|
Vikosi vya upinzani vilivyoongozwa na chama cha upinzani, United Force for Change, tarehe 13 alfajiri vilishambulia N'djamena, mji mkuu wa Chad, vikijaribu kuuteka mji huo na kuipindua serikali. Baada ya mapambano makali ya muda wa saa kadhaa, rais Idriss Deby alitangaza kupitia redio akisema "Jeshi la serikali limeshinda vikosi vya upinzani", mji mkuu N'djamena na hali ya taifa zima iko chini ya udhibiti wa serikali, na uchaguzi mkuu utafanyika katika tarehe 3 Mei kama ulivyopangwa.
Siku moja kabla siku hiyo, wajumbe wa chama cha upinzani huko Paris walitangaza kuwa wamekwisha kudhibiti maeneo ya 80% ya taifa la Chad na wamekuwa wakisogelea mji mkuu N'djamena. Habari nyingine zilisema kuwa vikosi vilivyoshindwa katika mapambano ya mji wa N'djamena sio vikosi vikuu, yaani vikosi vya upinzani vitakuwa tishio kubwa kwa serikali ya Deby.
Wachambuzi wanaona, ushambulizi wa kuuvamia mji mkuu ni tokeo la lazima la shughuli za kupinga serikali zilizoshamiri siku hadi siku. Katika sehemu ya mashariki nchini Chad vikosi kadhaa vilivyoongozwa na chama cha United Force for Change vilikuwa vikishughulika harakati za upinzani kwa muda mrefu. Tokea mwezi Septemba mwaka jana baadhi ya askari wa jeshi la serikali walitoroka na kuunda vikosi vya upinzani katika sehemu ya mashariki ya Chad kwenye Darfur, mpakani kati ya Chad na Sudan, wakidai rais ajiuzulu. Tokea mwezi Machi mwaka jana serikali ya Chad ilifanya msako mara nyingi lakini haikupata matokeo yoyote.
Uchaguzi mkuu wa Chad utafanyika tarehe 3 Mei, rais wa sasa Bw. Idriss Deby atakuwa mgombea urais akitaka kuendelea na urais wake. Rais huyo aliyepata urais katika uasi uliofanyika mwaka 1990 amekuwa mtawala wa Chad kwa miaka 16 sasa, na uchaguzi utakaofanyika mwezi Mei unaonelewa na chama cha upinzani kuwa ni uchaguzi ulio chini ya udhibiti wake, kwa sababu wagombea wengine urais wote wana uhusiano wa karibu na serikali ya Deby, ambao sababu yao ya kugombea urais ni kwa ajili ya kumsaidia Deby aendelee kuwa rais. Ndio kwa sababu hizo, vyama vyote vya upinzani vilishirikiana kuupinga uchaguzi huo, kwa kutumia fursa hiyo, vikosi vya upinzani vilifanya uasi vikijaribu kuuteka mji mkuu na kuipindua serikali.
Msukosuko uliotokea nchini Chad umesababisha uhusiano mbaya kati ya nchi hiyo na Sudan. Katika muda mrefu uliopita nchi hizo mbili zilikuwa mara kwa mara zikishutumiana kusaidia vikosi vya uasi vilivyopo ndani ya kila nchi. Mji mkuu wa Chad uliposhambuliwa, rais Deby aliilaumu serikali ya Sudan ilikodi vikosi vya upinzani wa serikali ya Chad na kufanya njama ya kuipinga. Lakini msemaji wa jeshi la Sudan tarehe 13 alisema Sudan haikuwahi kutoa msaada wowote kwa vikosi vya upinzani wa serikali ya Chad, na serikali ya Sudan haina uhusiano wowote na msukosuko nchini Chad.
Hali ya wasiwasi nchini Chad imevutia uangalifu wa kimataifa, Ufaransa, ikiwa ni nchi tawala ya zamani ya Chad na kuwa na askari wake nchini humo askari 1,200, kwa haraka inaingilia kati. Ofisa mmoja wa wizara ya ulinzi ya Ufaransa tarehe 13 alitangaza kuwa ndege moja ya Ufaransa ilivitupia bomu moja vikosi vilivyokuwa vikisogelea mji wa N'djamena kama ni onyo kwa vikosi vya upinzani.
Aidha, Kamati ya Umoja wa Ulaya tarehe 13 ilitoa taarifa ikisema inafuatilia sana hali ya Chad na kutaka pande zote ziwe na uvumilivu na kusimamisha vita. Katika taarifa hiyo, kamati hiyo ililaani vitendo vyote vya kijeshi na shughuli zote kwa lengo la kunyakua hatamu za serikali.
Katika siku hiyo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan pia alilaani ushambulizi wa vikosi vya upinzani na kutaka vikosi hivyo vitatue migogoro kwa njia ya amani.
|