Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-01 21:18:25    
Kitivo cha Confucius cha chuo kikuu cha Nairobi

cri

Rais Hu Jintao wa China atafanya ziara ya kiserikali nchini Kenye toka tarehe 27 hadi 29 mwezi Aprili. Katika ziara yake hiyo, rais Hu Jintao atakuwa na mazungumzo na wanafunzi wa kitivo cha Confuxius cha chuo kikuu cha Bairobi. Hivi karibuni, mwandishi wetu wa habari aliyeko Nairobi Bw. Chen Yonghua alikuwa na mahojiano na baadhi ya walimu na wanafunzi wa kitivo hicho. Sasa tunawaletea ripoti aliyoandika kutoka huko.

wasikilizaji wapendwa kama msingeambiwa, msingejua kuwa wimbo huu maarufu wa kichina mnaosikia sasa hivi uliimbwa na wanafunzi wa Afrika, ambao walianza kujifunza ligha ya Kichina kabla ya miezi michache iliyopita. Wanafunzi hao wanatoka kitivo cha Confucius cha chuo kikuu cha Nairobi, ambacho ni kitivo cha kwanza na cha kipekee cha Confucius kilichoanzishwa barani Afrika kutokana na ushirikiano kati ya chuo kikuu cha uwalimu cha Tianjin na chuo kikuu cha Nairobi, kwa hivi sasa kitivo hicho kina wanafunzi 25 wa Afrika. Tangu kufunguliwa masomo yake, wanafunzi hao wamesoma lugha ya kichina kwa miezi minne. Ingawa muda si mrefu, lakini wameweza kusalimiana kwa Kichina bila ya matatizo, tena wameweza kueleza baadhi ya mawazo yao kwa kichina.

Mwanafunzi wa kike Shariffa Begam Noordin ni mwanafunzi wa kitivo cha Confucius cha chuo kikuu cha Nairobi. Alipoeleza sababu ya kuchagua masomo ya lugha ya Kichina, alisema,

"Kwangu sababu ya kuchagua kujifunza lugha ya kichina ni kwanba ninapenda lugha hiyo, napenda utamaduni wa China na watu wa huko, wote hao wanataka kuendeleza urafiki na sisi."

Katika miaka ya karibuni, pamoja na maendeleo makubwa na uendelezaji wa ufunguaji mlango, lugha ya Kichina imekuwa moja ya lugha muhimu duniani. Hivi sasa idadi ya wageni wanaojifunza lugha ya Kichina imezidi milioni 30. Ili kutimiza mahitaji ya watu wa dunia ya kujifunza ligha ya kichina, China imeanzisha taasisi za Confucius zinazolenga kueneza lugha ya kichina na utamaduni wa China. Baada ya taasisi ya Confucius ya kwanza kuanzishwa katika Seoul, mji mkuu wa Korea ya Kusini mwaka 2004, China imeanzisha taasisi za Confcius makumi kadhaa katika mabara ya Amerika, Ulaya na Afrika. Hapo zamani kwa wanafunzi wa Afrika, njia pekee ya kujifunza lugha ya Kichina ilikuwa ni kwenda kuchukua mafunzo nchini China. Lakini hivi sasa, hali imebadilika, kwa uchache kabisa kwa watu wa Kenya.

Hii ni sauti ya mwalimu Sun Jing katika darasa la lugha ya Kichina la chuo kikuu cha Nairobi. Mwalimu Sun Jing alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa wanafunzi wa Kenya wanathamini nafasi hiyo ya kujifunza lugha ya Kichina nchini mwao. Baada ya kuanzishwa kitivo cha Kichina, wanafunzi wengi kulikwenda kujiandikisha, lakini ili kuhakikisha ubora wa mafunzo, katika hali ya hivi sasa ya kutokuwa na waalimu wengi, wanafunzi waliochukuliwa ni wachache sana katika awamu hiyo ya mwanzo.

Ingawa wanafunzi wa Afrika wana shauku kubwa ya kujifunza Kichina, lakini ni changamoto kubwa kwao. Ili kuinua ufanisi wa mafunzo, waalimu wawili wa chuo kikuu walitafuta mbimu nyingi, naibu mkurugenzi wa kitivo hicho bibi Song Lixian alisema,

"Licha ya somo la Kichina, pia tumefungua masomo ya utamaduni wa China. Kwani lugha na utamaduni ni vitu viwili visivyoweza kuachana. Tangu kufungua masomo, tumefanya shughuli nyingi za kuwafahamisha wanafunzi utamaduni wa China."

Mwalimu Song Lixian alisema, katika mwezi Januari, siku chache kabla ya siku kuu ya Spring ya wachina, waalimu walimwomba balozi wa China nchini Kenye BW. Guo Chongli kutoa mhadhara kwa wanafunzi hao, kisha walitengeneza chakula cha "jiaozi" kwa pamoja. Mwezi Februali, waliandaa semina kuhusu filamu za sinema za China na kuwaonyeshea sinema inayojulikana kama "Shujaa". Kwa kuwa waafrika wanapenda penda sana Wushu ya China, wanafunzi waliifurahikia sana sinema hiyo. Mbali na hayo waliandaa maonesho ya uandikaji wa hati za maneno ya Kichina na semina kuhusu michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008. shughuli hizo za kuvutia zimewasogeza wanafunzi hao karibu zaidi na China, ambazo zinafanya kazi muhimu za kuongeza juhudi za wanafunzi za kujifunza Kichina.

Mwalimu Song Lixian alisema, ili kuimarisha maingiliano, kila mwaka chuo kikuu cha uwalimu cha Tianjin kinatoa nafasi za kujifunza Kichina kwa wanafunzi 10 bora wa chuo kikuu cha Nairobi, licha ya hayo, ofisi ya uongozi wa mafunzo ya lugha ya Kichina ya baraza la serikali kwa wanafunzi wa nchi za nje, inatoa nafasi ya kusoma nchini China kwa wanafunzi wa nchi za kigeni. Hatua hizo ni nguvu kubwa inayoongeza juhudi za wanafunzi wa kitivo cha Confcius cha chuo kikuu cha Nairobi.

Mwalimu Song Lixian alisema, kwa kuwa hivi sasa kuna watu wengi wa Kenya wanaotaka kujifunza lugha ya Kichina, hivyo wameweka mpango wa kuongeza madarasa ya lugha ya Kichina hadi mawili au matatu ili kukidikisha wanafunzi wanaotoka nchi nyingine za bara la Afrika katika siku za baadaye.