Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-26 20:49:14    
Mapishi ya kukoroga asparaga pamoja na kamba

cri

Mahitaji

Asparaga gramu 300, kamba gramu 100, pilipili hoho moja, chumvi, sukari, mafuta ya ufuta nusu ya kijiko, mafuta kijiko kimoja, vitunguu saumu viwili

Njia

1. kata vitunguu saumu na pilipili hoho ziwe vipande vidogo. Ondoa gamba la asparaga, uikate iwe vipande. Osha kamba halafu ondoa mstari mweusi wa kamba, uikate iwe vipande viwili.

2. pasha moto weka maji kwenye sufuria, baada ya kuchemka tia vipande vya asparaga, baada ya dakika 2 vipakue halafu uviweke kwenye maji baridi, halafu ikaushe.

3. pasha moto tena, tia vipande vya kamba-mwakaje kwenye maji, mpaka kamba-mwakaje iive, ipakue.

4. koroga vipande vya asparaga, kamba-mwakaje pamoja na vipande vya pilipili hoho, vitunguu saumu, sukari, chumvi, mafuta ya ufuta, mafuta, korogakoroga. Mpaka hapo kitoweo hicho kiko tayari kuliwa.