Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-18 20:13:14    
Maonesho ya nguo ya majira ya Spring ya China

cri

Sekta ya nguo ya China imepata maendeleo ya haraka katika miaka ya karibuni, bidhaa nyingi za nguo za China zinapendwa na watu wengi wa nchini na nchi za nje. Lakini pengine hufahamu kwamba kila mwaka katika majira ya Spring sekta uzalishaji vitambaa na ushonaji wa nguo ya China hufanya maonesha kadhaa ya nyuzi za pamba, vitambaa na nguo hapa Beijing. Ikiwa unataka kununua vitu hivyo, maonesho hayo yatakupatia habari nyingi ili uweze kuchagua vizuri bidhaa unazozitaka.

Tarehe 26 mwezi Mach, maonesho ya kimataifa ya nguo ya mwaka 2006 yalifunguliwa hapa Beijing, maonesho hayo yanachukuliwa kuwa ni mwelekeo wa mabadiliko ya soko la nguo nchini China, na yanaanzisha mfululizo wa maonesho ya nguo katika majira ya Spring. Katika muda wa wiki moja nzima, wasichana wazuri walioonesha mavazi kwenye jukwa la maonesho wakipiga hatua za maringo walivalia mavazi ya mtindo mpya kabisa yaliyosanifiwa na wataalamu wa nguo wa nchini na wa nchi za nje, kutokana na maonesho hayo, watu wanaweza kujua mavazi yatakayopendwa na watu katika miaka miwili ya karibuni. Mavazi mengi ya kike yaliyooneshwa yalikuwa ya rangi nyekundu, pinki, na za rangi za machungwa na dhahabu, ambayo licha ya kuonesha uzuri na madaha ya wanawake, yanaonesha uzuri wahali ya juu ya wanawake; mavazi ya kiume yenye rangi ya kuvutia yatapendwa sana na watu, rangi ya dhahabu, ya rangi ya peach na ya machungwa yatapendwa na watu katika majira ya siku za joto, na kufanya watu wanaowanaovaa nguo hizo kuona raha na starehe. Aina zaidi ya 100 za nguo za kiume zenye nembo ya "msonobari mwekundu" zilioneshwa kwenye maonesho. Msanifu wa nguo hizo bibi Zhao alipoeleza ummalumu wa nguo zake alisema,

"Kila nguo niliyosanifu ilishonwa kwa vitu vya aina mbalimbali, kwa mfano nguo moja inashonwa kwa kitambaa chembamba na ngozi ya mnyama kwa pamoja, au inashondwa kwa kitambaa cha pamba na kitamba cha kitani kwa pamoja, pia kuna nguo inayoshonwa kwa kitambaa cha hariri na kitambaa cha pamba, ili kupata matokeo ya aina mbalimbali tofauti. Nguo niliyosanifu safari hii, ya watu wanayovaa katika mapumziko ilishonwa kwa ufundi wa ushonaji wa suti, na suti niliyosanifu ilielekezwa na wazo la starehe. Ninatarajia katika siku za baadaye wanaume wasivae nguo za aina zile zile walizovaa siku nyingi, bali ni zenye mabadiliko mengi."

Ikiwa tunasema wiki ya maonesho ya mavazi ya kimataifa ni yenye lengo la kufahamisha watu mwelekeo wa mabadiliko ya mavazi katika siku za baadaye, basi maonesho ya kimataifa ya mapambo ya nguo yaliyofanyika sambamba na maonesho ya mavazi, yanawafurahisha watu zaidi. Maonesho hayo ya mwaka huu yaliyokusanya nguo zenye nembo za aina zaidi ya elfu moja za nchi na sehemu 18 duniani, yalipamba moto, kiasi cha kushangaza watu. Mfanya-biashara mmoja wa nchi ya kigeni aliyefika Chna kununua bidhaa za nguo alisema, kweli hapa mtu ataona umaalumu wa aina nyingi za nguo na bei nafuu.

Msaidizi maalumu wa meneja mkuu wa kampuni ya Oudifen nchini China, ambayo inajulikana sana hapa nchini kwa utengenezaji wa nguo ndogo za kuvaliwa ndani, bibi Chen Shuyuan alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa nguo za kuvaliwa ndani za kampuni yao zilizooneshwa kwenye maonesho ya kimatiafa zimezidi aina elfu moja, na aina nyingi za nguo hizo zinapendwa sana na watu wa China na wa nchi za nje.

"Sidiria za kampuni yetu zina uwezo wa miali isiyoonekana ya infrared, na inaweza kufanya damu iende haraka zaidi ndani ya mishipa mwilini. Tena taswira zilizotariziwa juu yake ni za kuona kutoka pande zote mbili za sidiria, ambayo rangi yake ni ya dhahabu na majani ni ya rangi ya kahawia, taswira hizo zinaonesha majami ya miti, sidiria zinatengenezwa kwa ustadi mkubwa, kuonekana kuwa ya hali ya juu, na kuongeza kivutio cha wanawake. Sidiria hizo zinauzwa haraka, hata zinaisha haraka kabla ya mkupuo mwingine wa sidiria kuletwa kwetu."

Katika miaka ya karibuni, maonesho ya nguo ya Beijing ya majira ya Spring, yanavutia wafanya-biashara wengi wa kigeni. Bw. Salge Martin kutoka kampuni maarufu ya nguo ya Novalin ya Ufaransa alisema, kampuni yao kila mwaka inashiriki maonesho ya nguo ya China, ambapo inafanya maingiliano na ushirikiano na watu wa sekta hiyo ya China. Alisema, "Hii ni fursa nzuri ya maingiliano na wenzetu wa China."

Idhaa ya Kiswahili 2006-04-18