Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-04-28 23:24:29    
Waziri wa utalii wa Kenya azungumzia uhusiano kati ya China na Kenya na ushirikiano wa utalii

cri

Hivi karibuni mwandishi wetu wa habari aliyeko Nairobi Kenya alifanya mahojiano na waziri wa ziara wa Kenya Bw. Moris Dzoro, ambapo Bwana Dzoro alifurahia ziara ya rais Hu Jintao wa China nchini Kenya, alisema, ziara ya rais Hu Jintao wa China nchini Kenya ilimkumbusha Bw. Moris Dzoro ziara yake ya mwaka jana nchini China:

" Nilifurahisha sana kwamba serikali ya China ilituandalia sana, na safari hii serikali ya Kenya na wananchi wameandaa kumwonesha nchi yetu iliyopo na inavyopendeza.

Kama watu wa China walivyonipokea kwa ukarimu, mlango wa Kenya uko wazi kwa wachina, watachukua Kenya kama kwao, Bw. Dzoro alisema.

Kadiri uhusiano wa Kenya na China inavyosonga mbele, watalii wa China wanaotalii Kenya wameongezeka mwaka hadi mwaka. Bw. Dzoro alisema:

Watalii wa China wanaotembelea Kenya wameongezeka sana. Mwaka 2002, wachina waliotembelea Kenya walikuwa 2600, mwaka 2003, idadi hiyo ilikuwa 4800, hadi kufikia mwaka 2004, idadi hiyo iliongezeka kufikia 8600, na mwaka huu idad hiyo inatazamiwa kufikia 11000. Ongezeko hilo linatokana na uhusiano mwema kati ya Kenya na China.

Mapato kutokana na utalii yanachukua asilimia 12 ya jumla ya uzalishaji mali ya Kenya, na watalii kutoka China wanachangia mapato hayo makubwa. Bw. Dzoro alisema: Mapato ya utalii yanachukua asilimia 12 ya mapato ya jumla ya Kenya, mwaka jana pesa za kigeni katika sekta ya utalii zilikuwa bilioni 42, na wachina walichangia sana.

Dzoro alifahamisha kuwa watalii wa China hutembelea Mbuga wa wanyama wa Maasai Mar, ziwa la Nakur, na mji wa Nairobi. Alisema ingekuwa na barabara zuri, watatembelea sehemu nyingi zaidi.

Bw. Dzoro alisema, ili kuwavutia watalii wengi zaidi kutoka China, Kenya imechukua hatua nyingi zikiwemo, kuanzisha tovuti kuhusu habari za utalii za Kenya ambayo ni ya kichina kwenya Internet mwaka jana, na kuwarahisishia wachina utaratibu wa kuomba viza, hivi sasa viza ya Kenya inapatikana kwa wachina siku moja tu baada ya kuiomba. Bw. Dzoro alisema: Kenya imechukua hatua mbalimbali kuwavutia watalii wa China, zikiwemo ujenzi wa barabara, mahoteli na kuchukua hatua za kuhakikisha usalama.

Bw. Dzoro alisema anaamini kuwa ziara hiyo ya Rais Hu Jintao itaongeza urafiki wa China na Kenya, na kuimarisha zaidi ushirikiano ambao tayari upo kati ya nchi hizo mbili, na kwa wakati mmoja, anatumai kwamba China itaongeza uwekezaji katika miundo mbinu ya utalii nchini Kenya na kuongeza miradi ya kupelekeana watu. Bw. Dzoro alisema wachina ni watu wakarimu sana, hivi sasa anapanga kuitembelea China kwa mara nyingine, kwani anaona wachina ni wakarimu na wachangamfu.