Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-12 16:43:47    
Kwa nini Iran yatoa tishio la "uranium safi"

cri

Baada ya rais Mahumd Ahmadinejad wa Iran tarehe 11 kusema kwamba kwa haraka Iran itajiunga na klabu ya kimataifa ya teknolojia ya nyuklia, mara makamu wake Gholamreza Aghazadeh ambaye pia ni mwenyekiti wa shirika la nishati ya atomiki la Iran ametangaza kuwa Iran imefanikiwa kupata 3.5% ya uranium safi.

Tukio hilo la kupata uranium safi kwa Iran linafuatiliwa sana na jumuyia ya kimataifa, kwa sababu lilitokea baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 29 Machi kupitisha kwa kauli moja mwito wa kuitaka Iran isimamishe shughuli za kusafisha uranium, na katibu mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Bw. Mohammed el Baradei kufanya ziara nchini Iran hivi karibuni.

Vyombo vya habari vinaona kuwa ziara ya Baradei ni fursa nzuri kwa kupoza ukali wa mgongano wa suala la nyuklia la Iran. Wachambuzi wanaona, tangazo la Iran la kufanikiwa kupata uranium safi ni "tishio" kwa Bw. Baradei na linaashiria msitari wa mwisho wa Iran katika mazungumzo na Baradei na kuhimiza jumuyia ya kimataifa ikubali uwezo uliopo wa Iran. Kwa mara nyingine imethibitisha kwamba, kuwa na haki ya kutumia nishati ya nyuklia na kulinda maslahi ni mstari wa mwisho wa Iran, na hakika Iran haitarudi nyuma katika suala hilo.

Pamoja na kutangaza kufanikiwa kupata uranium safi, Iran pia inasema itafuata "mkataba wa kutoenea kwa silaha za nyuklia" na nyongeza za mkataba huo. Waziri wa mambo ya nje wa Iran tarehe 11 alipohojiwa na waandishi wa habari alisema, Iran itakuwa na ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, na alitumai Bw. Baradei ataeleza matakwa ya haki ya Iran kwenye ripoti yake baada ya ziara.

Wachambuzi wanaona kuwa msimao wa Iran unaonyumbulika kuhusu suala la nishati ya nyuklia unaonesha sera ya Iran ya kufanya mapambano bila "kuchuna uso" katika suala la nyuklia. Tokea Bw. Ahmadinejad awe rais wa Iran, katika mapambano dhidi ya Marekani na nchi za Ulaya, mbele ya shinikizo, tishio na ushawishi, Iran kwa upande mmoja Iran inataka ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, na kwa upande mwingine Iran inashikilia mstari wake wa mwisho bila kurudi nyuma, na mara kwa mara inazionesha Marekani na nchi za Ulaya nia yake thabiti na uwezo wake wa kuendeleza shughuli zake za nyuklia. Mwanzoni mwa mwezi huu, jeshi la Iran lilifanya mazoezi kabambe ya kivita katika Ghuba ya Uajemi, silaha za aina mpya zimeonekana hadharani zikionesha nguvu zake kubwa za ulinzi wa taifa.

Kuhusua kufanikiwa kwa Iran kupata uranium safi, msemaji wa ikulu ya Marekani alisema, Iran inaendelea kupiga hatua kwenye njia ya makosa. Kadhalika, Uingereza ilisema kitendo hicho cha Iran hakisaidii kitu utatuzi wa suala la nyuklia. Inasemekana kwamba, kuhusu suala la nyuklia la Iran mkutano wa mawaziri wa nchi 25 za Umoja wa Ulaya uliofanyika tarehe 10 kwa mara ya kwanza unafikiria kuchukua hatua mfululizo za kuiadhibu Iran. Hivi karibuni vyombo vya habari vya Marekani pia vilitangaza kuwa serikali ya Bush imekuwa ikiandaa hatua za kijeshi didi ya Iran ikiwemo kutumia silaha za nyuklia kubomoa zana za nyuklia nchini Iran. Lakini kuhusu suala hilo viongozi wa jeshi la Marekani wamekataa, hata hivyo rais Bushi na viongozi wa jeshi la Marekani hawakatai uwezekano wa kuchukua hatua za kila aina katika suala la nyuklia la Iran.

Wachambuzi wanaona, kutokana na nguvu kubwa ya kijeshi ya Iran na nafasi muhimu ya kijiografia katika mkakati wa kivita, na zana zake za kinyuklia zinazotapakaa huku na huko bia kuwa pamoja, itakuwa vigumu kwa Marekani na Israel kuzibomoa. Zaidi ya hayo, hivi sasa Marekani imezama katika matope nchini Iraq, kama ikianzisha vita itazongwa na matatizo mengi zaidi. Isitoshe, nchi za Magharibi zinaona kuwa Iran itatumia miaka tatu hadi kumi kabla ya kuwa na uwezo kamili wa kutangeneza silaha za nyuklia. Kwa hiyo, Marekani na Israel zitakuwa na wakati wa kutosha kuandaa vita dhidi ya Iran. Kutokana na hali hiyo, uwezekano wa kutokea kwa mapambano ya kijeshi katika Ghuba ya Uajemi hivi karibuni ni mdogo sana. Hata hivyo uwezekano wa Marekani na Israel kuchukua hatua za kijeshi kwa ghafla bado upo kufuatia migongano inavyozidi haraka kuwa mikali.

Wachambuzi wanaona kuwa, migongano inayozidi kuwa mikali imeongeza utata wa kutatua suala la nyuklia kwa njia ya kidiplomasia. Kwa hiyo, utatuzi wa suala hilo utakuwa na safari ndefu, pande zote zinapaswa kuwa na subira na kuchukua hatua za kusaidia ili suala hilo litatuliwe kwa njia ya amani.

Idhaa ya Kiswahili 2006-04-12