Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-24 15:48:28    
Uenezi wa televisheni waingia katika kipindi cha maendeleo ya haraka nchini China

cri

Ukiuliza chombo gani cha habari kina athari kubwa zaidi nchini China hivi sasa? Hakika utaambiwa: Televisheni! Ingawa televisheni ilitokea nchini China miaka 30 tu iliyopita, lakini hivi sasa imeingia katika kipindi cha uenezi wa haraka. Hivi sasa nchini China kumekuwa na seti za televisheni milioni 400 na watazamaji wamefikia bilioni 1.2.

Kipindi hiki cha habari kilichotangazwa na Kituo Kikuu cha Televisheni cha China CCTV kimekuwa miaka mingi na kinavutia zaidi kuliko vipindi vingine. Kituo Kikuu cha Televisheni cha China kilianzishwa mwaka 1958, hivi sasa kinatangaza vipindi vya habari, uchumi, muziki na opera, michezo, filamu, elimu kwa watoto, mambo ya kijeshi, sayansi na teknolojia na kilimo, na pia kinatangaza kwa Kiingereza, Kifaransa na Kihispania.

Ingawa kituo hicho kina vipindi vingi, lakini watu wanapofungua televisheni pengine hawachagui vipindi vya kituo hicho, kwani katika miaka 20 ya karibuni, vituo vya televisheni vimeanzishwa vingi na kufikia zaidi ya 400 nchini China licha ya vituo vya wilaya.

Watu wanaofaidika zaidi na matangazo ya televisheni ni wakulima ambao wamefikia milioni 900. Mkulima Wang Pengyan wa wilaya ya Changzhi mkoani Shanxi alisema, "Zamani, tulipata idhaa mbili tu na picha zilikuwa sio safi. Lakini sasa, tunaweza kupata idhaa zaidi ya 40 na picha ni safi. Televisheni imekuwa sehemu yetu muhimu katika maisha yetu."

Kama mkulima Wang Pengyan alivyokuwa zamani, wakulima wanaoishi katika maeneo ya mbali vijijini nchini China pia wahakuweza kupata habari za nje kutokana na mawasiliano mabaya. Lakini miaka ya karibuni wamezibua kutokana na kupatiwa matangazo ya televisheni.

Msemaji wa Idara Kuu ya Redio, Filamu na Televisheni ya China Bw. Zhu Hong alisema, mradi wa uenezi wa matangazo ya televisheni umepata maendeleo ya haraka hadi kufikia maeneo mengi vijijini, tofauti ya kupata matangazo ya televisheni kati ya vijiji na miji imepungua sana. Alisema, "Tangu mwaka 1998 tulipoanzisha mradi wa uenezi wa matangazo ya televisheni, wakulima milioni 97 wameweza kupata matangazo hayo. Mpango utakaotekelezwa ni kuvipatia vijiji vyote vyenye familia kuanzia ishirini na kuendelea kwa kila kijiji matangazo ya televisheni. Ili kuhakikisha mpango huo unatekelezwa bila tatizo serikali itatenga fedha yuan bilioni kumi kadhaa. Mwaka 1997 asilimia 87 ya maeneo ya China yamepata matangazo hayo, hadi mwaka 2005 maeneo hayo yamefikia asilimia 97. Uenezi wa matangazo ya televisheni umeingia katika kipindi cha haraka."

Kutokana na uenezi huo watazamaji wanafaidika sana kielimu na kiuchumi. Vituo vingi vimeanzishwa katika ushindani wa matangazo ya televisheni kwa kutangaza vipindi vinavyohusika moja kwa moja na masoko na burudani za kuwavutia watazamaji. Kati ya vituo hivyo kituo cha mkoa wa Hunan kimefanikiwa zaidi, ambacho kinatangaza michezo mingi ya burudani inayowavutia watazamaji wa mkoani.

Prof. Bi. You Jie wa Chuo cha Televisheni katika Chuo Kikuu cha Uenezi wa Habari cha China alisema, "Vipindi vya televisheni vya kituo cha televisheni cha Mkoa wa Hunan vinaweza kuridhisha watazamaji wake kwa upendo wao."

Katika matangazo ya televisheni, pia kuna filamu nyingi za televisheni za nchi za nje. Filamu za televisheni za Korea ya Kusini zimekuwa zinapendwa sana na wanawake wa mijini, ukifungua televisheni hakika utaweza kupata filamu za Korea ya Kusini katika idhaa fulani.

Matangazo ya televisheni yanapokuwa wazi kwa nchi za nje, filamu za televisheni za China pia zinanunuliwa na kutangazwa katika nchi za ng'ambo, hasa filamu zinazoeleza historia ya kale ya China. Kwa mujibu wa takwimu, mwaka jana filamu za televisheni ya China zilizouzwa katika nchi za nje zilifikia yuan milioni mia moja.

Idhaa ya kiswahili 2006-04-24