Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-18 16:14:53    
Mwanzilishi wa sekta ya uzalishaji mali wa teknolojia ya elimu ya viumbe nchini China

cri

Bw. Cheng Jing aliwahi kuwa mtafiti wa kwanza wa kampuni ya teknolojia ya kisayansi ya kisasa ya elimu ya viumbe nchini Marekani, na pia ni mtaalamu aliyebobea katika sekta ya uzalishaji mali wa teknolojia ya elimu ya viumbe duniani. Ili kutimiza lengo lake, kabla ya miaka minane iliyopita, aliacha mshahara mkubwa na mazingira bora, alirejea nchini China kuanzisha kampuni teknolojia ya kiwango cha juu ya elimu ya viumbe, ambayo ilikuwa kampuni ya kwanza ya aina hiyo hapa nchini inayojulikana kwa jina la Viumbe vya Boao. Ingawa aliishi miaka mingi nchi za nje, lakini ofisi ya Bw. Cheng Jing iliyoko Beijing inaonekana yenye umaalumu wa kichina, ambayo imewekwa samani nyingi nzuri za mtindo wa kale wa kichina. Bw. Cheng Jing ni mwembamba, mwenye madaha na elimu kubwa. Mwaka 1988 alikwenda kusoma nchini Uingereza, na alipata digrii ya udakatari ya elimu ya viumbe inayohusika na sekta ya sheria katika chuo kikuu cha Strathclyde, baada ya kuhitimu masomo yake alikuwa mtafiti wa kwanza katika kampuni kadhaa za teknolojia ya kisayansi ya kisasa za Uingereza na Marekani. Ili kuendeleza sekta ya teknolojia ya elimu ya viumbe ya China, aliacha hali nzuri aliyopata na kurejea China kuanzisha shughuli zake mwaka 1999.

"Naona kujiendeleza nchini China pengine nitaingia hasara kifedha, lakini kwa upande mwingine, China ilikuwa na upungufu katika sekta ya taknolojia ya elimu ya viumbe, hivyo nilirudi kushughulikia mambo hayo."

Muda si mrefu baada ya kurejea nchini, aliungwa mkono na chuo kikuu cha Qinghua, ambacho ni chuo maarufu sana nchini china, Bw. Chng Jing alianzisha kituo cha utafiti wa CMOS chip za sekta ya elimu ya viumbe cha kisasa duniani. Hapo baadaye alishauri serikali ya China kuanzisha kituo cha utafiti wa mradi wa CMOS chip cha kitaifa, jambo ambalo lilizingatiwa na viongozi wa China. Kwa kuungwa mkono na serikali ya China kwa fedha na sera, kampuni ya viumbe ya Boao inayozalisha CMOS chip ya elimu ya viumbe ilianzishwa mjini Beijing mwaka 2000, na Bw. Cheng Jing aliteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo.

Mtafiti wa ngazi ya juu wa kampuni ya teknolojia ya viumbe ya Boao Bw. Wang Xianhua alisema, katika kipindi cha mwanzo baada ya kuanzishwa kampuni hiyo, Bw. Cheng Jing aliweka mpango mwafaka na wenye mtazamo wa mbali kuhusu mwelekeo wa maendeleo ya kampuni yaani kuwa na teknolojia muhimu yenye haki-miliki ya kielimu ya kampuni hiyo, na kuifanya kampuni hiyo kuwa kama "maabara" ya teknolojia ya viumbe duniani wala siyo "karakana" ya uzalishaji mali. Bw. Wang Xianhua alisema,

"Nafikiri lengo lake ni wazi, licha ya kutaka Boao kuwa kampuni kubwa ya teknolojia ya viumbe, anaitaka kuwa kampuni ya teknolojia ya viumbe yenye nguvu kubwa ya kujiendeleza, na kwenda sanbamba na kampuni za aina hiyo za nchi za nje."

Hivi sasa kampuni ya teknolojia ya viumbe ya Boao imevumbua na kuzalisha teknolojia na bidhaa za viumbe vya kisasa, na imepiga hatua katika uzalishaji mali kwa kutumia uvumbuzi wake na kuinua kiwango cha uzalishaji mali kuwa cha kimataifa. Bidhaa za CMOS chip za teknolojia ya viumbe zinazalishwa kwenye msingi wa teknolojia ya viumbe ya hataza ya kampuni ya Boao, ambazo zinatumika katika uchujaji wa madawa, zimetumiwa na kampuni nyingi maarufu za madawa duniani zikiwemo za Johson & Johnson, Merck na Pfizer. Mbali na hayo kampuni ya Boao ilihawilisha teknolojia 8 za hataza za kampuni hiyo kwa Marekani, na kuanzisha ubia ambapo kampuni ya teknolojia ya viumbe ya AVIVA Biosciences nchini Marekani ilichukua sehemu ya hisa za kampuni hiyo kwa teknolojia yake. Kutokana na hayo, kampuni ya Boao imekuwa ya kwanza nchini China inayohawilisha teknolojia ya CMOS chip ya viumbe kwa Marekani.

Kutathimini maendeleo ya kampuni hiyo katika miaka 5 iliyopita, Bw. Cheng Jing alisema,

"Boao ilipita njia yenye shida nyingi katika miaka 5 iliyopita toka kuanzisha sekta ya teknolojia ya viumbe ya China hadi kubadilisha mawazo kuwa mali. Hadi hivi sasa, hataza zetu aina zaidi ya 80 zimesajiriwa, na theluthi mbili za hataza hizo zimesajiriwa duniani. Hivi sasa hataza za nchi za nje tulizoidhinishwa ni 10, za nchin ni aina zaidi ya 20. Licha ya hayo, aina za CMOS chips, zana za upimaji, soft ware na mikusanyiko ya data zimezidi 100."

Katika muda mfupi wa miaka 5, pato la kampuni ya Boao kutokana na mauzo liliongezeka kwa mara 3, idadi ya wafanyakazi imeongezeka karibu kufikia 400 ikilinganishwa na watu kadhaa tu katika kipindi cha mwanzoni, wafanyakazi wa kampuni wamekuwa wa aina mbalimbali wakiwemo za watafiti, wauzaji na wasimamizi kutoka hali ya mwanzoni ya kuwa na watafiti peke yake. Miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni ya Boao, wengi walikuwa wanafunzi waliosoma katika nchi za nje, na baadhi yao waliwahi kufanya kazi katika kampuni za nchi za nje, kwa upande mmoja watu hao wana uzoefu wa usimamizi wa kimatiafa, kwa upande mwingine wanafahamu soko na utamaduni wa China.

Zhu Xiaoxiang ni mfano bora kati ya wafanyakazi hao. Yeye ni mwanasayansi aliyesoma katika Marekani, hivi sasa anashughulikia uendelezaji wa mauzo kampuni ya Boao. Alidokeza kuwa hivi sasa kampuni yao inafanya utafiti kuhusu CMOS chip ya teknolojia ya viumbe ya kukagulia madawa, ambayo itatumika katika michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008, wachezaji wanaotaka kupata mafanikio mazuri kwa kutegemea madawa yanayokatazwa, watapatikana katika uchunguzi wa madawa wa CMOS chip ya aina hiyo. Bw. Zhu Xiaoxiang alisema, si kama tu CMOS chip itapunguza sana muda wa uchunguzi wa madawa, bali itapunguza sana gharama. Bw. Zhu Xiaoxiang ana imani kubwa juu ya mustakabali wa utafiti na matumizi ya CMOS chip za aina hiyo. Alisema, "ikiwa kazi zinakwenda vizuri, tutaweza kuzalisha CMOS chip hiyo mwaka 2008, na zitatumika katika uchunguzi wa madawa wa michezo ya Olimpiki. Tunaona tutafanikiwa."

Kuhusu maendeleo ya kampuni ya viumbe ya Boao katika siku za baadaye, Bw. Cheng Jing alisema, lengo la kampuni ni kutia fora katika matumizi ya teknolojia, wingi wa aina za bidhaa na ukuzaji wa masoko nchini China. Alisema, "kuhusu maendeleo ya kampuni katika siku za baadaye, kwanza ni kuelekea kwenye sayansi ya uhai kutoka eneo la CMOS chips za teknolojia ya viumbe, na kukuza shughuli za kampuni. Kwa kipindi cha wastani na kipindi kirefu, ninatarajia kampuni yetu kuzalisha bidhaa kuhusu upimaji wa ugonjwa wa malaria, usalama wa chakula na utafiti wa kisayansi, na hatimaye kuelekea kwenye upande wa tiba za magonjwa."

Licha ya kushughulikia utafiti wa kisayansi na usimamizi wa kampuni, Bw. Cheng Jing ni profesa wa chuo kikuu cha Qinghua, na ameandaa wanafunzi wengi bora, ambao zaidi ya nusu yao walikwenda kusoma zaidi katika vyuo vikuu maarufu nchini Marekani. Bw. Cheng Jing alisema, China ina upungufu mkubwa wa wataalamu wa teknolojia ya viumbe, baada ya wanafunzi hao kuhitimu masomo na kurejea nchini, watakuwa nguvu muhimu ya kuchangia maendeleo ya sekta ya teknolojia ya viumbe nchini China.

Idhaa ya kiswahili 2006-04-18