Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-12 20:12:34    
Supu iliyopikwa kwa doufu na kamba-mwakaje

cri

Mahitaji

Doufu, kamba mwakaje, uyoga na karoti kila kimoja gramu 50, ute wa yai moja, kiasi kidogo cha wanga, mvinyo wa kupikia, unga wa pilipili manga, mafuta ya ufuta, chumvi, sukari

Njia

1. kata doufu na uyoga ziwe vipande, kata karoti iwe vipande vidogovidogo.

2. chemsha maji halafu tia vipande vya doufu kwenye maji, baada ya dakika 2, vipakue. Chemsha maji tena, tia kamba-mwakaje kwenye maji yaliyochemka na korogakoroga, halafu ipakue.

3. koroga vipande vya uyoga na karoti pamoja na wanga, mvinyo wa kupikia, unga wa pilipili manga, chumvi.

4. pasha moto weka mafuta kwenye sufuria, mpaka yawe nyuzi joto ya asilimia 60, weka vipande vya doufu, uyoga, karoti, kamba mwakaje kwenye sufuria korogakoroga, halafu mimina maji, baada ya kuchamsha, mimina maji ya wanga, ute wa yai, korogakoroga kabla ya kupakue mimina mafuta ya ufuta, tia chumvi na unga wa pilipili manga. Mpaka hapo kitoweo hiki kita tayari kuliwa.