Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-20 20:13:44    
Kutatua suala la nyuklia la Iran kwa njia ya kidiplomasia kunanufaisha pande zote mbili, Marekani na Iran

cri

Baada ya mkutano wa nchi tano wanachama za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi ya Ujerumani kufanyika tarehe 18 huko Moscow kuhusu suala la nyuklia la Iran, siku ya pili wajumbe wa "kundi la nchi nane" pia walijadili suala hilo kwa kutumia muda wa mapumziko katika siku za mkutano wao wa kuandaa mkutano wa viongozi wa kundi hilo utakaofanyika Julai huko Saint Petersburg, lakini haukupata matokeo yoyote.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwenyekiti wa Baraza la Usalama iliyopitishwa tarehe 29 mwezi uliopita, inasema hivi sasa zimebaki siku kumi tu kabla ya mratibu mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki Duniani kuwasilisha ripoti yake kuhusu suala la nyuklia la Iran kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mazungumzo katika jumuiyia ya kimataifa yanakuwa mengi siku hadi siku kuhusu njia gani zitakazotumika kutatua suala la nyuklia la Iran. Hivi sasa ingawa uwezekano wa kutatua suala hilo kwa njia ya kidiplomasia bado upo lakini unakumbwa na changamoto kubwa.

Iran na Marekani, ni nchi muhimu zinazohusika na suala la nyuklia la Iran, lakini mpaka sasa kila moja haitaki kurudi nyuma. Baada ya taarifa ya mwenyekiti wa Baraza la Usalama kupitishwa, badala ya kurudi nyuma, Iran ilifanya luteka kwa kuonesha silaha zake za kisasa. Zaidi ya hayo tarehe 11 mwezi huu Iran ilitangaza kuwa imefanikiwa kupata uranium safi na kusema kwamba itakuwa nchi mwanachama wa "klabu ya kimataifa ya teknolojia ya nyuklia". Lakini je, mbele ya mpinzani wake mwenye nguvu mbona Iran ina msimamo mkali kama hivi? Wachambuzi wanaona kuwa kweli Iran ina kinga zake dhidi ya Marekani: Kwanza, mafuta ya Iran yanaathiri sana soko la mafuta duniani. Kwa makadirio ya Kampuni ya Mafuta ya Rand ya Marekani, iwapo Iran itapunguza mafuta kwa mapipa lakini tano kwa siku, bei ya mafuta itapanda hadi dola za Kimarekani 100 kwa pipa. Luteka iliyofanywa hivi karibuni ilidhihirisha kuwa Iran itasimamisha huduma zake za mafuta kiasi cha 20% duniani katika Ghuba ya Uajemi. Pili, Iran ina athari kubwa kwa siasa ya madhehebu ya Shiya, na ina uhusiano wa karibu na vyama vya Hamas na Jihad, ushirikiano wa vyama hivyo na Iran utakuwa tishio kubwa kwa Marekani na Israel.

Kadhalika, wachambuzi pia wanaona kuwa kinga hizo za Iran pia zinaweza kujiathiri. Kutokana na suala la nyuklia, wawekezaji wa nchi za nje wameikimbia Iran, ukata wa fedha umesababisha uchumi wa Iran kudorora. Mfumuko wa bei na ukosefu mkubwa wa ajira umeleta malalamiko mengi kutoka kwa wananchi. Ingawa Iran ni nchi inayozalisha mafuta kwa wingi lakini haina uwezo wa kusafisha mafuta, petroli inayotumika nchini humo inategemea nchi za nje kwa pesa za kigeni, kama nchi hiyo ikiwekewa vikwazo, uchumi wake utakumbwa na matatizo makubwa.

Ingawa kwa mdomo Marekani imesema itatatua suala la nyuklia la Iran kwa njia ya kidiplomasia, lakini kutumia nguvu za kijeshi pia inawezekana. Marekani inaona kuwa Iran ni nchi ya hatari sana. "Ripoti kuhusu Usalama wa Taifa" iliyotolewa na Marekani mwaka huu imesema, "Iran ni nchi pekee inayoiletea Marekani changamoto kubwa". Bila shaka Marekani ina nguvu za kutosha kuituliza Iran, lakini kutokana na ubabe wake duniani Marekani imesambaza askari wake huku na huko, kwamba nchini Iraq tu wako askari laki 1.35. Idadi ya watu wa Iran ni mara tatu kuliko Iraq, na ukubwa wa Iran kwa eneo ni mara nne kuliko Iraq. Kwa hiyo Marekani ikianzisha vita dhidi ya Iran matokeo yake yatakuwa mabaya zaidi, na pia "gharama" zake zitakuwa kubwa.

Kwa ujumla, mgongano kati ya Iran na Marekani ukiendelea bila kuweza kutatuliwa, hasara hazitakuwa tu kwa nchi hizo mbili, bali jumuyia nzima ya kimataifa. Ndio kwa sababu hiyo, Russia, China na nchi nyingine nyingi zinashikilia kutatua suala la nyuklia la Iran kwa njia ya mazungumzo.

Idhaa ya kiswahili 2006-04-20