Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-19 20:20:01    
Mapishi ya vipande vya nyama ya kuku pamoja na limau

cri

Mahitaji: Nyama ya paja la kuku gramu 1000, yai moja, unga kikombe kimoja, malimau mawili, mvinyo wa kupikia kijiko moja, chumvi vijiko viwili, mafuta ya ufuta nusu ya kijiko, pilipili manga nyeusi, juisi ya limao kijiko moja.

Njia :

1. ondoa ganda la limau na uikata iwe vipande.

2. osha nyama ya paja la kuku, kata iwe vipande vidogo, tia mvinyo wa kupikia, chumvi, mafuta ya ufuta, pilipili manga nyeusi, korogakoroga. Koroga yai pamoja na wanga.

3. tia mafuta ya vikombe vitatu kwenye sufuria, kuchovya vipande vya nyama ya kuku katika yai lililokorogwa pamoja na wanga, halafu uiweke kwenye sufuria, vikaange, mpaka yawe rangi ya hudhurungi, vipakue.

4. pasha moto tena, tia vipande vya nyama ya kuku na vipande vya limau, korogakoroga. Vipakue, mpaka hapo kitoweo hicho kiko tayari kuliwa.

Idhaa ya Kiswahili 2006-04-19