Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-02 20:41:22    
Benki za makazi vijijini zitaanzishwa miaka 10 ijayo

cri

Vyama vya ushirika wa fedha vya vijijini vinajitahidi kugawanya hatari ya utoaji mikopo katika ngazi 5 kwa muda wa mwaka mmoja hivi, kusimamia utaratibu wa usimamizi kwa miaka 3 na kuanzisha benki zenye umaalumu wa makazi ya vijijini hatua kwa hatua katika miaka 5 hadi miaka 10 ijayo.

Hayo ni maneno aliyoyasema naibu mkurugenzi wa kamati ya usimamizi wa sekta ya benki ya China Bw. Tang Shuangning alipotoa mhadhara tarehe 22 kwenye mkutano wa baraza la ngazi ya juu la mageuzi ya mambo ya fedha la China.

Bw. Tang Shuangning alisema, kumaliza kazi za ugawanyaji wa ngazi 5 kwa muda wa mwaka mmoja ni pamoja na kufahamu vizuri hali halisi ya hatari katika mambo ya fedha ya vyama vya ushirika vya sehemu za vijijini ili kuweka mitaji ya kutosha na kufanikisha utekelezaji wa mpango hatua kwa hatua.

Kunyoosha utaratibu kwa muda wa miaka 3 ni kunyoosha utaratibu wa usimamizi wa vyama vya ushirika wa fedha vya ngazi ya mikoa, wilaya na vya makazi ya sehemu za vijijini. Hivi sasa kuna matatizo ya kutofahamika vizuri lengo na maeneo ya majukumu ya vyama vya ushirika wa fedha vya ngazi ya mikoa katika utaratibu wa usimamizi wa mambo ya fedha ya vyama vya ushirika. Kwa kufuata kanuni za kunufaisha maendeleo ya uchumi wa huko na kujenga vijiji vya aina mpya, vyama vya ushirika wa fedha vya ngazi ya mikoa vinaruhusiwa kufanya utafiti wa kutafuta mfumo wa usimamizi unaoendana na hali halisi ya huko na kutatua suala hilo kwa muda wa miaka mitatu hivi.

Bw. Tang Shuangning alisema, msingi wa ushirikiano wa mambo ya fedha katika sehemu za vijijini ni hafifu, vyama vya ushirika vinadaiwa madeni mengi, tena kuna matatizo na migongano mingi yaliyotokea katika muda mrefu uliopita, na haiwezekani kutatuliwa kabisa katika muda mfupi. Hata hivyo, tunapaswa kuona kuwa baada ya mageuzi katika miaka zaidi ya miwili iliyopita, umewekwa msingi mzuri, kwa kufuata hali ya maendeleo ya hivi sasa na kutekeleza vizuri sera zilizopo sasa, lengo la kuanzisha benki za kisasa za makazi ya sehemu za vijijini kwa kutegemea jitihada ya vyama vya ushirika wa fedha vya sehemu za vijijini na uungaji mkono wa kutoka nje, litaweza kutimizwa hatua kwa hatua kwa muda wa kutoka miaka 5 hadi miaka 10.

Hadi mwishoni mwa mwaka uliopita, jumla ya mikopo ya fedha iliyotolewa na vyama vya ushirika wa fedha vya sehemu za vijijini kwa wakulima ilizidi Yuan za Renminbi trioni 2 kwa mara ya kwanaza, ambapo mikopo ya fedha iliyotolewa moja kwa moja kwa wakulima ilichukua 80% ya jumla ya mikopo iliyotolewa.

Katika mwaka uliopita, familia milioni 70 zilipata uungaji mkono wa mikopo zikichukua 31% ya jumla ya idadi ya familia za wakulima nchini China, ambayo ni kiasi cha milioni 220, na ni karibu 60% ya familia za wakulima wanaohitaji mikopo ya fedha na kutimiza masharti ya utoaji mikopo, ambapo wakulima zaidi ya milioni 200 walinufaika kutokana na mikopo.

Mwishoni mwa miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu, fedha za mikopo ambazo hazijarudishwa kwa vyama vya ushirika zilifikia Yuan trioni 2 na bilioni 389.5, kati yake fedha za kikopo ya kilimo ambazo hazijarudishwa zilifikia trioni 1 na bilioni 166.8, wakati fedha za mikopo ya familia za wakulima, ambazo bado hazijarudishwa ni kiasi cha Yuan bilioni 899.8.

Bw. Tang Shuangning alisema, kutokana na matatizo mbalimbali ya kiutaratibu, kimfumo na kisera, hivi sasa mitaji ya vyama vya ushirika wa fedha vya sehemu za vijijini siyo mizuri, mzigo wa mambo ya fedha ni mzito, uwezo wa kufidia hatari ya mikopo ni mdogo, marekebisho ya wakuu wa vyama vya ushirika hayakuwa kamili, mambo ambayo yamezuia maendeleo na utoaji huduma ya soko la sarafu la sehemu za vijijini.