Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-25 20:53:08    
Barua 0425

cri

Msikilizaji wetu Mussa Emmanuel Duttu wa Kahama SDA Church, Sanduku la barua 56 Kahama, Shinyanga, Tanzania amesema katika barua yake kuwa anashukuru kusikia kuwa kituo cha FM kilichojengwa Nairobi kimezinduliwa, na kuongezwa muda wa matangazo ya Idhaa ya Kiswahili, pamoja na kuwezesha matangazo yenu kurushwa kupitia Radio yetu ya taifa, Radio Tanzania Dar-es-Salaam na sauti ya Tanzania Zanzibar. Kweli CRI imeamua kazi, anasema amewakubali. Na yeye anatuambia kuwa, ataendelea kusikiliza CRI daima siku zote.

Anasema amekuwa msikilizaji wetu kwa muda mrefu sasa nashukuru kwa ushirikiano mkubwa tunaouonesha kwake. Ana watu wapatao wanne wamekuwa wasikilizaji pamoja naye katika matangazo ya CRI, wanaomba kujiunga nami katika CRI hajui tunasemaje?

Anaomba tumjibu, halafu anaomba ikiwezekana tumtumie picha za watu wanaofanya kazi katika CRI ili awaonenye angalau katika picha.

Tunawakaribisha kuwa wasikilizaji wa Radio China kimataifa na ni matumaini yetu kuwa watasikililza matangazo yetu na kutoa maoni na mapendekezo yao ili kutusaidia kuboresha vipindi vyetu. Kuhusu matangazo ya CRI kupitia Radio Tanzania Dar es Salaam na Sauti ya Zanzibar Tanzania bado tunajitahidi kutimiza lengo, kazi zinazohusika ni za aina mbalimbali, siyo rahisi kutimiza lengo, lakini tutaendelea na juhudi zetu ili kuwawezesha wasikilizaji wetu wengi wapate usikivu mzuri.

Anasema anapenda kutujulisha kuwa, atafunga ndoa, hivyo anapenda kutufahamisha tukiwa sehemu ya jamaa zake sisi wa CRI na kulingana na uanachama wake wa CRI, ndoa yake itafungwa mnamo mwezi wa saba mwaka huu, tarehe bado haijapangwa hivyo anatukaribisha tushiriki sherehe yake ya arusi .

Mwisho hongera sana kwa mkuu mpya wa CRI Bwana Wang Gengnian kwa jinsi anavyochapa kazi katika Radio China Kimataifa.

Tunamshukuru sana kutualika kwenye sherehe yake ya kufunga ndoa, kama ikiwezekana, wakati atakapofunga ndoa tutakuwepo nchini Tanzaia, tutafurahi kushiriki sherehe yake, hapa tunampa hongera kabla ya wakati, ni matumaini yetu kuwa bibi arusi na bwana arusi watapendana daima na kuishi maisha mazuri.

Msikilizaji wetu Okongo Okeya P.O.BOX 381 Iganga Uganda anasema katika barua yake kuwa, Radio China Kimataifa ewe ni mwanga na tumaini ya wasikilizaji katika sifa nyingi zaidi. Yeye mwenyewe tangu alipoanza kuisikiliza Redio China Kimataifa alifaidika kwa usikilizi mzuri na ataisikiliza kwa maisha yake yote Redio China Kimataifa heko na hongera sana Mungu awabariki ufanisi, ustawi, maendeleo, mabadiliko na mageuzo ya historia ni katika mahitaji ya kimsingi ya maisha ya wanadamu wote ulimwenguni. Na misingi hiyo inaongozwa na akili kamilifu inayotoka Beijing Radio China Kimataifa na kote duniani. Mambo mengine yote ya kijamii K.V. kusema kweli kutosema uwongo kuwa mwamminifu, adilifu, uhuru, usawa ya wanadamu wote ni mwanga pekee wa kufika ukweli halisi, Redio China Kimataifa ni daraja la urafiki linaloleta mwanga.

Daraja la Urafiki wa kimatafa udumu daima dawamu ili kushirikisha wasikilizaji wote mahala popote pale walipo ulimwenguni.

Anasema, daraja ni njia moja yenye usawa ya ustawi kwa waheshimiwa ndugu zao wapendwa wananchi wa taifa la China na serikali ya China. Radio China kimataifa ni kama kioo, kwa sababu hata ikiwa mbali kiasi gani tuko pamoja na tunaweza kupata sauti ya watangazaji kwa usaw, Ustawi, Ufanisi na Maendeleo zaidi. Hongera hongera kwa ufanisi mkubwa sana wa Radio China kimataifa.

Tunamshukuru sana msikilizaji wetu huyo wa Uganda Bwana Okongo Okeya kwa barua yake na pongezi lake la kututia moyo kuchapa kazi zaidi kwa ajili ya wasikilizaji wetu.