Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-03 19:46:54    
Mapishi ya nyama ya ng'ombe pamoja na sosi ya kambamti

cri

Mahitaji

Nyama ya paja la ng'ombe gramu 300, pilipili mboga moja, pilipili hoho moja, yai moja, nusu ya kitunguu, vitunguu maji gramu 5, tangawizi gramu 5, vitunguu saumu vipande viwili, sosi ya kambamti gramu 20, mchuzi wa sosi gramu 5, sukari gramu 5, mafuta ya ufuta gramu 5, maji ya wanga gramu 15, kiasi kidogo cha pilipili manga na M.S.G

Njia

1. osha nyama ya ng'ombe, halafu uikate iwe vipande virefu, weka kwenye bakuli moja, koroga pamoja na yai liliyokorogwa, mafuta vijiko viwili, wanga na mchuzi wa soya. Kata pilipili mboga na pilipili hoho ziwe vipande, uziweke kwenye maji joto, tia chumvi kidogo, halafu zipakue na kukausha. Kata kitunguu kiwe vipande.

2. pasha moto na tia mafuta kwenye sufuria, mpaka yawe nyuzi ya asilimia 60 tia vipande vya nyama ya ng'ombe, korogakoroga halafu tia vipande vya pilipili mboga, pilipili hoho na kitunguu, korogakoroga ipakue.

3. tia mafuta kidogo kwenye sufuria pasha moto, tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi , korogakoroga halafu tia vitu vilivyopakuliwa kabla ya hapo, tia mchuzi wa soya, sukari, pilipili manga, M.S.G, mimina maji kidogo korogakoroga halafu tia sosi ya kambamti na mimina maji ya wanga na kasha korogakoroga, kabla ya kupakuliwa mimina mafuta ya ufuta. Mpaka hapo kitoweo hicho kipo tayari kuliwa.