Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-24 14:44:20    
Hoteli dogo za kitibet mjini Lahsa

cri

Mji wa Lahsa ulioko kwenye sehemu yenye mwinuko wa mita 3600 kutoka usawa wa bahari, mbali na anga la buluu, na Mto Lahsa wenye maji safi pamoja na mahekalu ya walama ya rangi nyekundu na nyeupe, pia kuna hoteli ndogondogo za kitibet zilizotapakaa mjini Lahsa ambazo zinawavutia watalii wengi. Watalii wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani huwa wanakusanyika katika hoteli hizo ndogo bila kujali hali duni ya makazi hayo, wakijistarehesha katika hali ya raha.

Lahsa, mji mkuu wa Tibet ni mji unaojaa mwangaza wa jua, kwani mkoa wa Tibet uko kwenye uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet nchini China. Siku moja baada ya kula chakula cha adhuhuri, mwandishi wetu wa habari alipita katika hekalu maarufu la Dazhao la dini ya kibudha akielekea Barabara ya mashariki ya Beijing, ambayo ni barabara yenye maduka mengi mjini Lahsa, barabara hiyo inakaribia zaidi na Hekalu la Dazhao, hivyo kwenye barabara hiyo huwa na watalii na waumini wa dini wanaopitapita. Hoteli ya Balangxue iko kwenye barabara hiyo.

Kama hoteli nyingine ndogo za kitibet mjini Lahsa zililvyo, mlango wa Hoteli ya Balangxue si mkubwa na ambao hauonekani wazi jinsi kama unavyojisitiri miongoni mwa maduka mengi yaliyopambwa kwa mapambo ya rangi mbalimbali. Lakini kwenye mlango huo kuna chapa moja ya jina la hoteli iliyoandikwa kwa maandishi ya lugha za kichina, kitibet na kiingereza, hivyo watalii wanaweza kuiona.

Mwandishi wetu wa habari alipoingia katika hoteli hiyo, alimkuta msichana mmoja aliyebeba begi mabegani kama mtalii wa kawaida alivyo. Msichana huyo alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa jina lake ni Li Biqian, anatoka mkoani Guangdong, kusini mwa China, anapenda sana kutalii na kila mara anabeba begi lake mabegani kwenda sehemu mbalimbali kutalii. Kabla ya kufika Tibet, alitafuta habari kutoka kwenye mtandao wa internet kuhusu utalii wa Tibet, akapata habari kuhusu Hoteli hiyo. Alimwambia mwandishi wetu wa habari akisema:

"Nilisoma habari za kuwafahamisha watu kuhusu hoteli hiyo kwenye baadhi ya tovuti za utalii, zikisema kuwa gharama ya utalii kwenye hoteli hiyo ni nafuu, hoteli hiyo ina mandhari nzuri, hususan jengo la kitibet, ambalo linanivutia sana, hivyo nimefika hapa, naona hapa ni mahali pazuri kwelikweli."

Hivi sasa hoteli ndogo za mtindo wa kitibet kama ya Balangxue, zinapendwa sana na watalii wanatembea bila kushiriki matembezi yanayoongozwa na watu wa mashirika ya utalii. Hoteli hizo ndogo na rahisi za kitebet zinafanana na hoteli za vijana zinazowahudumia hasa watalii vijana. Huko utaweza kuburudika na chai ya samli, vilevile unaweza kupata kahawa halisi ya Ireland. Pengine ustawi wa hoteli hizo za kitibet mjini Lhasa ni kutokana na mseto wa jadi za kichina na ya nchi za magharibi, hoteli hizo ndogo zinapendwa na watalii kama hoteli zile kubwa za kifahari.

Hivi sasa mjini Lhasa kuna hoteli ndogo za kitibet zaidi ya 10, na moja ya hoteli hizo zenye sifa nzuri ni hoteli ya Balangxue. Hoteli ya Balangxue ni ya hoteli ya kwanza ya kitibet iliyojengwa mjini Lhasa, hivi sasa hata baadhi ya watu wa mbali wanaijua. Hii ni hoteli pekee nchini China iliyothibitishwa kuwa ni moja ya hoteli kumi nzuri duniani zilizojengwa sehemu ya milimani, ambazo ni hoteli za bei nafuu za kupokea wageni sehemu za milimani.

Ingawa hoteli hizo ni za gharama ndogo, lakini kivutio cha hoteli ya Balangxue siyo tu bei yake ni nafuu. Endapo utakaa huko, utajua uzuri wake maalumu.

Ndani ya ua wa hoteli ya Balangxue kuna ubao mmoja ulibandikwa vijikaratasi vyenye ujumbe wa aina mbalimbali zikiwemo habari kuhusu kukodi teksi, kuuza mabegi na vifaa vingine vya utalii na kutafuta wenzi wa safari. Msichana Zhong Yinxin kutoka Hongkong aliweka ujumbe kwenye ubao huo siku chache zilizopita, akitarajia kupata watu wanaosafiri pamoja naye katika matembezi. Alisema:

"Kamwe sitaki kufanya matembezi yanayoongozwa na watu wa mashirika ya utalii, sitakuwa na uhuru nikishiriki safari inayoongozwa na watu wa shirika la utalii, tena kuna matata mengi, nitakuwa sina budi kuongozwa nao hatua kwa hatua. Nimebandika ujumbe wangu kwenye ubao, ninataka kupata watu wengine wawili katika safari."

Msichana Zhong Yinxin alimwanbia mwandishi wetu kwa furaha, watu wengi wamewasiliana naye baada ya kusoma ujumbe wake. Hatimaye aliamua kusafiri pamoja na wasichana wawili waliotoka mji wa Xhenzhen. Katika Balangxue, habari zinaenezwa kwa njia ya kizamani lakini ni njia inayofaa.

Balangxue pia ni sehemu nzuri ya maingiliano ya watu. Katika nasafi ile ndogo, ni rahisi kwa watu kukaa pamoja kwa mapatano. Baada ya watu waliotoka sehemu mbalimbali duniani kukaa huko, wanapeana salamu na kueleza habari kuhusu uchovu na furaha walizopata katika safari zao; watu hao wanantoka katika mazingira ya utamaduni tofauti, katika nafasi hiyo ndogo wanakutana na kuingiliana, ni dhahiri kuwa maingiliano ya utamaduni wao ni ya hali ya kawaida kabisa na ya kuvutia.

Katikati ya ua wa hoteli ya Balangxue kuna bustani moja ndogo iliyozungushiwa vyuma. Katika upande wa magharibi ya bustani hiyo ndogo kuna sehemu ya kunywea chai, ambapo meza kadhaa ndogo zimekwekwa chini ya miavuli yenye rangi za aina mbalimbali. Wageni wanaweza kula chakula, kunywa chai, kusoma vitabu na kupiga soga kwenye meza hizo.

Bw. Zhang Shukai aliyetoka Sichuan alisema, viti vyote kwenye sehemu hiyo huenea watu. Alisema:

"Watu waliokuwa huko wote ni watalii wa kujitembeza waliotoka sehemu mbalimbali nchini na nchi za nje. Kila siku sehemu hiyo kuna watu wengi, wakati mwingine ni zaidi ya 10 au 20, watu wengi wanakaa kwenye viti wakiduwaa, hali ya namna hii ni ya kupendeza sana. Pengine unaona ajabu, kwanini wote wanakaa huko wakiduwaa. Huko unaweza kufahamiana na watu wengi. Kila mwaka ninakwenda huko kukaa siku kadhaa, ninapenda hali hiyo na kutaka kupumzika na kutulia kabisa."

Bw. Zhang Shukai alimwambia mwandishi wa habari kuwa hapo awali kabisa alifika Lhasa akitarajia kuwa na maono ya ujasiri na kusisimua. Lakini baada ya kufika Balangxue na kuwa mmoja wa watalii wanaojitembeza, alifahamu vizuri mtindo wa maisha ya amani, kitu ambacho kilimfanya kuipenda Balangxue na kupenda Lhasa.

Idhaa ya kiswahili 2006-04-24