Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-14 19:51:40    
Shughuli za "safari ya kilomita elfu kumi ya amani na kirafiki kati ya China na nchi za kiarabu" kuanzishwa mwaka huu

cri

Mwaka huu ni mwaka wa kuadhimisha miaka 50 tangu China na nchi za kiarabu zianzishe uhusiano wa kibalozi, watu mashuhuri kutoka sekta mbalimbali ambao ni pamoja na wanadiplomasia, wsanii, waandishi habari na wanakampuni wameunda msafara wa magari utakaotembelea nchi 20 zikiwemo nchi 17 za kiarabu, ili kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi za kiarabu.

Shughuli hizo ziliandaliwa na shirikisho la urafiki wa watu wa China na shirikisho la urafiki kati ya China na nje na nchi za kiarabu. Kwenye sherehe ya kuanzishwa kwa shughuli hizo, mkurugenzi mkuu wa shirikisho la urafiki wa watu wa China na nje Bwana Chen Haosu alisema:

"Huu ni mwaka wa kuadhimisha miaka 50 ya urafiki kati ya China na nchi za kiarabu. Msafara ulioundwa na watu mashuhuri kutoka idara mbalimbali unaoonesha urafiki wa China na nje utatembelea nchi nyingi za kiarabu, kufikisha urafiki wa watu wa China kwa watu wa nchi za kiarabu na kuwafahamisha watu wa China ustaarabu wa kiarabu. Shughuli hizo hakika zitazidisha urafiki kati ya watu wa China na wa nchi za kiarabu, na kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta za utamaduni, uchumi, biashara na utalii."

Meneja mkuu wa klabu ya magari ya Beijing ambayo pia ni mshiriki wa shughuli hizo Bwana Zhao Xiangjie alifahamisha kuwa, msafara huo ulioundwa na watu 60 na magari 20 utafunga safari mwezi Oktoba mwaka huu kutoka Beijing, wataelekea eneo la magharibi kupita uwanda wa juu wa Pamirs, kuingia nchi za Pakistan, Iran, Kuwait, Saudi Arabia, Bahrain, Qartar, Nchi Falme za Kiarabu, Aman, Yemen, Sudan, Misri, Jordan, Palestina, Syria,Lebanon, Libye, Tunisia, Algeria na Morocco. Safari hiyo itafanyika kwa siku 50. Bw. Zhao Xianmgjie alisema:

"Hizo ni shughuli kubwa kabisa katika miaka 50 iliyopita tangu China na nchi za kiarabu zianzishe uhusiano wa kibalozi. Hii ni mara ya kwanza kwa msafara wa magari wa China kutembelea nchi 17 za kiarabu. Safari hiyo itafuata kihalisi njia ya hariri."

Katika safari hii, wajumbe 60 wa China watashuhudia ustaarabu wa Mto Manjano na ustaarabu wa Mto Nile uliokuwa na historia ya miaka 5000, safari hiyo itakuwa na kilimota zaidi ya elfu 20. msafara huo si kama tu utapita ukuta mkuu, uwanda wa juu wa Pamirs na jangwa la Sahara, bali pia utapita njia ya hariri na sehemu ya chanzo cha dini ya kiislamu.

Mtangazaji maarufu wa kituo kikuu cha televisheni cha China Bwana Chen Duo atakuwa mjumbe wa urafiki wa amani, atashiriki katika shughuli zote za safari hiyo pamoja na waandishi habari wa vyombo vingine vya habari na wajumbe wengine, Bw. Chen Duo aliyepewa cheti cha "Mjumbe wa Urafiki kati ya China na nchi za kiarabu". Alisema:

"Naona fahari kubwa kwa kuchaguliwa kuwa mtume wa urafiki kati ya China na nchi za kiarabu. Naona kuwa, katika dunia hii, watu kutoka nchi tofauti, sehemu tofauti, makabila tofauti na wenye imani tofauti wana matakwa ya aina moja, kwa amani. Amani inahitaji urafiki, na urafiki hauwezi kuwepo bila ya amani. Shughuli hizo ndizo zinalenga kuimarisha mawasiliano kati ya watu wa China na nchi za kiarabu ili kuleta urafiki. Nikiwa mjumbe wa urafiki, nitafanya juhudi chini juu kufanikisha shughuli hizo."

Lengo la shughuli za "safari ya kilomita elfu kumi ya amani na urafiki kati ya China na nchi za kiarabu" ni kuhimiza mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na nchi za kiarabu, kuzidisha maelewano na mshikamano kati ya makabila mbalimbali, na kuzidisha urafiki kati ya watu wa China na nchi za kiarabu. Isitoshe, katika kipindi cha safari hiyo, shughuli mbalimbali za kiutamaduni zitafanyika katika nchi mbalimbali, na kufanya mazungumzo na maonesho ya kibiashara ili kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati wananchi wa nchi mbalimbali. Baadhi ya shughuli muhimu zitakuwa pamoja na sherehe ya ufungaji safari nchini China, utiaji saini kwenye taarifa ya amani ya Piramidi, sherehe ya kukamilishwa kwa safari hiyo, na mkutano wa kwanza wa urafiki kati ya China na nchi za kiarabu unaotazamiwa kufanyika mjini Kartoum kati kati ya mwezi Novemba.

Shughuli hizo pia zimepata uungaji mkono wa serikali ya nchi mbalimbali za kiarabu. Mkuu wa tume ya nchi za kiarabu nchini China, ambaye pia ni balozi wa Aman nchini China Bwana Abdula Zahir Hosni alisema:

"Naona hizo ni shughuli nzuri sana, mabalozi wote wa nchi za kiarabu wanaona kuwa, shughuli hizo zitasaidia kuimarisha uhusiano wa kirafiki kati ya China na nchi za kiarabu. China imefanya juhudi kubwa kwa ajili ya shughuli hizo, naamini kuwa, shughuli hizo zitaleta manufaa ya pamoja kwa pande zote za China na nchi za kiarabu."

Shughuli hizo zimevutia uangalifu mkubwa wa vyombo vya habari vya China na nchi za nje. Kituo kikuu cha televisheni cha China CCTV, Radio China Kimataifa, radio ya serikali kuu ya China na vituo vingine vya televisheni vya miji mikubwa ya China, magazeti na tovuti za Internet za China zitatoa habari kuhusu safari hiyo. Baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za kiarabu kama vile shirika la habari la Misri na kituo cha televisheni cha Al Jazeera pia vitatoa habari kuhusu shughuli hizo.