo ya upungufu wa mitaji, wataalamu na teknolojia, hivyo viwanda vingi vya magari vilichagua kuchukua nafasi yake katika soko la magari wala siyo kufanya utafiti vyenyewe."

Bw. Liu Shijin alisema kuwa na mauzo mazuri kwa kutegemea kununua teknolojia ya nchi za nje ni sera za muda tu, maendeleo ya sekta ya magari ya China hayana budi kufuata njia ya kufanya uvumbuzi wa China yenyewe na kuwa na teknolojia ya uzalishaji magari ya China peke yake. Serikali ya China imeona umuhimu huo. Mwezi Aprili mwaka 2005 idara kuu ya forodha ya China na wizara ya biashara zilitoa uamuzi kwa pamoja kuongeza ushuru wa vipuri vya magari vinavyoagizwa kutoka nchi za nje. Baada ya maagizo hayo kutolewa, viwanda vya magari vya China vimetambua kuwa kipindi cha kupata faida kwa kuunganisha magari yoyote hapa nchini kinakaribia kwisha.

Wakati viwanda vingi vya magari vya China vilipokuwa na shauku kubwa katika uzalishaji wa magari ya kigeni, kulikuwa na baadhi ya viwanda vichache kabisa ambavyo viliondoka kwenye soko la magari ya kigeni ya viwango vya juu na wastani, na vinajitahidi kufanya utafiti na uvumbuzi kuhusu magari madogo. Mwaka jana idadi ya magari madogo ya Xiali yaliyozalishwa na kampuni ya magari ya Tianjin ilifikia laki 2, ikichukua 30% ya magari madogo ya kiwango hicho. Meneja mkuu wa kampuni ya magari ya Tianjin Bw. Wang Gang aliwaambia waandishi wa habari sababu muhimu za mafanikio yao ni kushikilia kufanya uvumbuzi wa kutengeneza magari yao wenyewe:

"Kwa uchache katika miaka 15 iliyopita tulijiendeleza kwa kutegemea mifumo yetu wenyewe ya utafiti, uzalishaji na usimamizi, tulijiendeleza hatua kwa hatua hadi kufikia kiwango cha leo. Sasa tumekuwa na kiwanda cha uzalishaji wa injini za magari na karakana ya uzalishaji wa transmission pamoja na mfumo kamili wa ununuzi na uuzaji."

Njia ya uvumbuzi ya magari ya Tianjin ilikuwa yenye matatizo mengi. Mwishoni mwa miaka ya 90 ya karne iliyopita na mwanzoni mwa karne hii, magari ya Xiali hayakupata soko kutokana na watu wengi kutoyajua. Kampuni hiyo ya magari haikufa moyo bali iliimarisha nguvu katika uvumbuzi na kujitahidi kuzalisha magari ya kubana matumizi yanayopunguza matumizi ya petroli na utoaji wa moshi, hatimaye yaanza kupendwa na watu. Hivi sasa kampuni ya magari ya Tianjin imeweka lengo la kuuza magari milioni 1 yenye hataza ya China kwa mwaka ifikapo mwaka 2010.

Baada ya kuona mafanikio ya kampuni ya magari ya Tianjin, kampuni nyingi za magari nchini China zilianza kutoa kipaumbele kufanya utafiti na uvumbuzi wake zenyewe katika maendeleo yao ya siku za baadaye. Meneja mkuu wa kampuni ya magari ya Great wall ya China bibi Wang Fengying alisema, "Hivi sasa soko la magari duniani linaona magari ya China ni bora na ya bei nafuu, na pia ni ya kushangaza watu katika maendeleo ya kasi ya teknolojia na ubora wa magari. Ingawa magari ya China siyo ya kiwango cha juu kabisa, lakini yamechukua nafasi kubwa katika soko la magari ya kiwango cha kati."

Ili kutimiza lengo la kufanya uvumbuzi wa magari ya China yenyewe, viwanda ya magari vya China vinatumia mbinu za aina mbalimbali za kukuza uwezo wa uvumbuzi.