Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-02 18:57:56    
Wahamiaji milioni moja nchini Marekani wafanya mgomo mkubwa

cri

Wahamiaji kutoka nchi za nje wanaoishi katika sehemu mbalimbali nchini Marekani tarehe 1 Mei walifanya maandamano na mgomo wa kazi, wakidai serikali ya Marekani ibadilishe sera ya wahamiaji na kulinda haki na maslahi halali ya wahamiaji.

Siku hiyo maandamano makubwa yalifanyika katika miji zaidi ya 50 ikiwemo New York, Chigaco, Los Angels na Washington. Huko New York, waandamanaji walipeana mikono na kushikamana kama "mkufu", wengine walipungapunga bendera za taifa za Marekani na nchi kadhaa za Latin Amerika, na wengine waliinua juu mabango yaliyosemeka "sisi ni wamarekani".

Kauli mbiu ya maandamano ya siku hiyo ni "siku isiyo na wahamiaji", waandalizi wa maandamano waliwataka wahamiaji kutoka nje na watu wanaounga mkono kulinda haki za wahamiaji wafanye mgomo wa kazi, wasinunue vitu, na kuwataka watoto wao kugoma masomo ili kuonesha umuhimu wa wahamiaji katika uchumi wa Marekani.

Mhamiaji mmoja wa Mexico alisema, sisi siyo wahalifu, tulifanya kazi kwa bidii na kutoa mchango mkubwa sana kwa uchumi wa Marekani. Leo hatufanyi kazi, kwani tunawataka watawala wajue kuwa, sisi wahamiaji tumetoa mchango kwa uchumi wa nchi hiyo. Ni dhahiri kuwa, maneno aliyosema yameonesha nia ya waandamaji wengi. Mhamiaji mwingine kutoka nchi ya Latin Amerika alisema, watu walifika Marekani wakitaka kutafuta kazi na kupata pesa za kumudu maisha, na wengi wao wanafanya kazi zenye kipato cha chini kabisa.

Habari zilisema kuwa, maandamano ya siku hiyo yalileta athari kwa uendeshaji wa makampuni na maduka kadhaa nchini Marekani. Viwanda kadhaa vikubwa vya kusindika vyakula vya nyama vilisimamisha kazi kutokana na mgomo wa kazi, na migahawa kadhaa ya McDonald yalipunguza muda wao wa kazi. Maandamano makubwa ya Tarehe 1 Mei yalilifanya suala la wahamiaji haramu lililosababisha migongano mikubwa kati ya maofisa wa serikali ya Marekani lionekane dhahiri zaidi.

Chini ya uhimizaji wa wabunge wahafidhina wa chama cha publica, mwaka jana baraza la chini la bunge la Marekani lilipitisha mswada wa kupiga vita vikali uhamiaji haramu. Mswada huo si kama tu unataka kuwarudisha wahamiaji wote haramu nyumbani kwao, bali pia unataka kutoa adhabu kwa mtu yeyote aliyewaajiri au aliyewasaidia wahamiaji haramu. Mswada huo ulipotolewa ulikosolewa na watu wengi, ambao watu wengi waliona mswada huo ni mkali wa kupita kiasi cha kukosa hisia za binadamu hata kidogo, hata mswada huo ulisababisha maandamano makubwa katika sehemu mbalimbali nchini Marekani.

Hivi sasa serikali ya Bush inakabiliwa na changamoto kubwa ya namna ya kuwatendea wahamiaji haramu. Kwa upande mmoja, serikali ya Bush inapinga kutoa msamaha mkubwa kwa wahamiaji haramu, kwani kufanya hivyo kama kutoa tuzo kwa vitendo haramu; kwa upande mwingine, kutokana na maslahi ya idara za viwanda na biashara, serikali ya Bush inapinga pia mswada wa kuwaadhibu vikali wahamiaji haramu. Hivyo serikali ya Bush imetoa mpango wake wa kutoa viza za kazi kwa wahamiaji haramu na kuwaruhusu wawe raia wa Marekani kutokana na sifa zao za kazi. Hatua hiyo ya Bush inajaribu kutoa suluhu na wahafidhina wa bunge la taifa ili kutatua mapema iwezekanavyo suala la wahamiaji haramu.

Juu ya mgomo wa kazi wa tarehe 1 Mei, Msemaji wa Ikulu ya Marekani Bwana Scott McCllelan alisema, rais Bush hakubali mgomo wa kazi, kwani watu wanaweza kuchagua njia ya kiamani kwa kueleza maoni yao. Lakini rais Bush anatumanini kuwa bunge la taifa litaweza kupitisha mswada wa kufanya mageuzi kutoka pande zote kuhusu wahamiaji, ili aweze kusaini mswada huo na kuufanya uwe sheria.

Na mwanzoni mwa mwezi uliopita, wabunge wa chama cha democratic na wabunge kadhaa wenye msimamo kati wa Baraza la juu la bunge la taifa la Marekani walitoa mswada wa pendekezo lao ambao unafanana na lile la serikali ya Bush.