Tarehe 27 mwezi huu dada wa makamu mpya wa rais wa Iraq Bw. Tarek al-Hashimi aliuawa kwa kupigwa risasi mbele ya nyumba yake mjini Baghdad, na askari wawili wa Italia pamoja na askari mmoja wa Romania waliuawa katika mlipuko uliotokea kusini mwa Iraq. Dalili nyingi zinaonesha kwamba hali ya usalama nchini Iraq bado ni mbaya. Kwa hiyo namna ya kutuliza hali ya vurugu inayozidi kuwa mbaya ni kazi kubwa inayoikabili serikali mpya ya Iraq.
Polisi nchini Iraq ilisema, asubuhi ya tarehe 27 mwezi huu dada wa Tarek al-Hashimi alipoalipokuwa anatoka nyumbani alishambuliwa kwa kupigwa risasi na mtu asiyefahamika ambaye alikuwa ndani ya gari lililopita kasi. Huyo ni jamaa wa pili kuuawa kati ya jamaa wa ukoo wa makamu wa rais Bw. Hashimi. Tarehe 13 mwezi huu ndugu mwingine wa makamu wa rais Bw. Ahmed Bakir al-Hashimi alipigwa risasi na kufa papo hapo wakati akipita kwenye makazi ya watu wa madhehebu ya Shiya, mashariki mwa Baghdad.
Tarehe 27 mwezi huu jemadari mkuu wa Italia alitangaza, mlipuko uliotokea tarehe 27 karibu na makao makuu ya jeshi la Italia nchini Iraq katika mji wa Nasiriyah, kusini mwa Iraq, ulisababisha vifo vya askari wawili wa Italia na askari mmoja wa Romania na askari wengine wawili wa Italia walijeruhiwa vibaya.
Siku hiyo hiyo ya tarehe 27, milipuko mingi ilitokea pembezoni mwa Baghdad na ilisababisha watu wasiopungua sita kupoteza maisha na watu na askari polisi 12 kujeruhiwa. Zaidi ya hayo, polisi nchini Iraq iligundua maiti kumi ambazo zote zilionekana kupigwa risasi kichwani na hakuna alama za kupigwa mwilini.
Tokea tarehe 22 mwezi huu mfuasi wa madhehebu wa Shiya, Bw. Jawad al-Maliki kuwa waziri mkuu, mchakato wa siasa umepiga hatua kubwa ya mbele. Lakini kutokana na hali ya siasa ilivyo sasa hatua hiyo haikusaidia kuboresha hali ya usalama. Kwa mujibu wa takwimu, tokea tarehe 22, katika muda wa siku tano tu watu wakiwa raia na askari polisi wa Iraq 108 wameuawa katika matukio ya nguvu za kisilaha.
Wachambuzi wanaona kwamba hali ya usalama inayozidi kuwa mbaya inahusika na kundi la al-Qaeda. Kiongozi wa tawi la kundi la al-Qaeda nchini Iraq Abu Musab al-Zarqawi tarehe 25 kwenye picha ya video alisema, serikali mpya ya Iraq ni "kibaraka" cha Marekani, akitaka watu wa madhehebu ya Shiya wajumuike na kupambana na serikali mpya, na alishutumu waislamu wa madhehebu ya Shiya walioshiriki katika serikali mpya na kuwaita kuwa ni "maajenti wa Marekani", na alisema kwamba kundi lake litafanya mashambulizi mengi zaidi dhidi ya Iraq. Vyombo vingi vya habari vinasema, kifo cha dada wa makamu wa rais Bw. Hashimi pengine kinahusika na wadhifa wa kaka yake, na Chama cha Waislamu cha Iraq kilichoongozwa na Hashimi kinaona vivyo hivyo. Ofisa mmoja mwandamizi wa chama hicho ambacho ni kikubwa katika madhehebu ya Shiya tarehe 27 alisisitiza kwamba kifo cha dada wa Hashimi hakiwezi kumwondoa Hashimi madarakani na chama chake kutoka serikali mpya.
Kadhalika, wachambuzi wanona kuwa mgongano kati ya madhehebu ya dini pia ni chanzo cha kusababisha matokeo ya umwagaji damu nchini Iraq. Tarehe 22 Februari mwaka huu mgongano uliosababishwa na tukio la kushambulia msikiti wa Ali al-Hadi mpaka sasa unaendelea, madhehebu ya Shiya, Suni na watu wa Kurd kila moja lina jeshi lake, serikali ya Iraq inashindwa kudhibiti hali ya vurugu.
Kwa kifupi, hivi sasa, hali ya usalama haijabadilika kuwa nzuri pamoja na kuundwa kwa serikali mpya, na hali hiyo mbaya ikiendelea hakika itaathari vibaya mchakato wa siasa nchini Iraq. Kwa hiyo kazi ya haraka inayomkabili waziri mkuu wa serikali mpya Bw. Jawad al-Maliki ni kushauriana na madhehebu mbalimbali na kuchagua waziri mkuu mpya anayefaa zaidi na kuunda serikali yenye umoja wa makabila ili kukomesha hali ya usalama inayozidi kuwa mbaya katika mchakato wa siasa nchini Iraq.
Idhaa ya kiswahili 2006-04-28
|