Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-25 16:29:41    
Wanauchumi wa China na wa nchi za nje waisifu hali ya uchumi wa China

cri

Wataalamu wa uchumi wa China na wa nchi za nje wanaohudhuria mkutano wa mwaka wa 2006 wa Baraza la Asia la Boao wanaona kuwa, ongezeko la asilimia 10.2 la uchumi wa China katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu ni hali ya kawaida, na hali ya uchumi wa China kwa jumla ni ya kufurahisha.

Takwimu za mwanzo zilizotolewa tarehe 20 na idara ya takwimu ya taifa ya China zimeonesha kuwa, thamani ya uzalishaji nchini China katika miezi mitatu ya kwanza iliongezeka kwa asilimia 10.2 kutliko mwaka jana wakati kama huu, na ongezeko hilo ni kubwa kidogo kuliko ongezeko la mwaka jana ambalo lilikuwa asilimia 9.9.

Mkuu wa zamani wa idara ya takwimu ya taifa ya China Bw. Li Deshui alisema, ongezeko hilo kubwa la uchumi wa China linahusiana na maendeleo mazuri ya uchumi duniani.

Habari zinasema kuwa, hivi karibuni Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeongeza matarajio kuhusu maendeleo ya uchumi ya umoja wa uchumi ulio muhimu zaidi duniani.

Bw. Li Deshui alisema, mwaka huu thamani ya uwezekaji wa mali zisizohamishika na thamani ya mauzo ya rejareja ya bidhaa zote zinaongezeka kwa haraka. Mauzo ya bidhaa katika nchi za nje yanaendelea kuongezeka, na mikwaruzano ya kibiashara haina athari kubwa kwenye mauzo ya bidhaa ya China katika nchi za nje. "Mambo hayo matatu yamesukuma mbele ongezeko la uchumi wa China katika miezi mitatu ya kwanza." Bw. Li alisema.

Kutokana na takwimu zilizotolewa na idara ya takwimu ya China, katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya uwekezaji wa mali zisizohamishika nchini China iliongezeka kwa asilimia 27.7 kuliko mwaka jana wakati kama huu; thamani ya mauzo ya rejareja ya bidhaa iliongezeka kwa asilimia 12.2; na thamani ya mauzo ya bidhaa katika nchi za nje iliongezeka kwa asilimia 25.8. Mtaalamu wa uchumi wa Kampuni ya Morgan Stanley Bwana Stephen Roach alisema, ongezeko la asilimia 10.2 ni hali ya kawaida hivi sasa, na haina haja ya kuchukua hatua ya dharua ili kuidhibiti.

Bw. Roach alisema, umoja wa uchumi ulio muhimu zaidi duniani umetilia maanani ongezeko kubwa la uchumi la kupita kiasi. Hivi karibuni Benki kuu za Marekani, Umoja wa Ulaya na Japan zilijadili kuchukua hatua kudhibiti mfumuko wa bei kwa mara ya kwanza katika miaka 15 iliyopita. Ongezeko la uchumi duniani litapungua kutokana na jambo hilo, na inakadiria kuwa, ongezeko la uchumi wa China ambao ni sehemu moja ya uchumi wa dunia pia litapungua.

Bw. Li Deshui alisema, hatuwezi kusema kuwa ongezeko la uchumi wa China ni la kupita kiasi kutokana na ongezeko kubwa katika miezi mitatu ya kwanza. Lakini amekiri kuwa, katika sekta kadhaa miradi mipya ni mingi na mikubwa, na mikopo iliyotolewa na benki za biashara ni mikubwa.

Mpango wa 11 wa maendeleo ya miaka mitano wa China umeweka lengo kuwa uchumi wa China utaongezeka kwa asilimia 7.5 kila mwaka kati ya mwaka 2006 hadi mwaka 2010. Ongezeko hilo ni dogo zaidi kuliko ongezeko la miaka 25 iliyopita ambalo ni asilimia 9.5. Pia unasema kuwa masoko ya nchini yatakuwa nguvu muhimu ya kusukuma mbele ongezeko la uchumi wa China.

Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya kemikali maalum ya Degussa nchini China Bw. Eric Baden alisema, ingawa ongezeko kubwa la uchumi wa china katika miezi mitatu ya kwanza mwaka huu, lakini hali ya uchumi wa China kwa ujumla ni ya kufurahisha. Alisema hatua za usimamizi wa ujumla zilizochukuliwa na serikali ya China zimepata maendeleo makubwa. Juhudi za China katika kurekebisha miundo ya uchumi na kugeuza njia ya ongezeko la uchumi zimemfanya awe na imani kubwa kuhusu maendeleo ya uchumi wa China katika muda mrefu ujao.

Bw. Roach alisema, maendeleo ya masoko ya China huenda yatakuwa na fursa kubwa zaidi kwa uchumi wa dunia katika karne ya 21.

Idhaa ya Kiswahili 2006-04-25